Tafadhali kuwa na huruma

Tafadhali kuwa na huruma

Tumejijengea hiyo hulka hasa sisi wanaume kuanzisha mahusiano ya kujifanyisha kwamba kweli unampenda kumbe unafanya hivyo kutimiza azma yako dirty mind.
Mwenzio anaamini hivyo kwa kupima urefu wa maji na miguu yote na mwili wote anazama anakufa huku ukimuangalia na kuchekelea!c umeshapata ulichotaka!!
Kweli kweli kabisa wanaume kupenda mwanamke huwa % chache sana ila tamaa %kubwa tamaa kubwa mfano wa bahari na kupenda ni mfano tu wa boti.
Wanawake wana mioyo sana jinsi tunavyowafanyia ingekuwa sisi tunatendwa hivyo dunia isingekuwa mahali salama WW3!
Umaweza kuwa na pesa ukamtaka mwanamke akakubali kwa kukupenda kwa dhati bila pesa zako ila sababu ulishakuwa na wale wanapkupendea pesa basi utamtreat huyu hivyohivyo bila kujali hisia zake za kweli kwako!
Amini usiamini ni wanaume wachache sana wanapenda wapendwe na mwanamke ila wengi hupenda akishamega apite hivi ndivyo ilivyo
 
View attachment 373517




Sio sawa kabisa kuingia katika mahusiano na mtu na kumfanya atengeneze hisia za kukupenda wewe, kumfanya mtu aamini kuwa wewe ni wa tofauti na wale wote ambao wamekwisha muumiza kihisia hapo mwanzo.

Anakuamini na anakukabidhi moyo, mapenzi na mwili wake, anakutegemea wewe, anapanga kesho yake pamoja na wewe, ana sucrifice kile kidogo alicho nacho kwa ajili yako.

Anajivunia kuwa na wewe kiasi cha kukutambulisha kwa familia yake na marafiki zake wote wa mbali na wa karibu, anabadilisha tabia yake kwa ajili yako, anaacha tabia zake fulani kwa ajili yako.

Muda mwingine anapoteza kazi fulani kukufuata wewe huko unakoishi kwa ajili ya wewe, anakuwa na maadui kwa ajili yako na anatukanwa na watu kwa ajili yako.

Wewe kwa ujinga wako au kwa ujinga juu ya jambo la kipumbavu, unamuacha yeye au unamtelekeza au unamuumiza kihisia, haumpendi tena. Unasahau ni yepi amepitia au mlipitia pamoja. Umesahau ahadi nono ulizomueleza hapo mwanzo, umesahau kila kitu kabisa

Unaanza kumuona ni ******** na ni mbaya kiasi gani, unaanza kumuita majina ya ajabu ajabu na kumtukana matusi ya nguoni, unakana mbele yake na kumwambia watoto si wako

Sio sawa ndugu yangu, inaumiza mno, ni maumivu makali sana moyoni, moyo unavuja damu, maumivu hayaponi kirahisi. Unaweza kuwa umefanya hivyo kwa kuwa na wewe ulifanyiwa hivyo kipindi cha nyuma na watu wengine ila sio busara kumfanyia mwenzako ambae hana hatia.

Unaweza ukachukulia kama ni mchezo fulani. Ila amini me nakwambia MUNGU hana furaha na hicho ulichokifanya na wewe pia.

Tafadhali sana nimejifunza kamwe usimfanye mtu akupende katika mahusiano wakati unajua kwamba haumpendi na hautadumu nae siku zote. Kamwe usimpumbaze mtu au kumtumia kwa faida zako.

Kuwa na huruma na huo moyo wa mpenzi wako uliojaa mapenzi na ambao hauna hatia masikini ya Mungu. Bila shaka unanisoma hapa, nenda ukamwambie ukweli kuhusu mustakabari wa mahusiano yenu. Nenda tafadhali, mueleze ukweli! Usimfiche, usiendelee kumdanganya na kumpa ahadi kedekede wakati unaona kabisa hilo jambo haliwzekani.!

Onyesha hekima yako angalau mara moja tu sasa hivi na Mungu atakubariki.


Pole sana kwa wale mlotendwa, upo na mtu ambaee macho yake km kicheche shimoni anahis nje kuna aduii pia poleni wale wenye wapenzi wenu mnawaamini sana lkn anakudharau na wewe unayependa zaidi ya mmoja amua moja ni yupi wa kuwa nawe, usiendelee kuumiza watoto wa watu.

Mapenzi matamu pindi umpatapo mwemye kujua nini maana ya mapenzi na wajibu kwa mpenzi na si kuleta drama katika moyo wa mtu uliokuwa serious na upendo juu yako......!








PRINCE NAAHJUM ALSINA
 
Kwani siku hizi kuna mapenzi ya kweli jamani au imebaki mazoea tu....??
Wengi wanasaga meno au walisha kufa wadudu
 
Difinition ya Love ni kuwa Unaempenda kwa dhati na moyo wako wote yeye hakupendi,ila Yule usiempenda kwa dhati yeye hajiwezi Kwako! Hivyo chaguo ni moja tu either umpende asie kupenda ila ukubali kuvumilia au umpende anaekupenda uishi raha mustarehe
 
samahani ndugu mtoa mada!! hapo umeongelea/umemsemea/umemtetea mwanamke ambaye ameolewa au anaishi na mume wake!! swali ni je? kwa wenzetu mnaooa hata wanawake wanne inakiwaje? hawa wanawake huwa hawafeel depressed kuona mwenzake anaongezeka?mean huu upendo na ma care yote mnayagawa vp? provided kwamba love haigawanyiki,na je unadhani hawaumii kweli na kuvunjika moyo pale unapoongeza mwingine?...nadhani umenielewa kidogo,nijibu kwa hekima na sio kwa mihemko
Prince Naahjum @Alsina
 
Back
Top Bottom