Tahadhari Kubwa kwa CHADEMA

Tahadhari Kubwa kwa CHADEMA

ninavyozidi soma hli sakata la CHADEMA nagundua kitu kimoja. Nacho ni UDHAIFU MKUBWA WA MBOWE.. Ni very WEAK..na Mnykika amrejeshee yale maneno ya UDHAIFU.

Nikwavile MBOWE hana BEI km hao wengine ndomana!
 
Hakuna mwanadamu asie na mapungugu bali Mungu pekee.Maamuzi ya kumvua zito na mkumbo vyeo sio wa mbowe.Acha kupotosha.
ninavyozidi soma hli sakata la CHADEMA nagundua kitu kimoja. Nacho ni UDHAIFU MKUBWA WA MBOWE.. Ni very WEAK..na Mnykika amrejeshee yale maneno ya UDHAIFU.
 
Najaribu kutafakari nasindwa kuona mantiki ya bandiko hili!!!! Eti Zitto afukuzwe kwa tuhuma za waraka au kwa tuhuma hewa ambazo wewe unadhani zinaweza kumfukuzisha?? Hizo tuhuma nyingine nje ya waraka wa Mkumbo hazikubaliki maana hata CC ya Chadema haikuziona kuwa zinaukweli.

Nachobaini kwako ni hofu ambayo wengi tunayo. Dhana ambayo tumeijenga kwenye akili zetu kuwa bila hawa au wale Chadema itakufa au itatumiwa na CCM. Udhaifu huu unatukosesha hata uwezo wa kuchambua na kuhoji.

Zitto kuwekwa kando hasa na uongozi ambao yeye anadhani hautendi haki ni sahihi kwani kuendelea kuwa kwenye wadhifa wake kwenye utawala anaoupinga ni kubariki matendo ya utawala ule. Ni vema ajitenge ili ajiandae hapo baadae kama wanachama tutamuona anafaa awe mwenyekiti tumpe.

Kumfukuza kwa waraka ambao umemtaja kwa nafsi ya tatu {yeye} si kumtendea haki. Na nikwambie kama Chadema itamuhukumu kwa dhana na tuhuma ambazo haziko wazi naamini tutarudi nyuma saaana.
 
Baada ya maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu ya Chadema hapo juzi, tumeuona utetezi walioutoa Zitto Kabwe na Kitila. Kuna mambo kadhaa ambayo nimeyaona yanahitaji kupewa umaanani kwa tahadhari kubwa sana. Kwanza niseme kuwa, kama waraka ulioitwa Waraka wa siri ndio uliotumiwa kumvua Zitto madaraka, basi Zitto hakutendewa haki maana waraka, kama wengi mlivyousoma, haukuonyesha kumshirikisha Zitto, angaau kwa hatua ile. Ila, kama alivyoeleza Zitto, kama amevuliwa madaraka kwa sababu zile alizozitaja, zile za kutoshirikiana na viongozi wnenzake wakuu, basi hukumu hiyo ni ya haki maana Zitto amekuwa akifanya siasa za ubnafsi, za kukijengea chama makundi na kujijenga yeye binafsi. Hizo ni siasa chafu na mtu wa namna hiyo hafai.

Sasa, tahadhari kwa Chadema ni hii: Ni dhahiri kuwa kumwajibisha Zitto Kabwe ulikuwa ni uamuzi mzuri ambao binafsi nilikuwa niiusubiria kwa muda mrefu. Lakini, kama mlivyomsikia Zitto na Mkumbo, wameamua kuitumia nafasi hiyo kwa kuzisaka huruma za wananchi na wapenzi wa Chadema, na wameamua kuitumia nafasi hiyo kujijenga zaidi kisiasa na mwisho kutekeleza tamaa zao. Ndio maana, licha ya Mkumbo kushirikiana na Mwigamba kuandaa waraka huo, waliona hawana haja ya kumshirikisha katika press conference, na waliamua hata kutomzungumzia. Kwa ujumla wamemtupia kapuni na wameamua kujipambanua wao wenyewe kama maswahiba, wanaojijenga kwa pamoja kisiasa.

Ni dhahiri kuwa, hatua hii ya awali ya Kamati Kuu ndiyo ilikuwa hatua muhimu katika kukiokoa Chama na kuyaweka hai matumaini ya Watanzania ya kuing'oa CCM mwaka 2015. Lakini, ni vyema mkaelewa pia, hatua hii muhimu yaweza ikawa ni chanzo ya maporomoko makubwa zaidi kwa Chadema kama haitasaidia kumfungia Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo Speed Governor. Hili ni kwa sababu, sasa wamejipambanua kama wapigania haki ndani ya chama (na si wapigania vyeo, kama walivyo) na sasa watakihujumu chama waziwazi katika majukwaa ya chama, kwa hoja ya uhuru wa kidemokrasia. Wanajua kuwa, wameshafanikiwa kuwafanya wananchi wawaone kuwa wanaonewa na uongozi wa Chadema; linalofuata sasa, watafanya hujuma nyingi za wazi dhidi ya uongozi, kwa sababu wanajua watu wameshawachukuliwa kama waonewa kwenye chama.

Ni kweli kuwa, bado chama hakijafikia hitimisho ya swala hili maana kimewapa watu hawa siku 14 wajitetee. Mkumbuke kuwa, wasaliti wana nguvu zaidi wakiwa ndani ya chama kuliko wawapo nje. Kama kweli Zitto amekuwa akitumiwa na CCM, basi kwa hao CCM kutakuwa na ushindi bado, ikiwa Zitto ataendelea kuwa ndani ya Chadema. CCM wanamhitaji Zitto akiwa ndani ya Chadema, maana wanajua hawana uwezo kuivuruga Chadema bila mamluki wao ndani ya Chadema. Ikiwezekana, chama kichukue hatua zaidi mapema ili kuhakikisha tunaondoa unafki huu mapema. Mkichelewa, Zitto na Kitila wataibua matatizo mengine makubwa karibu zaidi na uchaguzi Mkuu wa 2015 na hilo litakuwa na athari kubwa zaidi kwenye chama. Sisi tulio wanachama wa Chadema na waathirika wa siasa za CCM, tutaumia sana pale Zitto atakapotumika kukibomoa chama zaidi, hasa karibu na Uchaguzi Mkuu 2015. Chukueni tahadhari, Zitto asije akafifisha ndoto zetu za kuing'oa CCM.

Na nyinyi viongozi wakuu, onyesheni ukomavu wenu kwa kufanya na kuikuza demokrasia ndani ya Chama. Tunahitaji uhuru wa maoni (sio ule wa siri wa akina Mkumbo) uendelezwe chamani. Watu wawe huru kutoa maoni yao. Narudia, NI VYEMA ZITTO KABWE ACHUKULIWE HATUA ZAIDI, BILA KUJALI KUTAKUWA NA ATHARI GANI KWA SASA. NI VYEMA TUPATE MPASUKO MKUBWA SASA, KULIKO KUSUBIRI MPASUKO AWEZAO KUULETA SIKU CHACHE KABLA YA UCHAGUZI MKUU.

Dah natatizika sana nawe!!! Umekiri kuwa kama ni waraka umeotumika kuwavua nyadhifa zao basi CC itakuwa imetenda isivyo. Ila unaupata ujasiri wa kuishauri CC hiyo hiyo itende zaidi ya maamuzi ambayo wewe binafsi unayaona si sahihi kulingana za sababu zilizotolewa!!!

Nimeshangaa umewaza nini?? Kwahiyo unaishawishi CC iamue kwakuwa wewe umesema kwa kudhania 1, 2, 3, n.k?? CC imesema ni waraka uliotumika kuwavua sasa wewe unaesema ni sababu hizi au zile tukuelewe vipi?? Halafu kwanini uishi kwa dhana, kuwa akiachiwa itakuwa hivi au vile?? kwanini usidhani kuwa kama ataachiwa atafanya kile au hiki kizuri??
 
mkuu, hata mie ni mwanaCDM ila suingi mkono udikteta dhidi ya demokrasia ....kosa kubwa la zzk kwa mujibu wa viongozi wa juu wa CDM ni yeye 'kuutamani' uwenyekiti, usisahau hili halijaanza leo, ni muendelezo tu wa hekaya zilezile toka atangaze nia kugombea kiti hicho. sasa baadhi ya wanachama tusiokuwa wanafki tunahoji, ina maana nafasi fulani ni kwa ajili ya watu fulani ndani ya chama na sio mchakato wa kidemokrasia tena kama kinavyojulikana chama chetu?! tofauti kati ya maccm na sisi ni ipi ambayo tunaipigania na kuiamini?! naunga mkono wanaCDM yeyote anayeona kuna haja ya kufanya mabadiliko ktk nafasi za juu za uongozi - tunataka mawazo mapya!!!!!!sio kujificha kwenye 'kauli' mbiu mpya ya usaliti, uhaini.

Mkuu, unachokisema 'udikteta' hakuna akipendaye kamwe. Ila kama mambo yanafanyika kama kwenye ule waraka tuliousoma, basi ni lazima hatua stahiki zichukuliwe. Dk. Kitila na Mwigamba, kwa kuuandika waraka ule, wanaonesha walikuwa wakiuhujumu uongozi kwa siri. Kama nia yao ilikuwa kuurekebisha uongozi, na kuweka uongozi madhubuti, kusingekuwa na usiri kwenye harakati zao. Harakati zao ni hujuma tupu, na hakuna chama au taasisi ambayo ingeweza kuzivumilia. Katika hili tusimlaumu Mbowe, kwa sababu sote tunaona jinsi alivyofanya kazi kubwa ya kukiimarisha chama, japo nakiri yeye kama binadamu wengine wote ana mapungufu yake.
 
Ambiere Lubua.
Ni kweli Zitto ametajwa au kuhisishwa na mengi, lakini bado tujue Zitto akisaidiwa kidogo anaweza kuwa na msaada mzuri kwa chama na Taifa.
Naamini adhabu alopewa inamuonesha kuwa njia apitiayo sio sahihi, naamini anaweza kujifunza na kubadilika. Kama akibadilika akiwa Zitto wa zamani basi, chama na Taifa litapata mtu safi.

Tuvute subira, tumpe muda ajitazame mwenyewe na labda atakuwa mwana Mpotevu.Nafikiri asifukuzwe unless hakuna njia ingine kumsaidia.

Mkuu, wasiwasi wangu ni kuwa akipewa nafasi zaidi atakidhoofisha chama na atafifisha ndoto zetu za kuing'oa CCM. Zitto amepewa nafasi nyingi sana ila amezitumia kwa kujenga migogoro zaidi, badala ya kujirudi. Hata hivyo, nakubaiana na wewe kuwa Zitto ni mwanasiasa mahiri ambaye anaweza kutumika vyema kukijenga chama, ikiwa yeye mwenyewe atakuwa tayari. Kwa ujumla, Zitto ni kama moto, unaweza kuutumia kupikia chakula au unaweza kuutumia kuunguza nyumba.
 
Baada ya maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu ya Chadema hapo juzi, tumeuona utetezi walioutoa Zitto Kabwe na Kitila. Kuna mambo kadhaa ambayo nimeyaona yanahitaji kupewa umaanani kwa tahadhari kubwa sana. Kwanza niseme kuwa, kama waraka ulioitwa Waraka wa siri ndio uliotumiwa kumvua Zitto madaraka, basi Zitto hakutendewa haki maana waraka, kama wengi mlivyousoma, haukuonyesha kumshirikisha Zitto, angaau kwa hatua ile. Ila, kama alivyoeleza Zitto, kama amevuliwa madaraka kwa sababu zile alizozitaja, zile za kutoshirikiana na viongozi wnenzake wakuu, basi hukumu hiyo ni ya haki maana Zitto amekuwa akifanya siasa za ubnafsi, za kukijengea chama makundi na kujijenga yeye binafsi. Hizo ni siasa chafu na mtu wa namna hiyo hafai.

Sasa, tahadhari kwa Chadema ni hii: Ni dhahiri kuwa kumwajibisha Zitto Kabwe ulikuwa ni uamuzi mzuri ambao binafsi nilikuwa niiusubiria kwa muda mrefu. Lakini, kama mlivyomsikia Zitto na Mkumbo, wameamua kuitumia nafasi hiyo kwa kuzisaka huruma za wananchi na wapenzi wa Chadema, na wameamua kuitumia nafasi hiyo kujijenga zaidi kisiasa na mwisho kutekeleza tamaa zao. Ndio maana, licha ya Mkumbo kushirikiana na Mwigamba kuandaa waraka huo, waliona hawana haja ya kumshirikisha katika press conference, na waliamua hata kutomzungumzia. Kwa ujumla wamemtupia kapuni na wameamua kujipambanua wao wenyewe kama maswahiba, wanaojijenga kwa pamoja kisiasa.

Ni dhahiri kuwa, hatua hii ya awali ya Kamati Kuu ndiyo ilikuwa hatua muhimu katika kukiokoa Chama na kuyaweka hai matumaini ya Watanzania ya kuing'oa CCM mwaka 2015. Lakini, ni vyema mkaelewa pia, hatua hii muhimu yaweza ikawa ni chanzo ya maporomoko makubwa zaidi kwa Chadema kama haitasaidia kumfungia Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo Speed Governor. Hili ni kwa sababu, sasa wamejipambanua kama wapigania haki ndani ya chama (na si wapigania vyeo, kama walivyo) na sasa watakihujumu chama waziwazi katika majukwaa ya chama, kwa hoja ya uhuru wa kidemokrasia. Wanajua kuwa, wameshafanikiwa kuwafanya wananchi wawaone kuwa wanaonewa na uongozi wa Chadema; linalofuata sasa, watafanya hujuma nyingi za wazi dhidi ya uongozi, kwa sababu wanajua watu wameshawachukuliwa kama waonewa kwenye chama.

Ni kweli kuwa, bado chama hakijafikia hitimisho ya swala hili maana kimewapa watu hawa siku 14 wajitetee. Mkumbuke kuwa, wasaliti wana nguvu zaidi wakiwa ndani ya chama kuliko wawapo nje. Kama kweli Zitto amekuwa akitumiwa na CCM, basi kwa hao CCM kutakuwa na ushindi bado, ikiwa Zitto ataendelea kuwa ndani ya Chadema. CCM wanamhitaji Zitto akiwa ndani ya Chadema, maana wanajua hawana uwezo kuivuruga Chadema bila mamluki wao ndani ya Chadema. Ikiwezekana, chama kichukue hatua zaidi mapema ili kuhakikisha tunaondoa unafki huu mapema. Mkichelewa, Zitto na Kitila wataibua matatizo mengine makubwa karibu zaidi na uchaguzi Mkuu wa 2015 na hilo litakuwa na athari kubwa zaidi kwenye chama. Sisi tulio wanachama wa Chadema na waathirika wa siasa za CCM, tutaumia sana pale Zitto atakapotumika kukibomoa chama zaidi, hasa karibu na Uchaguzi Mkuu 2015. Chukueni tahadhari, Zitto asije akafifisha ndoto zetu za kuing'oa CCM.

Na nyinyi viongozi wakuu, onyesheni ukomavu wenu kwa kufanya na kuikuza demokrasia ndani ya Chama. Tunahitaji uhuru wa maoni (sio ule wa siri wa akina Mkumbo) uendelezwe chamani. Watu wawe huru kutoa maoni yao. Narudia, NI VYEMA ZITTO KABWE ACHUKULIWE HATUA ZAIDI, BILA KUJALI KUTAKUWA NA ATHARI GANI KWA SASA. NI VYEMA TUPATE MPASUKO MKUBWA SASA, KULIKO KUSUBIRI MPASUKO AWEZAO KUULETA SIKU CHACHE KABLA YA UCHAGUZI MKUU.

Zitto amepofushwa na ukwasi mkubwa alionao kupitia Sisiem, tena kwa njia haramu. Anaubia na mafisadi, na viongozi wetu wakuu. Wamemwezesha kujipatia umaarufu kwa michezo yao ya kuigiza ambayo hata siku moja haikufika mwisho mfano kweli zzk afanye kukusanya kura ya kukosa imani na waziri mkuu?! au ni kamchezo na mfalme? Afuatilie pesa za Uswis, unaamini nk. Kama taarifa inayotembea mtandaoni sasa kuwa alishiriki bomu la Arusha, je unafikiri yupo level gani?

Mkumbo ameuweka weledi wake kwa rehani ya posho ya laki mbili mbili kila mwezi na urafiki wa mtu asiyefaa. Biblia ina ushauri mzuri sana wa marafiki kwenye mithali na Joshua bin Sira. Bado anashindwa kuchagua njia anashindwa kumkana rafiki yake, lakini anajua anakoenda huyu rafiki yake huyu zzk na marafiki zake akina mwigulu nchemba si kuzuri. Hata hivyo anakufa tai shingoni.

Mwigamba, nashindwa kumwelewa, sintashangaa kama akafanana na Ben Saa Nane kwa kuwatosa MP7. Ule mtego wa Lema Arusha nadhani ni usanii tu. MKUMBO naye si ajabu ni hivyo hivyo tu wameamua kumshika Mbogo kwa pembe

Ninaamini siku ya kikao kingine zzk atachinjiwa baharini
.
 
Zzk hana nia njema na cdm tuliyaona matatizo yake meng toka muda mrefu bora angefukuzwa cku nying amekuwa akikwamisha harakati cku nying kwa ubinafsi wake wa siasa kufanya siasa yake kwa lengo la kujitafutia umaru binafsi
 
Mkuu bandiko lako poa kabisa napendekeza asifukuzwa ila apewe adhabu na kuwa adhabu ile iwe under Mou akivunja makubaliano kwa heir mwalimu.cc wasipepese macho wamuambie yeye ni kibaraka wa ccm
 
Hivi mkuu huna kazi ya kufanya unashinda jf kujaza server tuu, kama huna cha kufanya njoo site yangu hapa kinyerezi nkupe kazi ya kusimamia wapiga tofali.

pole ndugu yangu... kwa taarifa yako sipo tanzania.
 
Ambiere Lubua.
Ni kweli Zitto ametajwa au kuhisishwa na mengi, lakini bado tujue Zitto akisaidiwa kidogo anaweza kuwa na msaada mzuri kwa chama na Taifa.
Naamini adhabu alopewa inamuonesha kuwa njia apitiayo sio sahihi, naamini anaweza kujifunza na kubadilika. Kama akibadilika akiwa Zitto wa zamani basi, chama na Taifa litapata mtu safi.

Tuvute subira, tumpe muda ajitazame mwenyewe na labda atakuwa mwana Mpotevu.Nafikiri asifukuzwe unless hakuna njia ingine kumsaidia.

mkuu zzk habebeki adhabu anayostahili ni kufukuzwa uanachama kabisa.
 
Kijan unaonekana unaongozwa na mihemko ya mwili huku Ukuiacha akili ifanye kazi ikiwa 05% ! Mbona hakuna tuhuza za ZZK zilizo na VIVID & CONCRAT evidence makosa yake ? Mashtaka yenu yamejaa, INADAIWA,INASEMEKANA nk. Toeni ushahidi hai wa tuhuma kama yeye alivoutoa yeye jana ! Inaonekana cdm imegawanyika kikanda ktk mzozo huu ! Wachaga,kanda ya ziwa na Mbeya wako upande wa ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI,NDIYO MZEE na upde mwengine ni WANA MABADILIKO naWAPENDA DEMOCRASIA ! KIJANA RELAX ,FANYA ANALETICAL REVIEW kujua tatizo na c kusema nilihitaji ZZKafukuzwa kitambo !
 
Nadhani kwa kutazama tu ulichoandika hapa, wewe ndiye uonekanaye kutotumia akili kuliko mimi. Nadhani kama umesoma uzi wangu vizuri utaelewa kuwa nimezungumzia mapungufu ya pande zote kwa kifupi lakini kwa hoja. Tatizo mnakuwa mashabiki wa wanasiasa kadha wa kadha bila kuruhusu bongo zenu ziweze kuchambua mambo. Siasa sio soka au mchezo wa kuigiza, ushabki kwenye siasa ni maafa kwa jamii.
 
Back
Top Bottom