Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,407
Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo makubwa. Tutumie nafasi hii vizuri rafiki.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu NITAANZA MWAKA MPYA.
Siku chache zilizopita nilikuwa na marafiki tukifanya mazungumzo mbalimbali kuhusu maisha. Tukafika eneo la mtindo wa maisha, kuhusu ulaji na ufanyaji wa mazoezi.
Rafiki mmoja akasema kuanzia tarehe tatu mwezi wa kwanza nitaacha kunywa pombe na nitaanza kufanya mazoezi kila siku. Nikamuuliza kwa nini tarehe tatu? Kwa nini usianze kesho? Akanijibu, bado kuna mwaka mpya, acha kwanza upite ili nianze vizuri.
Nikamjibu kama huwezi kuanza kesho, basi hata hiyo tarehe tatu unayosema hutaweza kuanza. Na hata ukianza hutafika mbali. Maana kama huna nidhamu ya kuweza kuanza sasa, hutakuwa nayo kuweza kuanza siku hizo ulizopanga.
Hili ni jambo muhimu sana kwa kila mmoja wetu kutafakari.
Najua yapo mengi ambayo tumejidanganya kwamba mwaka mpya ukianza tutaanza kuyafanya. Ukweli ni kwamba tunajidanganya, hakuna kipya kwenye mwaka mpya zaidi ya mabadiliko ya tarehe, hivyo kufikiria kuna mambo ya kipekee yatakayotokea baada ya mwaka mpya, ni njia ya kulea uzembe.
Kama kuna kitu chochote muhimu unataka kufanya kwenye maisha yako, kama huwezi kukianza leo, basi hutaweza kukianza hiyo mwaka mpya unayosema. Na hata ukikazana ukaanza, hutafika mbali. Kwa sababu kinachokufanya usianze leo ndiyo kitakachokuzuia usianze kwenye mwaka mpya.
Jambo lolote tunalotaka kufanya kwenye maisha yetu, tunahitaji nidhamu, na kama hatuna nidhamu hiyo tutatafuta njia za kujidanganya ili tusijione ni wazembe. Na moja ya njia hizo ni kusema utaanza mwaka mpya.
Kama kipo kitu unataka kufanya, anza kufanya sasa, anza kufanya hata kwa hatua ndogo kabisa. Usisubiri mwaka mpya, wewe ni yule yule na hakuna mabadiliko yanayoletwa na kubadilika kwa tarehe, mabadiliko unayaleta wewe mwenyewe. Anza kuyaleta leo.
Karibu kwenye semina ya 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO, kushiriki tuma ujumbe wenye neno semina kwa njia ya wasap kwenda namba 0755 953 887, muhimu, tuma ujumbe kwenye wasap tu.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
[HASHTAG]#KochaMakirita[/HASHTAG]