Tafadhali Kikwete, tumia nafasi hii... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafadhali Kikwete, tumia nafasi hii...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Apr 4, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Mpendwa Mwenyekiti wa Chama,

  Ninayo heshima kubwa kukufahamisha kuwa ndani ya chama chako hakuna kundi hata moja lenye nguvu zaidi yako.Mtazame Lowassa.Pamoja na kuwa Laigwan na mkwe wa mgombea,wenzake wamemuona mchafu.Wakamkataa mkwewe na yeye pia.Akashindwa.

  Mtazame Sitta.Pamoja na kumuunga mkono 'Masamaki' pale Kirumba Mwanza,ameshindwa.Watazame vijana wako Nape na Lusinde.Chama chako kinawachukulia hawa kama hazina ya baadaye.Hazina hii haitafaa.Hawa wamejaa kejeli,matusi,propaganda,tambo na porojo.Wameshachaha mapema.

  Mtazame Benja.Pamoja na kutegemewa kama Mzee wa Busara wa chama,aliacha hoja na kujikita kwenye ukoo usiomuhusu.Akaumbuka.Yeye na Wasira,Sendeka na wazee wengine wameshapungukiwa busara za kukinusuru chama na kushindwa.Hawafai kuongoza kampeni nyingine yoyote,popote.

  Tumia nafasi na nguvu yako kama Mwenyekiti kudhibiti chama chako.Wavue na wavike magamba wanaostahili.Usimuonee haya mtu.Urafiki,ukaribu na utaratibu wako hausaidii kitu.

  Tukutane 2015 au kwenye chaguzi yoyote ndogo uambulie hata nafasi ya pili.Mimi si mwanachama wa chama chochote kwa kukosa kadi husika.Lakini, naiunga mkono CHADEMA na watu wake.Napenda mabadiliko.Peeeeeeeooooopleeeeeee's!!!!!!!
   
Loading...