Tafakuri kuhusu Kifo

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
570
1,000
Uzuri ni kitu kinachopita hakikai katika mwili wa binadamu milele, ni kama maua waridi toka nje yaangalie asubuhi ni mazuri na yenye kuvutia rudi jioni yamenyauka na kupoteza uzuri wake.
Hata maisha ni ya kupita nina maisha mapya sasa ya zamani nimeyaacha. Tutaendelea kubadilika hadi tutakapoingia kaburini. Utoto wetu umepita sasa ni vijana na mida si mrefu tutakuwa wazee. Wengine tutakuwa mababu na wengine mabibi na msisahau kaburi linatusubiri kila mmoja wetu. Na kama kuna siku ya hukumu tunayosikia tangia utoto wetu kila mtu atahukumiwa kutokana na matendo yake.

Tutakapo ondoka sisi duniani wengine wataendelea kuishi, kitakachobaki ni kumbukumbu tu kwa waliobaki na pengine hatuna uhakika kama kizazi kinachokuja kitatukumbuka au kitatusahau.

Ni muhimu kukumbuka sisi ni watu wa kupita tu humu duniani hatudumu. Maisha yetu duniani ni mafupi mno. Na baada ya kufa je tunaenda wapi? kama tuko duniani ni lazima tutakuwa tumetoka sehemu fulani. Ni lazima kutakuwa na kisababishi cha uwepo wetu duniani.

utafutaji wangu wa ukweli utaendelea hadi nitakapoingia kaburini nitakapouacha huu mwili ninaoutumia kila siku kwa maisha yangu ya duniani.

sisi binadamu ni kina nani? ni bora kiasi gani zaidi ya wanyama? wote tunakufa, wote tunakula chakula kile kile kinachozalishwa na ardhi na tunachangia dunia moja. Kitu cha ziada tulicho nacho ni akili yetu iliyo tufanya tuwatawale wanyama na dunia. lakini bado sisi ni wadhaifu na maisha yetu ni mafupi mno.Maisha yetu ni kama kufuta mavumbi kwenye kioo leo mtu yupo kesho hayupo. Hata wale ambao ni wenye nguvu na majasiri waliotetemesha dunia wamekufa na hawapo tena.

Ninapofikiria haya nafikiria kuhusu mungu na siku ya mwisho ambayo masikio yangu yamekuwa yakiisikia mara kwa mara. Siwezi kukataa moja kwa moja kuhusu siku hii kwa sababu nimezungukwa na ushahidi wa kuwepo kwa mungu. nimeumbwa kwamba bila chakula siwezi kuishi na kwa miaka yangu yote nitaishi kwa kula kama wanyama wengine wote.

Kila siku nafikiria siku yangu ya kufa wakati mwili wangu utakapojitenga na roho. Nitakapoiacha dunia na kila kitu kilichopo.

Kwahiyo kuwa mwangalifu na maisha yako na angalia nyendo zako hujui kesho yako itakuwa vipi na usiiishi kama hautokufa na pengine huenda tutakapokufa tutakutana na hukumu nani anajua?

Chukua muda wako na fikiria kuwa makini mno huo ndio ushauri wangu. Kwasababu hakuna mtu atakaye hukumiwa kwa kutenda mema bali mabaya na ushahidi wa hili jambo ni humu dunia huwa atuadhibu watu waliotenda mema bali mabaya. Kuwa mwangalifu na maisha yako.
 

Myakubanga

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,843
2,000
Kuishi huku unawaza utakufa lini ni kujenga woga usio na msingi.
Kifo kipo constant,na haituongezei chochote kuishi ukiwaza utakufaje!
Otherwise,hoja yako ni nzuri,lakini yenye matege ya kimantiki ndani yake.
Umetumia neno "Inawezekana kuna hukumu" hivyo kudhihirisha huna hakika na uliyo andika hapa.
Kwa maneno mengine,unajaribu kutushawishi tuishi kwa hofu zisizo na uhakika wowote.
 

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
570
1,000
Kuna sehemu nimesema watu waishi kwa hofu? Jaribu kutafakari ujumbe kabla ya kujibu ili uheshimiwe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Similar Discussions

Top Bottom