Tafsiri yake nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafsiri yake nini?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Anfaal, Sep 28, 2010.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yapo maneno mengi saana yanatamkwa na waomba na wanaowaombea Kura.
  Mfano;
  1. JK wakati yupo Iringa baadhi ya vyombo vya habari vilimkariri akisema; Chagua CHAMA na si mgombea. Wakati huu alikuwa akimnadi mgombea wa CCM na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Monica Mbega.
  Ni wazi kuwa Monica Mbega amekumbana na upinzani wa hali ya juu baada ya kuanguka kwa Mwakalebela. Na sasa hivi unaonekana mchuano mkali kati ya CHADEMA na CCM.
  2. Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA ndugu Nyimbo katika moja ya kampeni zake za Uchaguzi alisikika na yeye akinadi; CHAGUA mtu na si CHAMA.
  Hapa tunaweza kupata tafsiri ipi kwa wale wanaohimiza achaguliwe mtu na wale wanohimiza chama ndio kipewe nafasi??
  Na je CHAMA hakina watu au watu hawana CHAMA?
   
 2. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushawachanganya akili hapo. House of great thinkers iko totally confused sasa hivi. :becky: :becky: :becky:
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  la msingi ni kuchagua mtu na si chama kama ilivyoonekana toka awali, kuna watu makini kama nyimbo unamchagua bila kujali chama so ni vema maslahi ya watu yakawekwa mbele chama baadae.
   
 4. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ukichagua mtu atakuwa anasimamia sera gani? Je watu hawaamini sera vyama vyao? Na ukichagua CHAMA nani atasimamia sera na kwanini watu bogus ndio wapewe nafasi?
   
 5. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CCM inatumia kauli ya chagua chama usichague mtu kwa sababu chama chao kinamsingi hadi kijijini na kinaaminika kuwa na sera nzuri na ni chama cha NYERERE hivyo kinajiuza chenyewe tokana na historia yake chini ya mwalimu nyerere. Ikiwa mgombea hauziki wanataka abebwe na chama.
  CHADEMA na wapinzani wengine vyama vyao sio maarufu na havina misingi hadi vijijini ni vyama ambavyo kwa sehemu kubwa ya Tanzania havina historia inayovifanya vitambulike kwa wananchi wa hali ya chini hususan waliopo vijijini ambao ni wapiga kura wengi, Hivyo wagombea wavyama hivyo ujinadi kwa kauli ya chagua mtu na si chama wakiamini uwezo wao na historia za utendaji wao kwa wapiga kura unajulikana mfano NYIMBO, SLAA, ZITTO ,NTAGAZWA NK. pia wagombea wengine wana taka kupimwa wao yaani waukumiwe wao na si kitumike chama chake kumuhukumu. AU mpinzani wake hasa wa CCM apewe nafasi kwa sababu ya umaarufu wa chama chake na si utendaji wake.
   
 6. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unachagua MTU yaani mtu unayemuamini ana uwezo wa kuongoza na anautendaji uliotukuka obvious huyu anauwezo wa kusimamia SERA ya CHAMA chake. LAKINI ukichagua CHAMA bila kujali mtu yaani mgombea wake ni nani? ana historia gani ya kiutendaji na mchango wake ni hupi ktk kusukuma maendeleo ya Taifa Tanzania hapo bila shaka utachagua mtu BOGUS
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo vyama havina maana na watu ndio wenye maana??? Pamoja na sababu ya mwl Nyerere, vyama vya upinzani navyo vimeshindwa kuwa vyama. Ni miaka 15 sasa toka vianzishwe, inamaana wanahitaji miaka mingapi ili waweze kusema chagua chama na si mtu?? Sasa km wananchi wengi wapo kijijini na msimamo ni kuchagua mtu, inamaana kuna utata juu ya hivyo vyama?? Licha ya kuwa Mwl Nyerere anaaminika kuwa alijenga misingi imara ya CCM na ndiyo uwepo wa kuchagua mtu na si CHAMA, misingi ya namna hii haivunjiki??? Kuna mtu kama Fidel Castro, toka 1950's amekuwa akisimamia ujamaa lakini sasa hivi umemshinda. Hapa ninamaanisha kuwa haja ni kuwa na vyama imara vyenye uwezo wa kuhimili mikikimikiki na si vyenye kuamini katika uwepo wa sura fulani. Licha ya ubovu wa CCM lakini wameweza na wanaendelea kuwaaminisha wananchi kuwa wachague chama. Binafsi naamini katika dhana ya kuu ya CHAMA na si mtu, hivyo naiona hii ni changamoto kwa UPINZANI.
   
Loading...