Tafadhali naomba mawazo na ushauri kuhusu hili jambo

Tafadhali naomba mawazo na ushauri kuhusu hili jambo

Desire mobutu seseseko

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2018
Posts
1,000
Reaction score
1,466
HABARI wakuu.

Leo nakuja tena kwenu wana jamii najua siwezi kosa ushauri, maoni ya namna yeyote nayoweza maliza hili tatizo langu linalonisumbua kwa sasa. Iko hivi nina mpenzi wangu niliedumu nae kwa takribani miaka 5 inaenda sasa, binti kwao wapo watatu wakike wote yaani yeye ni wa kwanza age 26+ ana elimu ya diploma.

Turudi nyuma kidogo mnamo mwaka 2016 alipata ujauzito nikiwa chuo Mkoa mwingine yeye yupo Mkoa wa kijani. Ilikua shida sana kusolve hili jambo kutokana na ukali wa mama yake. Walinitafuta kupitia dada yake mtoto wa mamkubwa wake kuwa tunasolve vipi tatizo? Mimi nilikua tayari kuwasililiza, walinipa option ya kutoa sababu haikuwa kubwa, niliwatumia kiasi fulan wamalize mchakato. Baadae mawasiliano yakawa hafifu kati ya mimi na binti. Nikablockiwa kila sehemu siweza kumpata tena. Nilijaribu kuwasiliana na dadake sasa yule, akanambia binti alikataa kutoa tena baadae na hawana mawasiliano tena.

Nilijaribu kumtafuta sanaa kujua nini kinaendelea bila mafanikio, hatimae siku zikasogea, miezi kadhaa nikamcheki messenger nikapata mawasiliano naye japo kwa shida sana akaelewa na kupanga kuonana nikirudi mkoa. Na alidai mimba hakuna. Baada ya kufika Mbeya tulionana na hakua na Mimba alikubaliana kuwa pamoja na mimi kuwa bado ananipenda pamoja na mambo magumu alopitia kipindi yuko na Mimba home kwao Mama yake ni mkali sana.

Baada ya hapo nilitaka kujua nini kiliendelea kipindi kile cha ujauzito alinielezea kuwa Alitolewa mimba ikiwa kubwa kabisa na Mama mzazi kabisa alimchukua na kwenda kumtoa bila kuuliza ni ya nani wala maswali mengine kama mzazi baada ya kupona kuwa sawa ndio akaulizwa kuwa ni ya nani ilikua. Binti akamjibu baada ya hapo maisha yakaendelea. Mama hakua na neno tena, zaidi ya kumchukua na kumuweka Vijiti kama njia ya uzazi wa mpango. Ina maana wakati tunarudiana na binti alikua tayari ana hivo vijiti ndani ya mwili wake. Tueliendelea kuwa pamoja, kuhusu relation yangu ndugu jamaa na marafiki hasa upande wangu wanamjua sana! kutokana na side effects za njia hiyo ya mpango alizopitia mwaka huu tulikubaliana tutoe vijiti.

Kwa lengo la kuwa fiti, tulifanikiwa hilo miezi kadhaa nyuma. Sasa ni mjamzito na mama yake tupo mkoa nyanda za kati kikazi anaishi huko. Binti ameenda huko akiwa na mimba kabisa tukiwa tunajua hilo baada ya kukubaliana mimi na yeye kuhusu namna ya kuanza maisha!! akiwa huko mama yake kajua. Binti anapitia changamoto, kusimangwa kuwa amesaliti familia anajali kuhusu yeye tu na maneno makali mno anapewa binti muda huu anakosa raha kabisa na inaonekana mzazi wakw hajakubaliana kabsa na hili jambo sababu amezungumza mengi na kukumbushia ya nyuma na matusi juu. Sijajua yawezekana Mama ana matarajio makubwa sana kwa binti yake..

Hadi sasa sijatoa taarifa yeyote kwa upande wa familia yangu kuwa binti ana ujauzito. NAOMBENI mawazo Mimi ni jobless ila ninaweka sawa mambo shughuli shughuli zangu ndogo ndogo za maisha yaweze kwenda!!

Nakaribisha ushauri na mawazo wakuu!! Ni muhimu sana. Ahsanteni!
 
Mmhh sina cha kusema mkuu ila pole sana
Ila kitakachowafanya muendelee kuwa pamoja ni msimamo wenu wa pamoja wew na huyo binti

Bila kusahau tafuta hela, tafuta hela, tafuta hela
Kama binti amekuvumilia hivo jua hataweza kuvumilia tena umaskini akileta hiko kiumbe duniani so TAFUTA HELA.
 
Mkuu kwani hiyo mimba mlipanga au ilitokea tu bila mipango?

Na kutoa hivyo vijiti mlimahirikisha mama yake?? Wewe bado huishi na wala hujamuoa hivyo ni poa kumshauri maamuzi yenu muwe mnamshirikisha mama yake.

Ingekua poa pia km dem angekua muwazi kwa mamaye, hii ya kumficha ficha mpaka anapata mimba kindezi wakati mnajua maza anamtegemea sana binti huo ni upumbavu wa kutumia hisia zaidi na sio akili.
Na ni ajabu sana hata wewe mwanaume unatumia hisia na sio akili.
 
Ukiwa huna kazi jiepushe kabisa na zinaa...... Epuka kabisa kua kichocheo Cha kuharibu familia na maisha ya mabinti za watu

Lile neno miaka inaenda me nahitaji mtoto, mara naomba nkubebeshe mimba tutalea na wakati we mwenyewe unajua maisha yako hayajakaa sawa kataa kabisa kabisa

Mwisho wa siku matatizo na majukumu makubwa yatabaki kwako ww baba kwa mama kazi yake haitakua kama yako

Usijiingize kweny ndoa kama unajua maisha yako bado hayajakaa sawa utakufa na pressure ma magonjwa mengine yanayohusishwa na moyo

Ukiona mtoto wa mwenzio amevaa amependeza unaweza hisi gharama gharama unaweza zimudu ingia kweny kuitafuta hiyo pesa ya kununua nguo za mtoto ndo utajua maisha na majukumu ni yako pekee.
 
Pole Sana ila jamiiforum hutapata majibu SI wenyewe tumevurugwa mambo mengi vichwani..kwani hukuwa na smartphone ya kupigia nyeto??
 
Mama anatarajia mwanae achumbiwe wafanye bridal shower kitchen party send off na harusi kubwa wewe jambazi la kitanzania unachukulia normal tu

Mkuu shukuru hajaingiwa na wazo la kalumanzila
 
Kama unampenda kweli kwa nini usimuoe ndo mtoe hivyo vijiti?
Huna nia nzuri na binti wa watu wewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom