Nasakadoo
JF-Expert Member
- Sep 18, 2014
- 343
- 169
Nawasalimia wapendwa katika BWANA na ALLAH (S.A.W)… Heri ya Mwaka mpya 2016 na mbarikiwe wote mtakaosoma uzi wangu huu wa kwanza kwa Mwaka huu hapa.
Baada ya Salamu,naomba tena nitoe feedback fupi kuhusu Jukwaa hili na Nilichokiambulia,n.k.
Ukifuatilia baadhi ya Threads zangu nimekuwa nikihangaika kuomba kazi,kutafuta kazi… huku nikijiainisha nina kiwango gani cha elimu,na ninapenda kada ipi,na ninaweza ku fit wapi.
Wadau wengi humu mlisifia uandishi wangu,mlikomenti kuwa mnaniombea nipate kazi.… nami nilishukuru,lakini sasa cha Muhimu ni pale baadhi ya Watu walipoguswa na kunijia PM tukazungumza na wengine baadhi walinipigia simu maana namba yangu ilikuwa wazi.
Kusema Ukweli wadau naomba niwaambie kuwa sikuwahi kubahatika kupata kazi kutokana na hao. Kwanza nilikuwa napewa ahadi nzuri za kupewa kazi,ila mwishowe miadi inayeyuka, mtu anajikomiti kabisa kuwa tutaonana labda siku fulani,siku ya siku ikifika zinakuwa ni kalenda kila kukicha. Nilikuwa napiga simu mpaka wengine hawapokei,wanakata. Ila ukija kwenye Comments zao wanaonesha kweli wanataka kunisaidia na wana moyo na wameguswa,ila in reality mimi niliona kama sikutendewa kama nilivyodhani. Sasa sikujua kama ni kwangu tu,au na kwa wengine watafuta ajira nao ilikuwa inakuwa hivyo. (Kiukweli inauma)
Moja ya sababu zao wale niliobahatika kuwasiliana nao, zilikuwa kwanza kama zinarandana.
-Kwa sasa nipo nje ya Nchi ila soon nitarudi,nitahakikisha tumeonana nikushughulikie.
-Nipo Mkoani kikazi,ila next week nitakuwa Dar,make sure tunaonana.
-Kati ya Noah au Bajaj unapendelea ipi ili wiki kesho tuonane tupeane mkataba uanze kazi,najua unahangaika sana nitakusaidia.
-Kuna duka za Hardware lakini siyo Dar,ni Mkoani kama unaweza tufanye maarifa uje.
-Kuna Site najenga,unaweza kuja kusimamia maana mimi huwa natoka toka. Kama utaweza itakuwa poa sana Jumamosi tukutane kwa sasa nipo Bagamoyo…
-Bajaj ipo tayari, kama una uwezo wa kuleta hesabu ya Tsh 25,000-30,000 kwa siku tuwasiliane mkuu nikukabidhi chombo…(Wakati inafahamika kabisa kwenye bajaji hesabu yake ni 15,000,17,000 ikizidi sana ni Elfu 20,000kulingana na maeneo ya kazi)....
-N.k. NA NILIKUWA NAKUBALI MASHARTI .
Wakuu,ndugu zangu kama mlivyoona,nimejaribu kuainisha baadhi ya Majibu na ahadi zilizokuwa zinatoka kwa waliotaka kunipa kazi… lakini hao wote imebaki hivyo hivyo mpaka leo hii unasoma haya maandishi. Offcourse,wapo wawili watatu ambao tumeonana wakanielelekeza niombe kazi kwa njia ipi,kama washauri yaani. Lakini yote kwa yote sikupata kazi,nimebaki kama nilivyo hadi mwaka 2015 umeisha.
Baada ya feedback hiyo,sasa naomba tena, Natafuta AJIRA…KAZI…KIBARUA…
Nilishajieleza sana,na kada zangu ni za kawaida yaani siyo za elimu ya Juu sana
√Dreva wa Gari za kawaida.
√Dreva wa Bajaj hasa TVS KING.
√Kuuza duka la aina yoyote isipokuwa duka la dawa za binadamu na mifugo.
√Kusimamia miradi mbali mbali, mfano Restaurant,Bar and Pubs,Sites,etc…
Nipo Mbezi ya Kimara,jinsia yangu ni Me. Umri wangu miaka 26/27. Namba yangu ya simu ni 0718 651 174.
Na ukifungua baadhi ya link kwa Jina la @Nasakadoo utaona maelezo yangu kwa kina. Ila ili kuokoa muda,naomba ni paste hapa chini maelezo yangu nikiomba kwa mara ya mwisho mwaka 2015..
Nitayaweka kama comment, au mods watanisaidia namna ya kuunganisha....

Last edited by a moderator: