TABORA: Jeshi la Polisi lakamata kilo 100 za bangi

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
bangi-bangi_210_120.jpg
​

JESHI la polisi mkoani Tabora linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na bangi kiasi cha kilo 100 kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana kamanda wa polisi mkoani Tabora, Wilbrod Mutafungwa alisema kwamba bangi hiyo ilikamatwa kwenye basi la Dar Lux lenye namba za usajili T 332 DGC aina ya HIGHER linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam.

Alisema kwamba jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wananchi wema kwamba kwenye basi hilo kulikuwa na mabegi sita yote yakiwa yamebeba kiasi kikubwa cha dawa za kulevya aina ya bangi.

Kamanda huyo wa polisi alisema kwamba mara baada ya basi hilo kuwasili wilaya ya Nzega majira ya saa kumi jioni na baada ya kufanya upekuzi ndani ya buti za gari walikuta kiasi hicho cha bangi kikiwa kwenye mabegi sita.

Aliwataja waliokamatwa na bangi hiyo kuwa ni madereva wa gari hilo, Philipo Musa (35) na Said Ngozo (43) wote ni wakazi wa mkoani Iringa na kuongeza kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya jeshi hilo kukamilisha upelelezi wa shauri hilo.

Chanzo:HabariLeo
 
Wamekosea itakua ni zile tumbaku wamefananisha na bangi
Siku hizi intelijensia imehakiwa hata vinavyoonekana havijulikani
 
JESHI la polisi mkoani Tabora linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na bangi kiasi cha kilo 100 kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana kamanda wa polisi mkoani Tabora, Wilbrod Mutafungwa alisema kwamba bangi hiyo ilikamatwa kwenye basi la Dar Lux lenye namba za usajili T 332 DGC aina ya HIGHER linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam.

Alisema kwamba jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wananchi wema kwamba kwenye basi hilo kulikuwa na mabegi sita yote yakiwa yamebeba kiasi kikubwa cha dawa za kulevya aina ya bangi.

Kamanda huyo wa polisi alisema kwamba mara baada ya basi hilo kuwasili wilaya ya Nzega majira ya saa kumi jioni na baada ya kufanya upekuzi ndani ya buti za gari walikuta kiasi hicho cha bangi kikiwa kwenye mabegi sita.

Aliwataja waliokamatwa na bangi hiyo kuwa ni madereva wa gari hilo, Philipo Musa (35) na Said Ngozo (43) wote ni wakazi wa mkoani Iringa na kuongeza kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya jeshi hilo kukamilisha upelelezi wa shauri hilo.

Chanzo:HabariLeo
Ikiuzwa kwa bei shirikishi inaweza kusaidia kuinua kipato cha jeshi letu la kamatakamata!
 
Wakikamata kilo 100 za BANGI wanatangaza. Subiri wakanate kilo 100 za Cocaine....
 
Alisema kwamba jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wananchi wema kwamba kwenye basi hilo kulikuwa na mabegi sita yote yakiwa yamebeba kiasi kikubwa cha dawa za kulevya aina ya bangi.

Na walaaniwe wenye kutoa hiyo taarifa kwa sababu sio ajabu kuwa wao walichukua chao mapemaa kabla gari haijatoka Mwanza lakini wakawachomea wenzao nguru. Hebu fikiria, huyo dereva na utingo wangeliamua wakabadilishia mizigo gari jingine si mzigo ungelifika darisalama salama??
Ningelikuwa polisi, ningefuatilia huyo mtonyaji naye aisaidie polisi.
 
Aisee, jamaa yangu alikuwa ndani ya basi hili ,basi lenyewe lilishikwa mida ya saa tatu wakaachiwa saa 10 kuendelea na safari.... Waliingia dar kesho yake saa 9 alasiri...Ila to be honest, mtu anawezaje kusafirisha kiasi chote hicho kwa basi la abiria? Anyway kuna mtu alichomesha and ku-deal na hayo majani ni against na sheria za jamhuri.
 
Back
Top Bottom