tangu nimefika mwenzangu hana kabisa mapenzi na mimi, mapenzi yamepungua kabisa kwangu tangu nimepata ujauzito napenda kula udongo jana kauona kasema SITAKI UDONGO NYUMBANI NDANI KWANGU.
nimejaribu kumuelewesha unatokea nataman tu hata mimi siipendi hanielewi kabisa inshort hana mapenzi na mimi
wanajamvi nifanyeje nimrudishe katika hali yake ya kawaida??? .
tutajuaje huenda wewe ndo ulimlazimisha akupeleke kwao.
Mabint wa kileo shida sana. Ving'ang'anizi.
Alikupeleke ili uridhike, wewe ukatenga na mimba.
Ona sasa.
sio kweli yeye ndio alikua analazimisha kunipeleka kwao
Ulikosea sana dada kushika mimba wakat hujui msimamo wa mwenza wako.
Na kwann ushike mimba wakat hata mahari hujatolewa?
........ Binafsi nawalaumu sana wanawake wanaoridhika na maneno ya wapenzi wao wakat hata hawajaanza hatua hata moja ya ndoa.
Sisi wanaume tunakumbwa na tamaa hvyo tunalazmika kutumia hata udanganyifu lakn tunasahau kuwa tunasababisha watoto wa mitaan
Mimi ni mwanamume, nitakachokuambia ni sahihi kwa asilimia 93.
Huyo jamaa hana mapenzi na wewe kabisaa, hakuwahi kuwa na mpango wa kukuowa na hiyo mimba imeingia bila nyie kupanga kwamba sasa mzae, amekupokea kwa sababu tu hana jinsi, vinginevyo asingekupokea kabisa. Hapop kuna mawili, huenda ukishazaa mtoto anaweza kurejea kwenye furaha yake nakukubali matokeo kwamba tayari ameshakamatika na hana jinsi, baadaye mazowea yatachukua nafasi na kukubali reality. Au kama ni kichwa ngumu basi ndiyo utaishi kwa shida tu namna hiyo.
Ushauri wangu kwako.
Kaa naye mfungukie wazi, mwambie kwa upole akueleze kwa nini hakupendi na amebadilika baada ya wewe kupata ujauzito. Muulize ni nani aliyeingilia furaha yenu, ni huyo mgeni aliyeko tumboni, ni wewe umeishiwa mvuto,ni mapenzi tu yamefika ukomo au kuna mtu mwingine pembeni, usipepese jicho na useme ukiwa umemkodolea bila kurembua jicho. Muulize ni plan gani aliyonayo kwa kuzingatia kwamba kuna mgeni anakuja. Jaribu kushirikisha akil yakokung'amua ukweli.
Mwisho wa siku maisha yako ni wewe, kama mpenzi haeleweki subiri mpenzi wako wa kweli yuko tumboni atakufariji kwa kila kitu, labda kama hauna kipato hilo ni jaribu jingine. Mtoto huwa anakuja na baraka zake, hopefully ukizaa mambo yatakaa sawa, yasipokaa sawa angalia ustaarabu.
ivi kwani MWAFIKIRI NI RAHISI SANA KU LET GO, KULEA MTOTO MWENYEWE DUNIA HII BILA MSAADA WA MUME SI RAHISI, MSIRAHISISHE, WENGI MNAKUJA MWASEMA ETI JIPANGE, HUWEZI LEA MWANAO NA BLAH BLAH KIBAO,
ITS NT EASY.
Kama mtu ana kipato hawezi kulea mtoto?ivi kwani MWAFIKIRI NI RAHISI SANA KU LET GO, KULEA MTOTO MWENYEWE DUNIA HII BILA MSAADA WA MUME SI RAHISI, MSIRAHISISHE, WENGI MNAKUJA MWASEMA ETI JIPANGE, HUWEZI LEA MWANAO NA BLAH BLAH KIBAO,
ITS NT EASY.
ivi kwani MWAFIKIRI NI RAHISI SANA KU LET GO, KULEA MTOTO MWENYEWE DUNIA HII BILA MSAADA WA MUME SI RAHISI, MSIRAHISISHE, WENGI MNAKUJA MWASEMA ETI JIPANGE, HUWEZI LEA MWANAO NA BLAH BLAH KIBAO,
ITS NT EASY.