Tahadhari kwa Zitto Kabwe

Tahadhari kwa Zitto Kabwe

Nomile

Member
Joined
Dec 5, 2012
Posts
99
Reaction score
122
Naam, Bwana Zitto Sikia haya ninayoenda kuandika hapa. Siasa zetu katika nchi za kiafrika ni zaidi ya Siasa.Ujenzi wa chama si kazi ya lelemama kwanza inahitaji watu makini,pesa,mipango mkakati iliyo madhubuti na uwanja sahihi wa kufanyia siasa zenyewe.

Siasa zetu za kiafrika sio sawa na zile za nchi zilizoendelea, kwamba sera pekee zinaweza kumshawishi mtu akuunge mkono katika chama chako, hapa kwetu unajua vyama vyetu wafuasi wengi wana matarajio ya muda mfupi na wanalenga kupata jambo fulani kipindi fulanI, katika muktadha huu utakuta Migogoro mingi inaibuka kwenye vyama hivi ambavyo havina rasilimali za kutosha mwisho mgogoro ukikomaa utakuta chama kinakufa kifo cha kawaida, na hapa sina maana chama kifutwe kwa msajiri.

Hakika kuna matarajio uliyonayo moyoni mwako lakini hayataweza kutokea katika siasa za ACT maana sasa wale waliokupokea wanahitaji muda ili waanze kupishana na wewe na hapo ndio utajikuta unakuwa Easy target.Chama kikiyumba utakuwa unajiona unalo jukumu la kurekebisha mambo na hapo Zitto utakuwa hauna amani tena moyoni utakuwa unajutia yale yaliyotokea na yanayobeba historia ya maisha yako kisiasa.

Sasa jukumu unalo tena zito,kipindi hiki unapoangalia mbele kwenye uchaguzi mkuu ujao,hakika itakuwa ni kazi ngumu mno wewe kurudi bungeni katika kipindi hicho ijapokuwa unaweza ukadhani ni rahisi lakini nataka nikwambie kwamba si rahisi maana kazi uliyonayo itakuwa kukijenga chama na si kujenga himaya yako ndani ya ACT,Akina Mwigamba naweza kusema hakuna chemistry kati yako na Mwigamba na hilo litakuwa tatizo la msingi.

Mwigamba anaamini katika mawazo yake na wewe pia, kamwe hamtaweza ku compromise pindi mkitofautiana katika harakati zenu mlizo anza.

Safari hii uliyoianza ni tofauti kabisa na ile uliyoianza pale ulipokua na umri wa miaka 16. kipindi hicho ulipata mafanikio mengi ndani ya siasa na nje ya siasa, ulipewa nafasi na chama chako kutenda majukumu makubwa,lkn safari hii ukiwa na umri wa 39 umeanza safari mpya yenye mashaka mengi.
 
Anaamini atakijenga chama chake kwa hisani ya CCM, hiyo ndo turufu pekee aliyonayo. Lakini akumbuke wakiona jitihada zake zinakwama watamtupa kama kondom iliyotumika!
 
Zitto atakuja sana kumlaumu Kitila Mkumbo. Mambo yakianza kukwama tu Zitto ataanza kumtafuta mchawi wake. Na hapa ndipo Kitila Mkumbo atakapoanza kutofautiana na Zitto.
 
Naam, Bwana Zitto Sikia haya ninayoenda kuandika hapa. Siasa zetu katika nchi za kiafrika ni zaidi ya Siasa. ujenzi wa chama si kazi ya lelemama kwanza inahitaji watu makini,pesa,mipango mkakati iliyomadhubuti na uwanja sahihi wa kufanyia siasa zenyewe.

Siasa zetu za kiafrika sio sawa na zile za nchi zilizoendelea, kwamba sera pekee zinaweza kumshawishi mtu akuunge mkono katika chama chako, hapa kwetu unajua vyama vyetu wafuasi wengi wanamatarajio ya mda mfupi na wanalenga kupata jambo flani kipindi flan, katika muktada huu utakuta Migogoro mingi inaibuka kwenye vyama hivi ambavyo havina rasilimali za kotosha mwisho mgogoro ukikomaa utakuta chama kinakufa kifo cha kawaida, na hapa sina maana chama kifutwe kwa msajiri.

Hakika kuna matarajio uliyonayo moyoni mwako lakini hayataweza kutokea katika siasa za ACT maana sasa wale waliokupokea wanahitaji mda ili waanze kipishana na wewe na hapo ndo utajikuta unakuwa Easy target. chama kikiyumba utakuwa unajiona unalojukumu la kurekebisha mambo na hapo zitto utakuwa hauna amani tena moyoni utakuwa unajutia yale yaliyotokea na yanayobeba historia ya maisha yako kisiasa.

Sasa jukumu unalo tena zito,kipindi hiki unapo angalia mbele kwenye uchaguzi mkuu ujao,hakika itakuwa ni kazi ngumu mno wewe kurudi bungeni katika kipindi hicho ijapokuwa unaweza ukadhani ni rahisi lkn nataka nikwambie kwamba si rahisi maana kazi uliyonayo itakuwa kukijenga chama na si kujenga himaya yako ndani ya ACT,Akina Mwigamba naweza kusema hakuna chemistry katinyako na Mwigamba na hilo litakuwa tatizo la msingi.Mwigamba anaamini katika mawazo yake na wewe pia, kamwe hamtaweza ku compromise pindi mkitofaitiana katika harakati zenu mlizo anza.

Safari hii uliyoianza ni tofauti kabisa na ile uliyoianza pale ulipokua na umri wa miaka 16. kipindi hicho ulipata mahanikio mengi ndani ya siasa na nje ya siasa, ulipewa nafasi na chama chako kutenda majukumu makubwa,lkn safari hii ukiwa na umri wa 39 umeanza safari mpya yenye mashaka mengi

Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...
 
zitto anadhani kejenga chama cha siasa ni mchezo haya sasa kazi kwako
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...
Hivi maelengo ya ACT kama chama cha upinzani ni yepi? Ni kwa namna gani kitakuwa tishio kwa CHADEMA? Naomba kufahamishwa.
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...

kwani act nia yao ni kuwa chama kikuu cha upinzani au kushika dola?
kama dhamira yao nikuwa chama kikuu cha upinzani waendelee kuitishia chadema
ila kama wanalengo la kushika dola itabidi wawe tishio kwa ccm
 
ACT sawa....sawa ....kabisa.Vizuri nawe ukajiunga na UKAWA kutupunguzia mzigo sisi wenye elimu ndogo ya siasa....Umoja ni Nguvu na Uhuru ni Kazi.
 
Ushauri wako na tahadhari ni muhimu. Zitto ana anadhani atarudi tu bungeni kirahisi. Thubutu anatakiwa atoke jasho!
 
Duh leo bavicha naona hamjakunywa chai wala lunch, zitto kawamaliza kabisa maana mnapokezana tu kufungua uzi wake, mara Facebook mara twitter mara Jf, bundle leo zinalipwa ufipa kwa foleni,
 
Anaamini atakijenga chama chake kwa hisani ya CCM, hiyo ndo turufu pekee aliyonayo. Lakini akumbuke wakiona jitihada zake zinakwama watamtupa kama kondom iliyotumika!

Nina hakika ZZK hatakuwa mgombea wa urais wa ACT ila mfadhiri wao mkuu ambae pia amekalia kuti kavu CCM. Yeye anadhani asipopitishwa na CCM atakimbilia ACT na kushinda, huoni mashehe tayari wameanza kuwa karibu nae.MARK MY WORD.
 
Duh leo bavicha naona hamjakunywa chai wala lunch, zitto kawamaliza kabisa maana mnapokezana tu kufungua uzi wake, mara Facebook mara twitter mara Jf, bundle leo zinalipwa ufipa kwa foleni,

Gari lilikuwa service na sasa tumemwaga oil chafu by lissu

swissme
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...
Inaonekana unatumiwa na CCM, Kwa nini useme ACT itakuwa tishio kwa CHADEMA? Unatakiwa kujenga hoja. Kwani kuna mashindano ya vyama?
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...

Hakuna watu wenye kampeni mbaya na hatari kama wachaga, jiulize hata serikalini zile nafasi nyeti wameshika wao hasa za lesa. Wafanyabiashara wengi kwenye majiji ni wachaga. Hata barabara ya lami ilianza Dar- Moshi-Arusha. Jiulize ni kwanini. Kwahiyo ogopa sana hawa wachaga hata Nyerere walimsumbua sana akina Mtei, Mareale. Vilevile angalia vyama vingi vya upinzani wenyeviti wao ni toka Kilimanjaro. Mbatia, Mbowe, Mrema, Peter Mziray sijajua huyu Makaidi anatoka mkoa gani. Na wachaga hata walioko ccm tu wanapenda siku moja watoe Rais na wana umoja sana kuliko makabila mengine labda wanaowafuta ni Wahaya na Wanyakyusa. Makabila mengine hatuna huo umoja.
 
Zito atakuwa kama Lamwai au mrema. Anadhani chama kinajengwa kwa cku moja. Kwanza mpaka sasa amesha choka kwani zile transactions kutoka ccm hakuna tena
 
Hakuna watu wenye kampeni mbaya na hatari kama wachaga, jiulize hata serikalini zile nafasi nyeti wameshika wao hasa za lesa. Wafanyabiashara wengi kwenye majiji ni wachaga. Hata barabara ya lami ilianza Dar- Moshi-Arusha. Jiulize ni kwanini. Kwahiyo ogopa sana hawa wachaga hata Nyerere walimsumbua sana akina Mtei, Mareale. Vilevile angalia vyama vingi vya upinzani wenyeviti wao ni toka Kilimanjaro. Mbatia, Mbowe, Mrema, Peter Mziray sijajua huyu Makaidi anatoka mkoa gani. Na wachaga hata walioko ccm tu wanapenda siku moja watoe Rais na wana umoja sana kuliko makabila mengine labda wanaowafuta ni Wahaya na Wanyakyusa. Makabila mengine hatuna huo umoja.

Toa upuuzi wako kichwa panzi wewe.
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...

Siyo rahisi kivile!
 
Anaamini atakijenga chama chake kwa hisani ya CCM, hiyo ndo turufu pekee aliyonayo. Lakini akumbuke wakiona jitihada zake zinakwama watamtupa kama kondom iliyotumika!

Mliwaita CUF Kuwa ni CCM-B, leo mko nao
 
Back
Top Bottom