TAFAKARI: kauli ya Mbowe na katiba mpya iliyokataliwa na UKAWA

dos santos

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
252
250
Akiongea kwenye tafrija fupi ya kuishukuru timu ya kampeni pamoja na wananchi waliowaunga mkono Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alisema,

"Kwa kura za Rais kwa mujibu wa sheria za nchi hii zinadai akishatangazwa hawezi kubadilishwa na huwezi kwenda kwenye mahakamani yoyote.Hizi sheria zinatungwa na mwanadamu, hazikutungwa na Mungu. Na zimetungwa na Mwanadamu ili zipoke haki katika jamii, hatutakubali haki hiyo ipokwe kijinga hivyo na sisi tukakaa kimya tukatulia tukapiga magoti. Mwisho wa sheria mbovu ni action za wananchi na sisi tunasema hiyo sheria itabadilishwa haki itapatikana na tutatengeneza mwanzo wa Tanzania mpya kama ambavyo tulikusudia kabla ya uchaguzi", mwisho wa kunukuu.

Hapo Mbowe alikuwa akilalamikia sheria mbovu ya kutokuhoji matokeo ya urais yakishatangazwa. Lakini cha kujiuliza kwa wanasiasa wetu fursa ya kupata sheria ya kuhoji matokeo ya urais waliipata lakini wakaipuuza. Ni kama hawakuona ubaya wa sheria hiyo kuingia nayo tena katika uchaguzi wa mwaka huu.

Wapinzani walipata fursa nzuri ya kuingia ndani ya uchaguzi wa 2015 wakiwa na sheria ya kuhoji matokeo ya urais pamoja na uundwaji wa tume huru. Hayo na mengine yalikuwepo katika katiba mpya ilyopendekezwa na ikapingwa vikali na kundi la wanasiasa waliounda umoja uliojulikanakama UKAWA.

Kubwa wanasiasa wetu waliikataa katiba hiyo pendekezwa kwa kuwa itakuwa na serikali mbili badala ya tatu. Hili ndio ambalo lilifanya wanasiasa wa upinzani kukataa kila kitu kilichokuwemo ndani ya katiba hiyo.Hawakuangalia mazuri yaliyokuwemo ambayo yangeweza kupelekea kupatikana na mengine mazuri zaidinasiasa. Rais Kikwete aliahidi kuingia uchaguzi mwa mwaka huu na katiba mpya, ambayo ndani yake kulikuwa na tume huru na sheria ya kuhoji mahakamani matokeo ya urais.

Ukitafakari kwa kina jambo hili waweza kuingia shaka juu ya wanasiasa wetu wa upinzani na nia yao ya dhati ya kuleta mabadiliko. Kwa nchi za kiafrika ambako demokrasia ni jambo linaloendelea kukua siku hadi siku, kupata katiba mpya yenye kila kizuri ni jambo gumu. Kwa mwenye kutafakari si haba kupata sheria fulani ambayo inaweza kusaidia kupatikana kwa mengine mazuri kwa siku za usoni.

Wanasiasa wetu mara nyingi hupenda kuangalia au kukazania yale yenye maslahi yao kwanza zaidi halafu wananchi. Tujiulize hivi nini athari ambayo inapatikana mpaka sasa kuwepo kwa serikali mbili na kukosekanika kwa serikali tatu.Lakini angalia athari ya kukosekanika kwa Tume huru ya uchaguzi na kutokuwepo kwa sheria ya kuhoji matokeo ya urais Mahakamani. Wanasiasa wetu ni kama hawana vipaumbele na kama vipo basi ni kiini macho.

Wananchi wenzangu ni vizuri kuanza kufuatilia vizuri mambo kadhaa katika nchi badala ya kuwaamini wanasiasa katika kila wanachosema na kuona kipo sawa.Ndio hawa hawa wanaounga mkono au kutopinga kuongezeka kwa posho za wabunge kila kukicha.Soma hapo chini kuhusu sheria ya kuhoji matokeo ya rais kama ilivyoainishwa katika katiba mpya iliyyopendekezwa.

KUPINGA MATOKEO YA RAIS MAHAKAMANI90.-

(1) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2), endapo mtu yeyote aliyeshiriki kama mgombea katika nafasi ya madaraka ya Rais katika uchaguzi wa Rais hakuridhika na matokeo ya uchaguzi huo, anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Juu kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

(2) Malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais yatawasilishwa Mahakama ya Juu ndani ya muda wa siku saba baada ya siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais.31(3) Mahakama ya Juu itasikiliza na kutoa uamuzi wa shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais ndani ya siku kumi na nne tangu kupokea malalamiko yaliyowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) na uamuzi huo utakuwa wa mwisho.

(4) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (3), Mahakama ya Juu inaweza kutoa uamuzi wa kumthibitisha Rais bila kutoa sababu za uamuzi na sababu hizo zitatolewa ndani ya kipindi kisichozidi siku thelathini tangu siku ya kutoa uamuzi.(5) Iwapo Mahakama ya Juu itaamua kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais si halali, uchaguzi wa Rais utarudiwa ndani ya siku sitini baada ya uamuzi kutolewa.

Uundwaji wa tume huru umeelezwa kwa kirefu katika katiba hiyo iliyopendekezwa katika sura ya pili.
 
Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,193
2,000

Katiba mpya isingeweza kutumika katika uchaguzi huu, ilikuwa iweke kipindi cha mpito; kwa uhakika ingetumika 2020
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
8,309
2,000
Umenitahadi kuandika lakini ni Pumba tupu , hiyo katiba inayopendekezwa ilipingwa na mbowe peke yake??? au ilipingwa na wananchi pamoja na time ya warioba? Kwa sababu iliomdoa msoni ya wananchi kwa 80% we unaleta dhihaka kama vile anayeathirika na mfumo huu no mbowe tu si wananchi wote nawe ukiwemo
 
Mp Kalix2

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
5,946
2,000
Ukisha kuwa kwenye ulevi wa Madaraka huwezi kuona uapande wa pili wa shilingi.

Hili hapa chini unaionaje.

Kwa nini Serikali ya Muungano ijivishe kofia ya kuendesha mambo ya Tanganyika?
Unadhani huu uongo na hadaa za jina Tanzania Bara hauwezi kuwa na mwisho?

Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
75. Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya utekelezaji katika Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano na kwa mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanzania Bara.
 
Mp Kalix2

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
5,946
2,000
Umeona ukweli unatabia ya kujitenge!
Ukiangalia hapo Tanganyika au wanavyopenda kuiita Tanzania Bara haipo tena ameshakuwa PM wa JMTKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya
Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Ebu tuangalie Katiba ya Zanzibar kama inamtambua huyu PM wenu wa JMTanzania pamoja na maeneo mengine yenye kuleta mwanga wa aina ya Muungano uliopo!

_________________________K__a_ti_b_a_ _y_a_ Z__a_n_zi_b_a_r_ _ya_ _1_9_8_4_________________________
Mamlaka ya Baadhi ya Vyombo vya Muungano
124.(1) Vyombo vilivyoainishwa chini ya kijifungu cha (2) cha kifungu hiki na kama vilivyoanzishwa kwa mujibu wa vifungu vya Katiba ya Muungano, vitakuwa na mamlaka ya kutekeleza shughuli zake Zanzibar kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa katika Katiba ya Muungano na Sheria yoyote nyengine iliyotungwa na ama Bunge au Baraza la Wawakilishi kwa ajili hiyo.
(2)Vyombo vyenyewe vilivyotajwa katika kijifungu cha(1) ni:
(a) Mahkama ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano;
(b) Tume ya Pamoja ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano;
(c) Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, vyombo vilivyoainishwa katika kijifungu cha (2) vitahesabika kama ni vyombo vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika shughuli zake hapa Zanzibar.
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,356
2,000
Tushachoka nafuu tupate Raisi mchapakazi na makini... Katiba hata ya zamani ni nzuri tu tatizo utu wetu chuki na husda ndio vinatusumbua
 
Haemoglobin

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
295
195
Katiba tuliyonayo ilkua nzuri kwenye karne ya 20 ilipotungwa, kutokana na changamoto na kasi ya maendeleo ya kifikra na kiuchumi za karne ya 21 pamoja na utandawazi katiba hii haitufai hata kidogo,Tanzania inahitaji katiba itakayozingatia matakwa ya wananchi na sio ya kikundi fulani cha watu.
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
10,554
2,000
Tushachoka nafuu tupate Raisi mchapakazi na makini... Katiba hata ya zamani ni nzuri tu tatizo utu wetu chuki na husda ndio vinatusumbua
Mkuu kweli huoni hatari ya kutegemea mtu anaye shika madaraka? Lipo hitaji la sheria kutoa miongozo ya namna ya kuongoza!. Katiba inayo mbana kiongozi kuwajibika kwa wana nchi ni njema.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom