Tahadhari: Jihadharini na Tapeli mwenye namba hii...

Tahadhari: Jihadharini na Tapeli mwenye namba hii...

Mi bado sijaelewa hapa,mbona hamjaeleza na kuweka wazi mnamtumia hela kwa sababu zipi?
 
Nami alifanya hivyo hivyo. Akajitambulisha anaitwa John Bwire wa Raia Mwema. Akatuma sms kuwa tuwasiliane tu kwa sms maana yupo kwenye kikao halafu amepigiwa simu mjomba wake anaumwa sana hivyo nimtumie huyo mjomba wake pesa. kwa kuwa alitumia namba ya Voda nikacheki kwenye Mpesa nikakuta jina ni jingine kabisa tofauti na alilojitambulisha nalo. Ni wapuuzi sana hao.
 
Tuyuku pole sana mkuu

Jina gani ulilokutana nalo? Hiyo ndio staili anayoifanya huyu jamaa nami kanitajia kuwa yeye ni Mhariri wwa Mwananchi na akanitajia jina na akadai yuko kikaoni. Akataka nimsaidie kumtumia pesa mpwa wake then akitoka kikaoni atanirudishia. Mie nikamjibu niko nje ya mji a nitarudi late hours na simu yangu haikuwa na pesa hadi niweke mjini. Akaniambia nikirudi nimwambie ili anipe namba ya kutuma hiyo pesa.

Ajabu majira ya saa moja jioni akani-sms kuniuliza kama nimesharudi mjini ili anipe namba ya huy nduguye. hapo ndipo machale yaliponicheza maana mtu gani ana kikao saa 3 asubuhi hadi saa moja jioni hajatoka anasubiri mie nitoke shamba nimtumie pesa nduguyake. Nikaamua kutumia namba nyingine ya huyo Mhariri ambayo ninayo ili nijue kama kweli ni yeye au lah.

Mhariri huyo akapokea na nilipompa habari akashangaa sana akasema mie ni mtu wa pili kumwambia kitu hicho kwa siku hiyohiyo moja.Yule tapeli bila kujua akapiga simu kuniambia kuwa kachepuka kikaoni kunicheki ili nimsaidie. Nikamwambia kwanza sauti tu sio ya yule mhariri. Jamaa akakata simu hapohapo na kuizima. Nikamtumia msg kuwa nimeshamripoti polisi ili atafutwe kwa utapeli. msg iliingia usiku wa manane na simu ikazimwa tena na sijui kama kaiwasha hadi leo.

Nimegundua wale wote wanaoweka namba zao kwenye magazeti ni wahanga wa hii kitu na namba zao na majina yanatumiwa na matapeli. Inabidi kuchukua tahadhari sana
 
Back
Top Bottom