Tafakuri miaka 41 ya CCM

Tafakuri miaka 41 ya CCM

Jef Kirhiku

Member
Joined
Dec 10, 2016
Posts
39
Reaction score
76
Heri ya siku ya kuzaliwa CCM .
Leo chama cha mapinduzi kimetimiza miaka 41 tangu kuasisiwa kwake. Ni umri mkubwa ambao vijana wengi tunaoishi sasa tulizaliwa tukakikuta chama hiki.

Moja ya nguvu kubwa ya chama hiki ni muundo wake unaotambaa kila mahali katika nchi hii na kwenda mpaka ngazi ya chini kabisa ukilinganisha na vyama vingine vya siasa hapa Tanzania.

Lakini pili utaratibu /utamaduni wake wa kubadili Uongozi mara kwa mara kukidhi mahitaji ya Nyakati, umeendelea kukipa uhai na taswira mpya inayowavutia wengi.

Wakati kikiadhimisha umri huo wa miaka 41 ni vyema kujitafakari namna chama kinavyowaandaa makada wake kutoa uongozi mzuri kwa taifa na chama.

Kuna tofauti kubwa kati ya mtu aliyeandaliwa kuwa kiongozi na mtu ambaye imetokea tuu amekuwa kiongozi.

Utaratibu wa kuwapa mafunzo ndani na nje ya nchi ,kuwapa nafasi ndani na nje ya serikali na kuwatizama kwa muda mrefu wanachama watakaotoa uongozi mzuri kwa Taifa na chama bado ni mwafaka katika kuandaa viongozi.
Tuendelee kujenga mifumo mizuri ya kubaini na kuwaendeleza wanachama wenye uwezo na vipaji vya uongozi.

Tuendelee pia kufanya maamuzi ndani ya vikao yanayotokana na mijadala inayotoa fursa kwa kila mtu kuwa huru na kueleza maoni na mtazamo wake kabla ya kufikia uamuzi .Hoja yenye nguvu ndiyo inayoshinda bila kujalisha ameitoa nani.

Isitokee mtu au kikundi fulani cha watu wakajifanya chama ni mali yao, wakitakacho wao ndo hicho hicho, kuwa na maoni tofauti nao ni usaliti na ukosefu wa uzalendo .Hapo chama kitaharibikiwa .

Happy Birthday ccm .

Japhari Mtoro .
Mwanachama wa CCM toka Singida .
5/02/2018 .
0714195367 .
 
Hee kumbe leo ni ccm day. Mbona hakuna mbwembwe. Au na chama nacho kinaisoma namba
 
Watasherekaje wakati mwenye hati miliki ya CCM Mzee Kingunge kafariki na kazikwa leo?Wao wote wanajua hata kama hawatamki kwa sauti kubwa lakini wanajua na kutambua kuwa CCM ni mali ya Mzee Kingunge wala hana ubia,hao wote ni waigizaji,lakini mtuzi anabakia Mzee Kingunge R.I.P
 
Pamoja Kada!
Heri ya siku ya kuzaliwa CCM .
Leo chama cha mapinduzi kimetimiza miaka 41 tangu kuasisiwa kwake. Ni umri mkubwa ambao vijana wengi tunaoishi sasa tulizaliwa tukakikuta chama hiki.

Moja ya nguvu kubwa ya chama hiki ni muundo wake unaotambaa kila mahali katika nchi hii na kwenda mpaka ngazi ya chini kabisa ukilinganisha na vyama vingine vya siasa hapa Tanzania.

Lakini pili utaratibu /utamaduni wake wa kubadili Uongozi mara kwa mara kukidhi mahitaji ya Nyakati, umeendelea kukipa uhai na taswira mpya inayowavutia wengi.

Wakati kikiadhimisha umri huo wa miaka 41 ni vyema kujitafakari namna chama kinavyowaandaa makada wake kutoa uongozi mzuri kwa taifa na chama.

Kuna tofauti kubwa kati ya mtu aliyeandaliwa kuwa kiongozi na mtu ambaye imetokea tuu amekuwa kiongozi.

Utaratibu wa kuwapa mafunzo ndani na nje ya nchi ,kuwapa nafasi ndani na nje ya serikali na kuwatizama kwa muda mrefu wanachama watakaotoa uongozi mzuri kwa Taifa na chama bado ni mwafaka katika kuandaa viongozi.
Tuendelee kujenga mifumo mizuri ya kubaini na kuwaendeleza wanachama wenye uwezo na vipaji vya uongozi.

Tuendelee pia kufanya maamuzi ndani ya vikao yanayotokana na mijadala inayotoa fursa kwa kila mtu kuwa huru na kueleza maoni na mtazamo wake kabla ya kufikia uamuzi .Hoja yenye nguvu ndiyo inayoshinda bila kujalisha ameitoa nani.

Isitokee mtu au kikundi fulani cha watu wakajifanya chama ni mali yao, wakitakacho wao ndo hicho hicho, kuwa na maoni tofauti nao ni usaliti na ukosefu wa uzalendo .Hapo chama kitaharibikiwa .

Happy Birthday ccm .

Japhari Mtoro .
Mwanachama wa CCM toka Singida .
5/02/2018 .
0714195367 .
 
Hapa kazi tu! Sehemu nyingi sherehe zilifanyika jana jumapili tarehe 04 Feb.2018 siku ya mapumziko leo ni siku ya kazi. Wakisema hapa kazi tu inatafsiriwa kwa vitendo.
Hee kumbe leo ni ccm day. Mbona hakuna mbwembwe. Au na chama nacho kinaisoma namba
 
Ila ndio mwisho wa CCM kutawala unakaribia ....

The End Is Near...

Kwa wanaojua Nguvu ya 40 wanaelewa...
Ilishatabiliwa sana kwa bahati wanaotabili ndiyo wana kila dalili za kufa kabla hata ya 40. CCM ilishavuka 40!
 
Back
Top Bottom