tablet za bei rahisi zaidi

tablet za bei rahisi zaidi

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,062
Reaction score
43,492
Kuna mdau aliwahi kuandika tablet ya google ya bei rahisi google nexus 7 sio vibaya tuka update zaidi kwa kuongezea tablet 2 nzuri zaidi kwa urahisi kuliko google nexus.

amazon kindle fire
Bei yake sasa imeshuka ni dola 159 aproximately hela za tanzania sh 240,000
gsmarena_013.jpg


humu kuna 8gb storage, mult touch (2 finger) processor 1.0 ghz dual core ram ni 512mb na inatumia android 2.3 gingerbread

Ni nzuri kwa matumizi ya kawaida kama kusoma vitabu na kuangalizia movie za safari. Kama una pc nzuri na kila kitu unafanya kwenye pc hii ni tablet yako.

amazon kindle fire hd
Hii bei yake ni dola 199 aproximately shilingi laki 3 za kibongo
amazon-kindle-fire-hd.jpg

Hii imeongezeka memory ni 16gb na unaweza touch na vidole 10 pia processor ni dual core katika clock speed ya 1.2 na ina ram 1gb. Os ni android 4 ice cream hii inakidhi mahitaji yote muhimu

blackberry playbook
Tablet ya ukweli kwa laki 2 na nusu tu.
blackberry-playbook.jpg

Hii tablet weakness yake inatumia os yao ya bb lakini myself nshaitumia ipo vizuri sana na nlikua suprised na urahisi wake maana bb wao wanauza ghali sana vitu vyao

Ina 5mp camera na kile cha video call ni 3mp ina hd na 16gb storage ina 1gb ram dual core 1ghz processor

Hizo tablet 3 ukijumlisha na ile nexus 7 unapata tablet rahisi duniani ambazo zinatoka makampuni yasiyo ya kulipua kama bidhaa za china
 
Asante mkuu, je zinapatikana wapi hapa Bongo.
 
kwa kindle fire hd imeanza kuuzwa mwezi huu wa 9 ntakudanganya nkikwabia ipo madukani japo zinaweza kuwepo.

Ila kwa kindle fire ya kawaida bila hd na blackberry playbook vipo madukani posta kkoo.

Na hizo bei nlizotaja ndo bei za reja reja walizotangaza kwenye website zao (hua kwa jumla wanauziwa rahisi wauze bei hio)
 
Aisee cheaf unge weka thread kama hii inayo husu laptops ingekua mwake zaidi.
:focus:
Hapo bashauli mtu achukue kindle fire HD au Nexus 7 na aachane na Playbook kwasababu kuu moja RIM wanapotea kutokana na kutofanya vizuri kwa new flagship zo pia na ueingi na uhuru wa apps zao.

turudi kwenye Kindle Fire HD Vs. Nexus 7
hapa kuna ushindani kidogo ila mwisho wa siku Nexus 7 anashinda
 
ipi nzuri kati ya urahisi wa bei au ubora wa kitu
 
unafikiria zikija bongo zitauzwa bei hiyo I'm sure the cheapest huku watauza 600,000
 
hizi ndo bei za kuship kuja tanzania kutoka amazon (wauzajia na watengenezaji wa kindle fire)

kama unahitaji kwa haraka itafika siku 4 hadi 7 na utachajiwa dola 9.99 tuseme dola 10

na kama huna haraka itafika siku 18 hadi 30 na utachajiwa dola 6.99 tuseme dola 7


lets say una haraka kindle fire hd dola 199 + shiping dola 9.99 hii sawa 208.9 tuseme 210 itakukost kama laki 3 na elfu 20 hivi sio mbaya.
 
Miaka inakimbia na kupotea kama moshi, 2012!
 
Miaka inakimbia na kupotea kama moshi, 2012!
Balaa sana almost miaka 12 imepita! Umri wa dogo amabe kama alizaliwa mwaka huo basi kamaliza darasa la 7 au ndiyo yupo darasa la 7...
 
Back
Top Bottom