Seif al Islam
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 2,156
- 640
Moja kati ya mbinu kubwa walizotumia wakoloni katika kulitawala bara laAfrika na kuiba mali asili za bara hili ni kujenga urafiki na viongozi wa nchi husika.Hii hujumuisha kutoa vitu vinavyoonekana kama zawadi na misaada (rejea ujenzi wa uwanja wa soka na kituo cha kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Nyerere).
Pia viongozi husika hupewa heshima na hadhi hata wasizofanana nazo (siongelei uprofessa wa JK). Kibaya zaidi kinachofanywa na wakoloni ni kuwasainisha viongozi wa nchi husika mikataba mikubwa ya uvunaji wa rasilimali katika nchi husika.
Mikataba hii huwa siri kubwa kati ya watawala wa Afrika na "mkoloni" husika. Kwa jinsi hali ya uhusiano na ushirikiano kati ya viongozi wa Tanzania (rejea ziara ya kinana huko china na sasa ziara ya JK huko uchina na ile iliyofanywa na rais wa China hapa nchini) na Tanzania kama nchi na china inavyozidi kukua huku mikataba ya ushirikiano na biashara kati ya nchi hizi mbili ikiendelea kuwekwa siri kati ya viongozi wa Tanzania (kama kweli nao wanaijua) na wachina mtu anaweza hata kufikiri kuwa Tanzania imegeuzwa "koloni" la china.
Kwa maoni yangu, Tanzania imegeuzwa kwa kupenda "koloni" la China na tofauti kati ya "ukoloni" huu na ule wa zamani ni kuwa huu wa sasa ni wa viongozi wetu kwenda kuwaita "wakoloni" kututawala na kutunyonya