Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,786
Watumishi kumi na moja wa shirika la Reli nchini (TRL) wa karakana ya Tabora wanashikiriwa na Jeshi la Polisi kupisha uchunguzi wa kina, katika kile kilichodaiwa kuwa,ni kuhusika katika kuhujumu shirika kwa kuuza mafuta ya Dizel ya kuendeshea Treni.
Akizungumza na ITV katika ofisi za shirika hilo mjini Tabora Kaimu Mhandisi wilaya Tabora Mhandisi,Edgar Bakuza amesema,baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza walibaini kuwepo na wizi mkubwa wa mafuta,na kukamata lita ishirini na madumu zaidi yaliyokuwa yamefichwa kwa ajili ya kupatia tena.
Aidha amesema kuwa,wilaya ya Tabora yenye njia za reli za Mwanza, Kigoma na Mpanda imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya wizi wa mafuta aina ya Dizel ka kusababisha utendaji kuwa duni huku treini za mizigo na abiria kulazimika kusimama njiani,na kukamatwa kwao kutakuwa fundisho.
Wakizungumzia changamoto inayoikabili karakana hiyo ya Tabora, baadhi ya wafanyakazi wamesema kuwa,eneo la karakana halina uzio hali ambayo imekuwa akiwapa wakati mgumu,kuwadhibiti waarifu,hoja iliyopingwa na mhandisi akidai hoja kubwa ni waadilifu na sio uzio.