TABOA Wasitisha mgomo wa Mabasi baada ya kukubaliana na Waziri Mbarawa

Ratile

Senior Member
Oct 13, 2012
191
104
TABOA wasitisha mgomo baada ya makubaliano na Waziri Mbarawa ya kurekebisha mapungufu yaliyofanya watake kugoma ndani ya siku 14.


C8fR-uZXUAAtl6b.jpg

Wakati huohuo, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), leo imesema inayafanyia kazi madai yaliyotolewa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (TABOA) pamoja na Umoja wa Wasafirishaji wa Abiria jijini Dar es Salaam (UWADAR). Hii ni siku moja baada ya vyama hivyo kutoa tamko la kutaka kusitisha huduma ya usafirishaji kuanzia siku ya Jumanne.

Hata hivyo, SUMATRA kupitia Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara, Johasen Kahatano imesema hakuna muswada wowote uliopelekwa bungeni wala suala la kusomwa kwa mara ya mwisho kwa muswada wa sheria inayotaka mmiliki wa gari kushitakiwa au kuhukumiwa kwa kosa alilofanya dereva.

“Hakuna kitu kama hicho, labda kama kuna kiongozi mwingine hapa katika mamlaka anayefahamu hilo, nitakupa namba ya simu ya Mkurugenzi Mkuu umuulize kama kuna jambo kama hilo,” alisema Kahatano.
View attachment 490693
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw. Gillard Ngewe (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea kusitishwa kwa mgomo uliopangwa kufanywa na wasafirishaji wa abiria na mizigo nchini, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani (TABOA) Bw. Abdallah Mohamed na kushoto ni Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala mkoa wa Dar es Salaam (UWADAR) Bw. Kismat Jaffar.

Vilevile alisema kuwa hajui wamiliki wa mabasi walikozipata taarifa za muswada huo na leo SUMATRA inaweza kuangalia nini cha kufanya kabla ya kuanza kwa mgomo wa mabasi hayo.

Wamiliki wa mabasi walitangaza kusitisha huduma za usafirishaji kuanzia kesho jumanne ikiwa ni kwa lengo la kupinga sheria ya SUMATRA Sura ya 413 na ile ya Leseni za Usafirishaji Sura ya 317, inayotaka mmiliki wa gari kushtakiwa au kuhukumiwa kwa kosa alilofanya dereva.

Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu akisoma mapendekezo yaliyotolewa kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho alisema mgomo huo siyo wa mabasi tu, unawahusu pia wasafirishaji wa malori pamoja na bajaji.

Hata hivyo wamiliki hao wa mabasi, leo walikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kuhusiana na namna ya kuyafanyia kazi madai yao.

Mkutano huo wa Waziri Mbarawa na TABOA umefikia makubaliano kuwa mgomo usitishwe na madai yao kushughulikiwa ndani ya siku 14.
 
TABOA wasitisha mgomo baada ya makubaliano na Waziri Mbarawa ya kurekebisha mapungufu yaliyofanya watake kugoma ndani ya siku 14.
aaf9bd497b7f2f32ea317fe3448f0b75.jpg
 
Hakuna mgomo walikuwa wanatishia tu! Awamu hii migomo iko likizo unatishia tu afu unazuga kuwa memukubaliana. Hapo hamna marekebisho wala nini.! Goma unyan'ganywe leseni yako afu una mabasi ishirini sijui utayapeleka wapi!
Walitishia 'kujamba" wakati wanaumwa tumbo la kuharisha...
 
Rais Magufuli anatakiwa kuivunja hii Sumatra kwani imekuwa ni idara yenye matatizo sana. Kila siku na sheria mpya.
 
Nashangaa mtu anacomment eti awamu hii hakuna mbabe wa kugoma, wakati kilichofanya Taboa watangaze kugoma wamekubaliwa kinafanyiwa kazi, sasa mnataka wagomee nini?
Kuna watu wajinga sana nchi hii. Wamejawa uchama hata kwenye mambo ya msingi. Tanzania ni ya wananchi siyo Mali ya magu
 
I wonder how the clients us who board the buses will organize a coup against the hijacked tariffs and fairs we pay day by day!!...... our decisions will be met on 2020 against the outgoing government!
 
Back
Top Bottom