MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,016
- 16,812
Salaam....
Kwa muda wa takribani miaka minne nimekua ktk mahusiano na mrembo mmoja ambae kwa sasa anasoma chuo kimoja dodoma na mimi nikiwa kanda ya ziwa
Tulikutana masomoni tukafahamiana nikampenda tukaanza mahusiano ambayo mwanzoni yalikua mazuri sana yenye ukaribu kwa hisia japokua ilifika muda tukawa tunaishi mbalimbali japokua ilikua tunakutana kwa mimi kusafiri kumfuata
Mwaka mmoja tu baada ya mahusiano kuanza alibadilika akawa anasema tuachane,anachukia wanaume,na mambo mengi ambayo badae akikaa anaomba msamaha unamsamehe anaendelea....alikuja kufanya jambo kubwa na la aibu ambalo alinificha lakini badae nilikuja kujua nikawa msaada wake mkubwa sana na akaahidi kunipenda kwa sababu kupitia tukio lile alisema aligundua kwamba nnampenda sana ukapita muda mambo yakawa hayaeleweki;ikawa inatokea unampigia sim hapokei text hajibu then ikitokea kapokea anajibu hovyo na anakua mpole na romantic akipata shida tu
To be honest nimemsaidia sana kwa mahaba yangu binafsi na si kitu kingine na nimemgharamia sana binti yule
Na kwa muda huu nimesafiri kuja kumuona lakini anatoa excuse nyingiii mno na mpaka muda huu nimemuona mara moja tu tena kwa dk zisizozidi tano na kwenye alikua anakuja kuchukua vitu nilivyomletea
Mbaya zaidi amekua akichat na watu wengi na tofauti sana akichat nao kwa mahaba sana hadi kufikia kupanga mahala pa kuonana na ukiona ukamuuliza ana kasirika anadai hao ni watu wake nisimuingilie kwa sababu yeye haingilii wangu na mpaka sasa nikawa nimeamuamuru achague watu wake au mimi amekaa kimya hataki kusema
Najua anafanya hivi yote haya kwa sababu anajua anapendwa sana na moyo wangu nevertheless isingekua kwa kiburi hicho
Naombeni ushauri nifanyeje kwa sababu nnampenda sana kutoka moyoni na nikitazama kumuacha nahisi kama kuna kitu kinapungua hivi
Naombeni ushauri View attachment 1163979
Mtangulize haraka Kuzimu.

