DOKEZO Tahadhari kwa wanaonunua viwanja kupitia kampuni ya Ardhisol - Morogoro

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

TheMnyonge

JF-Expert Member
Mar 25, 2022
739
1,871
Kampuni ya Ardhisol ni moja ya kampuni zinazofanya shughuli za upimaji wa maeneo!

Hawa jamaa wamekuwa wakizunguka kwa wananchi na kuwashawishi wawape viwanja kwa ajili ya kuvipima, na wao hutangaza kuviuza ilhali wenye maeneo yao walishauza kama squatter!

Kuna maeneo mengi ya mtaa wa MAKUNGANYA, wamefanya kuwarubuni wananchi waliokwisha uza maeneo yao, ili tu wapate plots za kuuza kupitia pages zao na kwa kuwa wanunuzi hawajui kuwa maeneo yanayouzwa tayari yana watu basi inazaliwa migogoro isiyoisha!

Kwa wale ambao mnatarajia kununua viwanja KUPITIA KAMPUNI YA ARDHISOL, Makunganya Morogoro, chukueni TAHADHARI kubwa, ili msijelizwa na kuachiwa urithi wa migogoro!

Upigaji sector ya ardhi unarudi kwa kasi kubwa sana, tuchukue TAHADHARI.
 
Kwa wasioijua MAKUNGANYA, ni mtaa unaopatikana ndani ya kata ya MKUNDI, na ipo upande wa kushoto ukiwa unatoka Morogoro kuelekea DODOMA!

Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom