Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 97
- 1,752
TAFSIRI HALISI YA KUFUTWA MASHITAKA YA MBOWE.
Bashir Yakub, WAKILI
+255 714 047 241
Nimemsikia Mbowe akisema kuwa hakutaka kufutiwa mashitaka bali alitaka kesi ifike mpaka mwisho/ hukumu.
Yawezekana anasema hivyo kutokana na sababu ya tafsiri halisi ya kufutiwa kwake mashitaka.
Kisheria ukifutiwa mashtaka kwa "Nolle Prosequi" chini ya Kifungu cha 91(1)CPA kama alivyofutiwa Mbowe sheria inaruhusu kukamatwa tena hapohapo au huko mbeleni na kushitakiwa tena upya kwa makosa yale yale.
Hii ni tofauti na pale kesi inaposikilizwa mpaka mwisho na mahakama ikatoa hukumu ya hatia au ya kuachiwa huru, ambapo sasa huwezi tena kukamatwa ama kushitakiwa tena kwa makosa yaleyale( autrefois acquital & autrefois convict).
Kufutiwa mashtaka kwa staili hii tafsiri yake sio kwamba huna hatia, bali ni kwamba kwa muda huo wanaokushitaki(serikali) wameamua tu kutoendelea na kesi ila wakiamua tena muda wowote, saa yoyote wanarudi kukushitaki.
Pengine hili ndo limemfanya Mbowe aseme hakutaka afutiwe mashtaka bali alitaka kesi iende mpaka hukumu/mwisho.
Pia kufutwa mashitaka kwa mtindo huu hutumika kisiasa kumnyamazisha mtu(blackmail).
Kila ukifukuta utatishiwa kurudishiwa mashtaka yako, ama tu we mwenyewe kila ukitaka kung'aka utakuwa unahofu kuwa unaweza kurudishiwa mashtaka yako na hivyo unajikuta ukiwa mpole.
Kwa ufupi kufutiwa mashtaka kwa mtindo huu hakuleti raha ya kudumu, amani ya nafsi, na uhuru wa kweli kwa aliyefutiwa kama ambavyo kesi ingekuwa imefika mwisho na hatma yako ikatangazwa na mahakama.
Hii ndio tafsiri halisi ya kufutwa mashtaka ya Mbowe.