Katika kipindi hiki cha uchaguzi tumeshuhudia nguvu kubwa ya CCM ikiyumba na kuifanya UKAWA kupiga hatua kubwa mbele.
Mambo haya tumeyashuhudia tangu pale mara baada ya Mh.Lowassa kujiunga na UKAWA na kupewa dhamana ya kugombea urais kupitia CHADEMA na kuungwa mkono na umoja wa vyama vinavyounda UKAWA.
Katika miji mingi tumeshuhudia UKAWA ikitikisa hasa katika majiji na miji mikubwa dhidi ya CCM na kuwapoteza kwa nafasi kubwa.
Ni kweli sehemu kubwa watu wanampokea na kuipokea UKAWA kama mkombozi na tumaini jipya juu yao haswa katika maeneo ambayo mh.Lowassa alifika na kuongea na wananchi.
Jambo hili ni zuri na lina faida kubwa sana dhidi ya CCM na kuwapoteza zaidi katika kila maeneo alipofika na hata kuwatumia vijana na vikundi vinavyo muunga mkono hakika vimesaidia sana haswa katika maeneo kama DSM,ARUSHA,MWANZA,MBEYA,KILIMANJARO,MTWARA na baadhi ya maeneo haswa katika miji mikubwa.
Lakini hali ni tofauti kwa maeneo ya ndani ya nchi ambayo ni vijijini kuna vijiji vingi hata kumfahamu au kutambua yanayoendelea hawajui harakati zinazoendelea na badala yake maeneo hayo CCM imejikita sana huko na kumnadi mgombea wao na kuwafanya wananchi kumtambua na kumpa nafasi.
CCM inatumia pia timu za vijana wanaomuunga mkono mh.Magufuli na kuwasambaza katika vijiji na maeneo mbalimbali ya nchi kitu ambacho UKAWA imejisahau na kuzisambaza timu hizo katika maeneo ambayo tayali wanaona hawana upinzani kama DSM,ARUSHA,MBEYA,MWANZA na baadhi ya maeneo, hii kitu naona ni kama kujiandalia matokeo mabaya na inanitisha kujiuliza je tuko makini kiasi gani juu ya haya.
Kama kweli UKAWA inahitaji kushika dola,yafaa kutumia siku hizi zilizobaki kwa umakini mkubwa pia kuwaunite vijana na makundi yanayomuunga mkono Lowassa na kwenda kupiga kampeni maeneo ya ndani ya nchi vinginevyo ni kujidanganya kula chakula kwa picha ya samaki huku ukiwaza unaipata ladha ile ya samaki.