Tafuta wa saizi yako...

seifutz

Member
Jul 18, 2021
34
113
Mahusiano ni maisha, Katika Kipindi ambacho bado upo Duniani Huwezi kukwepa Kutafuta Mwenza,

Sasa Usifanye Kosa la Kulazimisha mapenzi, Yatakula Furaha yako ,Yatakula Muda wako na yatakuondolea hadi Mood ya kupambana Kimaisha.

Tafuta wa Saizi Yako.

Wa Saizi Yako ki uchumi
Wa saizi yako Ki Uwezo

Kutafuta mtu ambae unajuwa kabisa hutaweza kumhudumia hilo Kosa usifanye,

Kumtafuta mtu kwa sababu ana uwezo hilo kosa usifanye ni ngumu sana kukuthamini sababu watu kama wewe anaweza kuwapata wengi tu kupitia huo uchumi wake.

Simaanishi uwatafute masikini wenzio, Namaabisha tafuta wa Saizi Yako, Hamtasumbuana sana.

Kuna wanawake bateji ya Siku tu laki nzima wakati huo wewe Laki unaitafuta mwezi mzima, huyu hakufai.

Uzuri wowote unaoona kwa mwanamke unatumia pesa kama huna pesa tafuta wa saizi yako ,hakuna anaependa Shida Duniani,

Hili neno Huyu mwanamke anapenda Pesa , linatokana na Uchumi ulionao

Kuna mtu anampa mchepuko laki 5 ya matumizi na hawazi, kitu ambacho wewe huwezi kufanya

Kwani wewe huwa huoni unakutana na Mdada anatumia Iphone wewe una Infinix, Na unajuwa huyu Dada Hakusoma , hana kazi na hana Ajira yoyote, Basi yupo wa Saizi yake ambae haoni shida kutoa Iphone 12 pro max.

Ukitafuta wa Saizi yako hayo mambo ya Iphone hawezi kukwambia ,Sana sana atakwambia anaomba Tsh. 10000 akasuke hiyo inaweza kuwa sio shida kwako kuliko kuambiwa "baby naomba laki na nusu nikaset nywele"

Suruhisho na kuishi kwa Uhuru na Furaha katika mapenzi ni kupata wa Saizi yako.
 
Mwanamke ni binadamu yeyote anayemiliki uke.

Sasa kujue uke wa saizi yako unaupima kwa kipato?

Btw hiki kiumbe hakijawahi eleweka toka dunia iwe milki ya binadamu.

Sass sijui kiumbe kama hiki kisichoeleweka kwa vipimo vyovyote wewe u5atumia nini kujua kuwa hiki ni saizi yako

Tusaidie kifaa cha kupima saizi yako na utwambie na gharama kabisaa ili tujipange.
 
Kitu kimoja msichokifahamu ni kwamba kuna wanawake hawana hulka za kuomba omba Pesa, mpaka wewe unaweza kujistukia na kuanza kumuulizia kama kuna chochote anachohitaji, na bado akaendelea na msimamo wake wa kutokuhitaji chochote kutoka kwako.

Nina ushahidi tosha na ninachokisema hapa
 
Y

Yuko wapi mkuuu tumwandike kweny kitabu cha guiness?
 
Kitu kimoja msichokifahamu ni kwamba kuna wanawake hawana hulka za kuomba omba Pesa, mpaka wewe unaweza kujistukia na kuanza kumuulizia kama kuna chochote anachohitaji, na bado akaendelea na msimamo wake wa kutokuhitaji chochote kutoka kwako.

Nina ushahidi tosha na ninachokisema hapa
Kwani mpka umuulize?! We mkuu vp unakwama wapi??
Asieomba ndio mzuri lkn hii haimaanishi kwamba hana shida

Sasa wewe chakufanya usimuulize

We ukijiona uko vizuri kidogo mtumie chochote hata vizawadi nunua mpe
Sio mpka umuulize
Ukiona hakuombia jiongezeeee mkulungwaaaaaa...... Huyo shida anazo ila anaona kusema
 
Ngoja nikatafute mvuta bangi mwenzangu🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom