Tafasiri yangu katika picha hii?

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,723
Reaction score
11,934
TAFASIRI YANGU KATIKA PICHA HII
1.Kila mtu ana uwezo wake tofauti na mwengine. Jifunze kuwaheshimu watu uliowazidi nguvu/uwezo. Si mara zote watakuwa dhaifu.

2. Unapokusudia kumuumiza mwingine, unaweza kuumia wewe. Wakati mwingine mabaya unayotaka kumtendea mwengine yanarudi kwako.

3. Tazama njia unazopitia unapojitafutia ridhiki. Njia nyingine zinaweza kukuletea mauti.

4. Tamaa iwe na kiasi. Tamaa ikifikia kiwango cha uroho, mauti yanakaribia.

5. Maguvu yana mipaka yake. Sio kila mahali utatumia maguvu na kufanikiwa, unahitaji akili zaidi.
6 ".............

 
Wakati mwingine sio tu tamaa bali hata kujiamini kupita kiasi kunaweza kusababisha
 
Wakati mwingine sio tu tamaa bali hata kujiamini kupita kiasi kunaweza kusababisha
 
Njaa ni mbaya sana!.
pale unapotaka kukamata fursa halafu njia hujaweka lzm yakupate!.
maamuzi ya bila kutafakari hupelekea majanga!.
Udhaifu wako ndio ushindi wa adui yako.
 
Wengi watatamani kuingia katika ufalme wa Mungu lakini wasiweze hii ni kutokana na kulemewa na mambo matatu kwa mujibu wa mwasisi wa Wokovu duniani:
i. Ulevi
ii. Ulafi
iii. Masumbufu ya dunia (tamaa ya mali)
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…