TAHADHARI: Airtel waanza mtindo wa kuibia wateja wao

manning

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Posts
5,093
Reaction score
11,948
Jana nilijiunga na bundle ya Tsh 9999 kwa mwezi, ambayo ni bundle ya mwezi,cha ajabu kila nikipiga simu wananiambia huna salio Leo nimeenda ofisi za AIRRTEL binti niliyemkuta alikili kuwa anaona salio katika akaunti yangu, lakini alipocheki salio kwenye simu yangu alishangaa,akaanza kusema ulitumia na alipohesabu dakika nilizotumia akaona kweli nawadai na akashindwa kabisa kuelewa kilichotokea na akaniahidi ananifungulia malalamiko ili watu wa IT wachunguze kilichotokea.

Nilipotoka nje jamaa mmoja akanambia wewe ni wa tatu kulalamika leo tu na akaongezea kuwa bila shaka wanakopesha watu hawalipi, kwa hiyo wanajaribu kufidia kwa kuwakata wateja wakubwa wanaoweka hera nyingi, kwa sababu wanaolalamika ni ambao wameweka hera nyingi. Watumiaji wa Airtel kuweni macho.
 
Ni kweli kbsaa wamekuwa vinara wa wizi sasa mm jpili nilinunua muda wa maongezi wa 499 cha ajabu nikapata ujumbe niwasiliane na customer care bdae wakaniambia nitajulishwa nimefuatilia mpaka ss nimesalimu amri!! Ni wezi hawa na hawajui kusikiliza mteja. Jmn tusikubali kuibiwa hvhv tupaze sauti wahanga wote kwa pamoja ili vitendo hivi vikome.
 
Mie kila mwezi lzm niibiwe kati ya buku au zaid nasma lazima kwa maana ya lazima
 
Niliwaha nikaenda tigo nao wakaniibia nikahamia voda nao juzi nimeweka vocha lakini salio linapungua kila kukicha hata kama sijapiga sim ukiuliza wanakwambia eti kuna huduma umejiunga, sijui awamu hii nikimbilie wapi
 
mkuu mitandao hii yoote bila shaka imepokea maelekezo maalum kutoka chama fulani.
 
MKUU unaongelea hilo tuu. Kuna mtindo wa Ku-SWAP simcard na kubadilisha namba kisha kukuibia hela zilizoko kwenye airtel money halafu wezi hao, wanakopa ili usirudie kuweka hela kwenye airtel money. Wakimaliza wana-block line yako inakosa mawasiliano.Mimi nasubiri hatima yangu, labda niende tume ya malalamiko kule TCRA!
Jana nilijiunga na bundle ya Tsh 9999 kwa mwezi, ambayo ni bundle ya mwezi,cha ajabu kila nikipiga simu wananiambia huna salio Leo nimeenda ofisi za AIRRTEL binti niliyemkuta alikili kuwa anaona salio katika akaunti yangu, lakini alipocheki salio kwenye simu yangu alishangaa,akaanza kusema ulitumia na alipohesabu dakika nilizotumia akaona kweli nawadai na akashindwa kabisa kuelewa kilichotokea na akaniahidi ananifungulia malalamiko ili watu wa IT wachunguze kilichotokea.

Nilipotoka nje jamaa mmoja akanambia wewe ni wa tatu kulalamika leo tu na akaongezea kuwa bila shaka wanakopesha watu hawalipi, kwa hiyo wanajaribu kufidia kwa kuwakata wateja wakubwa wanaoweka hera nyingi, kwa sababu wanaolalamika ni ambao wameweka hera nyingi. Watumiaji wa Airtel kuweni macho.
 
MKUU unaongelea hilo tuu. Kuna mtindo wa Ku-SWAP simcard na kubadilisha namba kisha kukuibia hela zilizoko kwenye airtel money halafu wezi hao, wanakopa ili usirudie kuweka hela kwenye airtel money. Wakimaliza wana-block line yako inakosa mawasiliano.Mimi nasubiri hatima yangu, labda niende tume ya malalamiko kule TCRA!
mkuu umeniogopesha tangu jana laini yangu ya airtel inasumbua hata majina niliyosevu hayasomeki na nilijaribu kuingia kwenye simu banking inagoma na kuniandikia nikarekebishe taarifa zangu wakati nilirekebisha hivi karibuni.Hii ni hatari kubwa, airtel wasipokuwa makini watapoteza wateja.
 
Kuna siku ishanitokea,nlikua na bundle ila wakanikata salio zaid ya 8000.Nliwapigia hakuna walichoshughulikia.WIZI MTUPU
 
Jana nilijiunga na bundle ya Tsh 9999 kwa mwezi, ambayo ni bundle ya mwezi,cha ajabu kila nikipiga simu wananiambia huna salio Leo nimeenda ofisi za AIRRTEL binti niliyemkuta alikili kuwa anaona salio katika akaunti yangu, lakini alipocheki salio kwenye simu yangu alishangaa,akaanza kusema ulitumia na alipohesabu dakika nilizotumia akaona kweli nawadai na akashindwa kabisa kuelewa kilichotokea na akaniahidi ananifungulia malalamiko ili watu wa IT wachunguze kilichotokea.

Nilipotoka nje jamaa mmoja akanambia wewe ni wa tatu kulalamika leo tu na akaongezea kuwa bila shaka wanakopesha watu hawalipi, kwa hiyo wanajaribu kufidia kwa kuwakata wateja wakubwa wanaoweka hera nyingi, kwa sababu wanaolalamika ni ambao wameweka hera nyingi. Watumiaji wa Airtel kuweni macho.

Mimi Ni Mtumiaji Wa Mtandao Wa Airtel,Ila Sijawahi Kuweka HERA Kwenye Simu Yangu,Huwa Naweka HELA. Sijajua Bado Hizo HERA Mnazoibiwa Ni Kitu Gani.
 
Mamitandao ya simu yote ushuzi mtupu ila Airtel ni uharo tena wa mlevi wa kimpumu. Ni wezi balaa.
 
Kama hayajakukuta unaweza usiamini,mimi tangu juzi sipati huduma ya 3G kwenye line yangu ya airtel sasa jana nikawapgia wakasema watanitumia setting very soon mpaka kunakucha sikuona hiyo sms ya setting,jioni hii nikawapgia tena wakasema ili niweze kuongea nao inabdi nikatwe sh 60 nikakubali wakakata nikaongea nao jibu likawa lilelile kama la jana kuwa watanitumia setting mpaka mdaa saa 22:50 sijaona chochote.Ama kweli airtel ni baba lao kwa wizi.
 
Mkuu mimi nipo Mwanza, nilinunua vocha yao hao airtel nikakwangua vibaya ikabidi niende ofisini kwao, nilimkuta mdada anamajibu kama kameza uchafu, akadai siku yoyote salio langu litaongezeka nilisubir wiki 2 hakuna kitu nikachukia nikatupa laini chooni nikahamia mtandao mwingine, hao airtel ni wezi wa kutisha na wafanyakazi wao wanajiona utafikiri haweendi cho.oni, binafsi hata bure huo mtandao sirudi ng'oo hata waning'oe kucha pu.mbav airtel mxiiiiiuuuuuuuuuuuuu
 
Mimi Ni Mtumiaji Wa Mtandao Wa Airtel,Ila Sijawahi Kuweka HERA Kwenye Simu Yangu,Huwa Naweka HELA. Sijajua Bado Hizo HERA Mnazoibiwa Ni Kitu Gani.

Sijakuelewa mkuu , umesema huwaga unaweka hera halafu huwaga huweki hera. Kwa ujumla hawa jamaa wanatwanga kotekote, kwa kupitia muda wa maongezi hasa bando na pia kupitia airtel money. Kuwa makini na utatuelewa tu au zamu yako haijafika.
 
Back
Top Bottom