dos santos
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 256
- 128
Akiongea kwenye tafrija fupi ya kuishukuru timu ya kampeni pamoja na wananchi waliowaunga mkono Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alisema,
"Kwa kura za Rais kwa mujibu wa sheria za nchi hii zinadai akishatangazwa hawezi kubadilishwa na huwezi kwenda kwenye mahakamani yoyote.Hizi sheria zinatungwa na mwanadamu, hazikutungwa na Mungu. Na zimetungwa na Mwanadamu ili zipoke haki katika jamii, hatutakubali haki hiyo ipokwe kijinga hivyo na sisi tukakaa kimya tukatulia tukapiga magoti. Mwisho wa sheria mbovu ni action za wananchi na sisi tunasema hiyo sheria itabadilishwa haki itapatikana na tutatengeneza mwanzo wa Tanzania mpya kama ambavyo tulikusudia kabla ya uchaguzi", mwisho wa kunukuu.
Hapo Mbowe alikuwa akilalamikia sheria mbovu ya kutokuhoji matokeo ya urais yakishatangazwa. Lakini cha kujiuliza kwa wanasiasa wetu fursa ya kupata sheria ya kuhoji matokeo ya urais waliipata lakini wakaipuuza. Ni kama hawakuona ubaya wa sheria hiyo kuingia nayo tena katika uchaguzi wa mwaka huu.
Wapinzani walipata fursa nzuri ya kuingia ndani ya uchaguzi wa 2015 wakiwa na sheria ya kuhoji matokeo ya urais pamoja na uundwaji wa tume huru. Hayo na mengine yalikuwepo katika katiba mpya ilyopendekezwa na ikapingwa vikali na kundi la wanasiasa waliounda umoja uliojulikanakama UKAWA.
Kubwa wanasiasa wetu waliikataa katiba hiyo pendekezwa kwa kuwa itakuwa na serikali mbili badala ya tatu. Hili ndio ambalo lilifanya wanasiasa wa upinzani kukataa kila kitu kilichokuwemo ndani ya katiba hiyo.Hawakuangalia mazuri yaliyokuwemo ambayo yangeweza kupelekea kupatikana na mengine mazuri zaidinasiasa. Rais Kikwete aliahidi kuingia uchaguzi mwa mwaka huu na katiba mpya, ambayo ndani yake kulikuwa na tume huru na sheria ya kuhoji mahakamani matokeo ya urais.
Ukitafakari kwa kina jambo hili waweza kuingia shaka juu ya wanasiasa wetu wa upinzani na nia yao ya dhati ya kuleta mabadiliko. Kwa nchi za kiafrika ambako demokrasia ni jambo linaloendelea kukua siku hadi siku, kupata katiba mpya yenye kila kizuri ni jambo gumu. Kwa mwenye kutafakari si haba kupata sheria fulani ambayo inaweza kusaidia kupatikana kwa mengine mazuri kwa siku za usoni.
Wanasiasa wetu mara nyingi hupenda kuangalia au kukazania yale yenye maslahi yao kwanza zaidi halafu wananchi. Tujiulize hivi nini athari ambayo inapatikana mpaka sasa kuwepo kwa serikali mbili na kukosekanika kwa serikali tatu.Lakini angalia athari ya kukosekanika kwa Tume huru ya uchaguzi na kutokuwepo kwa sheria ya kuhoji matokeo ya urais Mahakamani. Wanasiasa wetu ni kama hawana vipaumbele na kama vipo basi ni kiini macho.
Wananchi wenzangu ni vizuri kuanza kufuatilia vizuri mambo kadhaa katika nchi badala ya kuwaamini wanasiasa katika kila wanachosema na kuona kipo sawa.Ndio hawa hawa wanaounga mkono au kutopinga kuongezeka kwa posho za wabunge kila kukicha.Soma hapo chini kuhusu sheria ya kuhoji matokeo ya rais kama ilivyoainishwa katika katiba mpya iliyyopendekezwa.
KUPINGA MATOKEO YA RAIS MAHAKAMANI90.-
(1) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2), endapo mtu yeyote aliyeshiriki kama mgombea katika nafasi ya madaraka ya Rais katika uchaguzi wa Rais hakuridhika na matokeo ya uchaguzi huo, anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Juu kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi.
(2) Malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais yatawasilishwa Mahakama ya Juu ndani ya muda wa siku saba baada ya siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais.31(3) Mahakama ya Juu itasikiliza na kutoa uamuzi wa shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais ndani ya siku kumi na nne tangu kupokea malalamiko yaliyowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) na uamuzi huo utakuwa wa mwisho.
(4) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (3), Mahakama ya Juu inaweza kutoa uamuzi wa kumthibitisha Rais bila kutoa sababu za uamuzi na sababu hizo zitatolewa ndani ya kipindi kisichozidi siku thelathini tangu siku ya kutoa uamuzi.(5) Iwapo Mahakama ya Juu itaamua kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais si halali, uchaguzi wa Rais utarudiwa ndani ya siku sitini baada ya uamuzi kutolewa.
Uundwaji wa tume huru umeelezwa kwa kirefu katika katiba hiyo iliyopendekezwa katika sura ya pili.