mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 987
- 795
Maono na kiu ya watanzania wengi kuona viwanda vikishamiri ktk nchi yetu.Na pia Ni Maono na kiu ya Mh Rais wetu kuendelea kuzindua viwanda vikubwa vya kimkakati hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi, Uzalishaji, Unafuu wa bidhaa na kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumika katika uagizaji toka nje ya nchi.
Gazeti la Daily News la Tarehe 13 Mei 2024 ukurasa wa 8 limechapisha habari ya utafiti uliofanywa na Dr Patrokil Kanje Mhadhiri toka Chuo Kikuu cha Dar es salaam unaolezea pamoja na mengine vikwazo vya kisheria, utaratibu,Tozo na Compliance vilivyopelekea na vinavyopolekea viwanda kupunguza uzalishaji, Kufungwa na kutoanzishwa Tanzania.
Tafiti inaonyesha kwa mwaka 2021 bidhaa zenye thamani ya dola za marekani 458.7 Milioni (Karibu TZS Tirioni 1.3) ziliagizwa toka nje kuja nchini. Mahitaji yanaongezeka kwa asilimia 9 kwa mwaka huku uzalishaji ukipungua kwa asilimia 10 mpaka 20.
Mh Rais na Mawaziri wa kisekta hili si la kufumbia macho ama kulikalia kimya. Ni janga kubwa kwa uchumi wa nchi ,afya ya uchumi, maendeleo ya Taifa na usalama wetu.
Mwenyezi Mungu awajalie kufufua mirija na mishipa ya uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha mengi yaliopendekezwa kupitia Blue Print yanafanyiwa kazi kwa kuondoa vikwazo,mabonde,Milima na kero kwa wawekezaji wa ndani na wa nje.
Kwa kutekeleza kimkakati mapendekezo yaliotolewa na yanayoendelea kutolewa kupitia tafiti mbalimbali nina imani tutatoka hapa tunapokwama. Tunazo taasisi nyingi zenye kufanya tafiti zenye rutuba kwa maendeleo ya nchi kama REPOA,ESRF,UDSM,etc.
Wanasiasa kwa level zote hasa Mawaziri na watendaji ktk taasisi za Umma amkeni na muondoe bureaucracy (Ukiritimba) unaopelekea uchumi kusinyaa. Tuondoe vikwazo kwa faida ya nchi.
MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANGANYIKA,ZANZIBAR NA JMT