Tahadhari kwa Watumiaji wa Gesi ya Kupikia

Joined
Aug 23, 2025
Posts
8
Reaction score
9
TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA GESI YA KUPIKIA

Kama unatumia mtungi wa gesi jikoni, zingatia masharti haya ya usalama:

1. Kagua mara kwa mara
Angalia mtungi, bomba (pipe) na jiko lako kila mara.
Hakikisha havijachakaa, havijatoboka au kupasuka ili kuepuka uvujaji wa gesi.

2. Burner isiyo chakaa
Ikiwa unatumia mtungi mdogo, hakikisha burner/kiwashio chake hakijachakaa au kutoboka.
Burner ikizeeka huwa inavuja gesi na inaweza kusababisha ajali.

3. Ukisikia harufu ya gesi
Haraka fungua madirisha na milango ili gesi itoke nje.
Usiwake taa, swichi, wala moto wowote – unaweza kuchochea mlipuko.

4. Moto ukitokea
Zima gesi moja kwa moja kwa kufunga regulator ya mtungi endapo ni salama kufanya hivyo.

Tumia kizimia moto cha powder (Dry Chemical Fire Extinguisher) – ndicho kinachopendekezwa kuzima moto wa gesi (Class C).

Ikiwa moto ni mkubwa na umeshindikana, ondoka mara moja na piga simu 114 (Jeshi la Zimamoto na Uokoaji).

Tahadhari za ziada; unashauriwa yafuatayo:

5. Kama ikiwezekana Usihifadhi mtungi jikoni
Weka mtungi wa gesi nje au kama utashindwa kabisa weka sehemu yenye hewa ya kutosha.

6. Tumia vifaa sahihi tu
Tumia bomba maalumu la gesi (gas pipe) lenye ubora na linalokubalika. Badilisha kila baada ya miaka 2 au likichakaa.

7. Kagua vali (regulator)
Hakikisha regulator imefungwa vizuri na haina ulegevu.

8. Usiache gesi ikiwaka bila uangalizi
Epuka kuacha chakula jikoni bila mtu karibu.

9. Zima gesi kabisa baada ya matumizi
Baada ya kupika, funga regulator ya mtungi, siyo jiko pekee.

10. Weka kifaa cha kuzima moto (fire extinguisher)
Ni muhimu sana kuwa na kizimia moto cha powder (ABC extinguisher) jikoni.
 
Back
Top Bottom