Tafakuri: Chuki za Kisiasa Nchini Tanzania, Zinaleta Umoja wa Kitaifa na Uzalendo? Nini kifanyike?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Heshima kwenu wakuu,

Leo tujaribu kuangalia matukio ya Ukandamizaji kupitia vyombo vya dola, Je inatusaidia kama Taifa? Nini kifanyike kuondoka kwenye huuu mkwamo?

Naomba tutumie nafasi hii kushauri nini kifanyike ili kudumisha umoja wa Kitaifa ikizingatia sisi sote ni wamoja.

Chuki zimeanza zamani kidogo, Nakumbuka huko zazibar watu walikuwa hawazikani kwa sababu za kisiasa. Hivi sasa imefika hadi Tanganyika, watu hawazikani kisa Siasa, inaonekana Chuki ya Wazi mfano mdogo Kifo cha Mzee Ndesamburo.

Sasa hivi mtaani hakukaliki, mtu wa Upinzani anapofanya kosa hapelekwi mahakamani, Viongozi wa kisiasa wanatumia Mamlaka yao kuhukumu. Mfano Uharibifu wa Shamba la Mbowe.

Hivi juzi Serikali imeamua kukaa na Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwakanya ili Wafuate Sheria bila shaka wamesikia.

Sasa kwenye hili Swala, Wewe kama Mwananchi wa Kawaida, nini Mchango wako ili tujikwamue hapa tulipo.

Ninachoamini, Serikali haiwezi kuwatuma wanasiasa wabaguane au wanyanyasane kwa vyeo vyao.

Hapa chini nmeweka picha za Shamba la Freeman Mbowe mwenyekiti wa CHADEMA liloharibiwa kwa Kigezo kwamba kalima sehemu oevu, Kumba haya ni mashamba ya Familia yapo miaka nenda rudi. Je Angeshitakiwa sheria zingechukua mkondo wake? Kwanini Hakishitakiwa?

Je unaweza vaa Viatu vya moyo wa huyu baba aliyramrisha waharibu shamba? Unafikiri alishawahi kulima?

Unadhani anazo fedha za kulipa kama akishindwa kesi au watatumia kodi zetu kulipa fidia?

Unaamini kama alisifiwa baada ya tukio hili?

Usiku alilala usingizi mzuri?

Tufanyeje kuokoa kizazi kijacho dhidi ya hizi chuki?

Karibuni.

 
Duh hatari inabidi viongozi wetu waangalie siasa yet inapoelekea umoja n mshikamano unapotea bila sababu za msingi
 
Aisee yaani mtu kalima kwa nguvu na pesa nyingi tena kwa greenhouse kilimo bora kilichoishinda ccm na serikali yake then anatotokea mwehu mmoja anafanya haya, hili walilofanya litawagharimu kama si leo hata kesho litatokea na watajuta....Mh mbowe pole sana najua wewe ni mtu makini san na mvumilivu, Mungu atakulipa kwani amekuvusha mengi kwa watesi hawa.
 
Bila polisi hakuna ccm , hawataweza kuacha kutumia dola maana huo ndio uhai wao .

Nini kifanyike ? Ushauri wangu ni kwamba ccm iendelee tu kukandamiza wapinzani kwa kutumia dola , maana hiyo ndio njia pekee iliyobaki kwa wao kubaki madarakani .

Pendekezo - waende mbele zaidi kwa kuwaua wapinzani ili wabaki peke yao kwenye siasa za Tanzania , hivi vyama vya HOVYOHOVYO visipewe nafasi .

Mungu ibariki Tanzania .
 
KILIMANJARO: Nyumba ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hai, Dkt. Amini Uronu imechomwa moto usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana.

Mtoto wa Mwenyekiti huyo amesema kuwa Wazazi wake wote wamelazwa baada ya kapata madhara kiasi katika miili yao.
 
Sasa Huu Ni umoja gain wa kitaifa?
 
Mbowe ni mkwepa kodi hadi Bil.1.6 na mharibifu wa mazingira.
 
Nimesoma kwa masikitiko makubwa habari kutoka wilaya ya hai kwamba mkuu wa wilaya aliamuru kuharibiwa kwa shamba la kisasa la Mh Freeman mbowe.

Sababu iliyotolewa ni kwamba shamba hilo linakiuka sheria za mazingira. Hiyo, kisheria imekaa sawa nailewa.

Lakini siielewi hatua aliyochukua mkuu wa wilaya ya kuharibu miundombinu ya shamba hilo la kisasa la greenhouses.

Kitendo cha mkuu wa wilaya ni sawa na askari polisi kumpiga risasi na kumwua mtu ambaye ameiba kwa sababu kuiba ni kosa kisheria.

Ningemwelewa mkuu wa wilaya kama angempeleka Mh Mbowe mahakamani kwa kuvunja sheria, si kumhukumu kwa kuharibu shamba lake.Utawala wa sheria uko wapi hapa? Au hiyo sheria ya mazingira inampa dc mamlaka ya kuharibu mali inayodhaniwa kuharibu mazingira?

Naomba ufafanuzi kwa wanaoelewa sheria ya mazingira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…