TABOA NA UWADAR wadai hawajatangaza mgomo wa mabasi Jumanne

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Chama cha wamiliki wa mabasi TABOA na chama wamiliki wa daladala mkoa wa Dar es Salaam-UWADAR-wamesema hakutakuwa na mgomo siku ya jumanne na wataendelea kutoa huduma ya usafiri nchini nzima kama kawaida mbaka mkutano mkuu wa taboa unaotarajia kufanyika siku ya jumatano utakavyoamua.

Akizungumiza na vyombo vya habari kutokana na kuwepo kwa taarifa katika mitandao ya kijamii inatangaza maamuzi ya mgomo wa mabasi, mwenyekiti wa UWADAR Bwana Kismati Jaffar amesema kipande cha video kinachirishwa mitandaoni ni tukio ya mwaka jana, na halina na uhusiano na mgogoro uliotangazwa TABOA dhidi ya SUMATRA hivi karibuni.

Akizungumzia kanuni inayoleta mgogoro kati ya TABOA na SUMATRA, mweka hazina wa TABOA Bwana Issa Nkya amesema vyama hicho vinaendelea kusisitiza kutenganishwa na makosa kati ya mmiliki na dereva pamoja na faini ya shilingi lakini mbili na nusu ni kubwa sana.

Mkurugenzi wa huduma za sheria wa mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu na majini-SUMATRA- Bi Tumaini Slaa amesisitiza kuwa kanunia hizo zimezingatia na kutenganisha majukumu na adhabu kati ya mmiliki wa leseni na madereva,huku kaimu mkurugenzi wa uthibiti wa usafiri barabarani Bw. Leo Ngowi amesema SUMATRA inawasiliana na TCRA ili kuchukua hatua dhidi aliyesambaza taarifa hizo.



ITV
 
Kuuliza si ujinga, nimeona daladala nyingi zina namba iliyozungushiwa zikianza na mfano (S 123876 G), je hizi zinasimama badala ya nini
 
Back
Top Bottom