Tafasiri ya red brigade ya chadema

Tafasiri ya red brigade ya chadema

stewart frenk

Member
Joined
Jun 9, 2013
Posts
48
Reaction score
15
Nimekuwa nasoma threads mbalimbali juu ya upotoshaji mkubwa unaofanywa na watu wanaotuona sisi mazuzu tafsiri ya maudhui ya uwepo wa RED BRIGADE.Kwanza kwa mtu makini hatakiwi kutafasiri jambo ambalo lipo kwenye katiba ya taasisi nje ya tafsiri ya na mantiki ya humo kwa hiyo kutafsiri RED BRIGADE kwa kufanya infarance ya ITALY ni kiwango cha hali ya juu cha upotoshaji na kutudhani sie ni mambumbu HOJA tunatafasiri RED BRIGADE kwa kuona mantiki ya kuundwa uwepo na kazi zake(ulinzi wa mali na viongozi).Katiba ya Tanzania inakataza mtu au taasisi yeyote kuwa na Jeshi(ibara 147) Je tuseme Jeshi la wokovu pale kurasini ni uvunjifu wa katiba?Hapana Sioni dhambi yeyote kwa chadema kuwa na kikundi maalumu kwa ajili ya ulinzi wa mali na viongozi wake ambapo kuna Taasisi nyingi za watu binafsi zinafanya shughuli hii(ulinzi). Na wanatumia hadi silaha za moto Group4,ultimate security etc zote ni ulinzi na usalama wa mali Je vyombo vya dola vimeshindwa kazi hapana huo ndio ulinzi shirikishi.Nilidhani hawa jamaa (CHADEMA) wangepongezwa kuimarisha ulinzi wa mali na viongozi maana wanatekeleza dhana ya Ulinzi shirikishi na Polisi jamii ambayo itapunguza kiwango cha jinai kuliko upotoshaji unaofanywa

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
wananchi tunatakiwa tulaani kwa nguvu zetu zote na tupinge kwa nguvu zetu zote kwa vyama vya siasa kuanzisha vikundi vya jeshi au ulinzi kama wao wanavyoweza kuita. mtu yeyote au kikundi chochote kinachoanzisha kikundi cha jeshi katika siasa au dini huyo/hicho ndicho adui mkubwa wa amani yetu. hakuna sehemu vikundi hivi vimeleta maendeleo bali kuwafanya wananchi wakimbizi, wengine kuuawa na wengine kupata vilema vya maisha, wengi wamepoteza mwelekeo wa maisha. watu wanapokuwa wanatafuta madaraka watatumia njia yoyote na wakiona wameshindwa wanakimbialia msituni ili ama wachukue kwa nguvu au waitwe kwa mazungumzo na wapewe madaraka. bado nasisitiza katiba mpya ipunguze kwa kiasi kikubwa nafasi za uteuzi wa raisi hasa kuongoza taasisi na mashirika ziwe za kuwania kwa ushindani wa sifa. nafasi za kuteua zibaki chache sana hasa za mawazili tutapunguza chokochoko katika siasa
 
Nakupongeza kwa Tafsiri yako mwana JF. kinacho onekana hapa ni uwoga wa ccm na vyombo vyake vya ulinzi ambao wanaonekana kutishwa sana na Tamko la Chadema. Mantiki ya Hoja ya Chadema si tu kuanziasha Red Brigade bali kutengeneza usawa baina ya vyama vya siasa na kuamsha tafakari kubwa ya utendaji mbovu wa jeshi la Polisi katika nchi ya Tanzania. Vile vile ni kuvuta Uelewa wa watu wengi wasio tambua waweze kutambua kwamba CCm na serikali yake ni kandamizi kwa wao kuwa na kikundi cha ulinzi Green Guard na kuzuia vyama vingine visiwe na uwezo wa kuwa na makundi ya namna hiyo. SERIKALI YA TANZANIA INAZIIDI KUCHAFUKA KATIKA MEDANI YA KIMATAIFA ndio maana OBAMA alisema DEMOKRASIA si UCHAGUZI TU bali ni pamojja na maisha baada ya UCHAGUZI.
 
kwa mujibu wa LONGMAN DICTIONARY OF CONTEMPORARY ENGLISH NEW EDITION FOR ADVANCED LEARNERS uk 200, neno "brigade" lina maana tatu:1. A large group of soldiers forming part of an army. 2.an insulting word for a group of people who have the same beliefs. 3.a group of people who are organized to do something. Kuchagua maana ya jeshi tu ni mwelekeo wa dhahiri wa upotoshaji unaokusudiwa kuamsha chuki dhidi ya chadema.
 
Back
Top Bottom