Majaribio ya Mifumo ya SGR, Wananchi wanaokaa karibu na reli wapewa tahadhari

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
251
595
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
SHIRIKA LA RELI TANZANIA

Dar es Salaam, Tarehe 05 Aprili 2023.
Shirika la Reli Tanzania – TRC linautaarifu umma kuwa kwa kushirikiana na mkandarasi wa ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR (Standard Gauge Railway) kampuni ya Yapi Merkezi wanaendelea na zoezi la majaribio ya mifumo ya Ishara na Mawasiliano yanayohusisha uwashaji umeme kwenye nguzo zilizopo katika reli ya kiwango cha kimataifa Dar es Salaam hadi Morogoro kuanzia siku ya alhamisi tarehe 6 Aprili 2023.

Wananchi wakiwemo waenda kwa miguu, waendesha vyombo vya moto na watumiaji wengine wa barabara wanaombwa kuwa makini na kuchukua tahadhari wanapokuwa karibu na miundombinu ya reli ya kiwango cha kimataifa.

Tahadhari zinazoshauriwa ni pamoja na; kuacha kutembea, kucheza au kuketi katika tuta la reli ya kiwango cha kimataifa, kuacha kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa tuta la reli, kuacha kugusa au kupanda nguzo zilizo pembezoni mwa reli, kuacha kushika nyaya za umeme ambazo zimegusa ardhi kwenye tuta la reli na kufuata maelekezo kutoka kwa wafanyakazi watakaokuwa kwenye vivuko vya reli.

Timu ya Mkandarasi na TRC inaendelea na matangazo kupitia vipeperushi na vipaza sauti katika maeneo yaliyo jirani na mradi kuanzia umbali wa kilomita 0 eneo la Stesheni jijini Dar es Salaam hadi kilomita 203 mkoani Morogoro ili kuwafahamisha wananchi kuhusu zoezi la majaribio ya mifumo.

Jamila Mbarouk
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano

TRC.jpg
 

Attachments

  • PRESS Kuendelea na Majaribio ya mifumo.pdf
    444.4 KB · Views: 2
Tahadhari zinazoshauriwa ni pamoja na; kuacha kutembea, kucheza au kuketi katika tuta la reli ya kiwango cha kimataifa, kuacha kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa tuta la reli,
Kuna masai mle kwenye tuta wanalinda ila huwa wanatembelewa na jamaa zao usiku jitahidini ujumbe huu uwafikie wasije wakaenda kuwatafuta jamaa zao wakanasia huko huko
 
Back
Top Bottom