Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,618
Miaka mingi tafiti zimefanyika kwenye jamii na zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Tafiti hizi haziwasaidii watanzania kwa kuwa hawawezi kuzifanyia kazi. Ukienda nyumbani kwa profesa yeyote utakutana na makabati yaliyojaa tafiti mbali mbali - ni kama uchafu kwa sababu hazifanyiwi kazi.
NINI KIFANYIKE?
Kwa wale wenye kujua hiyo lugha, niwaombe - tusaidiane kuzitafsiri hizo tafiti na kuanza kuzifanyia kazi ili jamii ifaidike na makaratasi hayo.
Hatuwezi kwenda majumbani kwa hao maprofesa - badala yake tuwafundishe vijana wetu wajue matumizi sahihi ya computer hasa kwenye ku-search tafiti na kuzisoma, kuzitafsiri na kuanza kuzifanyia kazi.
Kwa mfano; zipo tafiti zimefanywa na wengi kuhusu mti wa mlongelonge na faida zake, lakini ukitembea kwenye miji mbalimbali mti huo haupo na kama upo basi hakuna anayejua faida zake. Majani ya mti yana faida kiafya zaidi ya karoti, maziwa, ndizi, uyoga na machungwa.
PENDEKEZO:
Kwa watakaohitaji kuwa na mimi - hasa wataalamu mbali mbali nawaomba tuungane ili tuweze kutengeneza ajira kupitia tafiti zilizoandikwa.
KARIBU TUIJENGE TANZANIA.