TAHADHARI kwa mnaotaka kuanzisha biashara nchini Tanzania kwa sasa!

Jumax

Senior Member
Mar 4, 2017
117
229
Habari za muda wanajamvi,
Wahenga walinena Tahadhari kabla ya hatari au vilevile Kinga ni bora kuliko tiba, basi nami naomba nianze kutoa tahadhari kama ifuatavyo.

Najua ni watanzania wengi wenye nia ya kuanzisha biashara ili kuweza kujikwamua kiuchumi, lakini pia kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kuanzisha biashara yeyote ile ili iweze kuwa biashara yenye mafanikio.

Kwa hali ya nchi yetu ilivyo kwa sasa inamlazimu mtu anaetaka kuanzisha biashara kutafakari kwa kina zaidi juu ya changamoto zinazoikumba sekta ya biashara na uchumi kwa ujumla nchini.

Kwa ufupi tu nianze kwa kusema mzunguko wa pesa nchini umedhoofika kama si kupungua sana hadi kufikia kiwango ambacho kimeanza kutupa hofu wananchi mfano mzuri ni jinsi tunavyoona wafanyabiashara wanavyolalamika kwamba mauzo yamepungua sana kwa zaidi ya asilimia 50 yaani kama mwaka 2015 mtu alikuwa anaweza kuuza mpaka sh. ml 1 kwa siku basi sasa kupata tu laki 5 imekuwa ni kama ndoto. Msingi wa biashara yoyote ile ni wateja, sasa hivi wateja(wananchi) hawana pesa maana yake ni kwamba biashara lazima ife.

Kwa wewe unaepanga kufungua biashara kwa kipindi hiki embu jaribu kuanzisha biashara ambayo wateja watakuwa wana uhitaji wa bidhaa yako iwe ni kwa hiari au lazima. mfano Biashara ya chakula, mtu hawezi kuacha kula hata uchumi ushuke kufikia zero. n.k

Sina nia ya kumkatisha mtu tamaa ila nimejaribu kueleza kile nikionacho mm, nakaribisha maoni na sikatai kukosolewa, Ahsanteni.
 
Unalengesha mashuwa kadri mawimbi yanavyokuja. Tulizowea kufunguwa biashara kwasababu fulani kafunguwa na mambo yake yana kwenda vizuri. Kipindi hiki ni cha kufikiri kwa makini kabla hujaanza biashara.
 
Zimbabwe yenyewe ambaye ambayo uchumi wake ushakufa lakini watu bado wanafanya biashara, sembuse nchi bikra kama bongo, miporojo kibao tena iliyojaa mihemko ya kibavicha

Duuhhh kazi kweli kweli.

Hili ni jukwaa la Biashara, watu wanabadirishana uzoefu, weledi na maarifa Ili waweze kufikia malengo. Badala ya kujenga hoja ima kusapoti au kukanusha unatuletea UHARO. Nampa pole yule aliekubeba miezi 9 tumboni.
 
Habari za muda wanajamvi,
Wahenga walinena Tahadhari kabla ya hatari au vilevile Kinga ni bora kuliko tiba, basi nami naomba nianze kutoa tahadhari kama ifuatavyo.

Najua ni watanzania wengi wenye nia ya kuanzisha biashara ili kuweza kujikwamua kiuchumi, lakini pia kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kuanzisha biashara yeyote ile ili iweze kuwa biashara yenye mafanikio.

Kwa hali ya nchi yetu ilivyo kwa sasa inamlazimu mtu anaetaka kuanzisha biashara kutafakari kwa kina zaidi juu ya changamoto zinazoikumba sekta ya biashara na uchumi kwa ujumla nchini.

Kwa ufupi tu nianze kwa kusema mzunguko wa pesa nchini umedhoofika kama si kupungua sana hadi kufikia kiwango ambacho kimeanza kutupa hofu wananchi mfano mzuri ni jinsi tunavyoona wafanyabiashara wanavyolalamika kwamba mauzo yamepungua sana kwa zaidi ya asilimia 50 yaani kama mwaka 2015 mtu alikuwa anaweza kuuza mpaka sh. ml 1 kwa siku basi sasa kupata tu laki 5 imekuwa ni kama ndoto. Msingi wa biashara yoyote ile ni wateja, sasa hivi wateja(wananchi) hawana pesa maana yake ni kwamba biashara lazima ife.

Kwa wewe unaepanga kufungua biashara kwa kipindi hiki embu jaribu kuanzisha biashara ambayo wateja watakuwa wana uhitaji wa bidhaa yako iwe ni kwa hiari au lazima. mfano Biashara ya chakula, mtu hawezi kuacha kula hata uchumi ushuke kufikia zero. n.k

Sina nia ya kumkatisha mtu tamaa ila nimejaribu kueleza kile nikionacho mm, nakaribisha maoni na sikatai kukosolewa, Ahsanteni.
True mkuu hata show room za magali zimepungua..
 
Baada ya kuona avatar yako nikajua utakua na hoja tofauti mkuu. Hapo umeenda kinyume kabisa na muasisi wa hiyo ES/BI. Jamaa yako Kiyosaki anaamini kwenye matatizo ndio real entreprenuers emerges
 
Back
Top Bottom