Tabiri Top 4 yako VPL

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,713
45,090
Baada ya mechi ya ngao ya jamii kupigwa, ni kiashiria tosha kuwa ligi inakaribia kuanza.

Timu zimejiandaa vizuri, kuanzia kwenye usajili wa vikosi vyao mpaka kwenye benchi la ufundi.

Huu ni msimu ambao timu kama Yanga imejiandaa kweli hasa kwenye usajili wa wachezaji wa kimataifa kama vile Mukoko na wengineo, lengo ikiwa ni kufuta ufalme wa Simba, huku Simba nayo ikijiimalisha vya kutosha kama maingizo mapya ya akina Bwalya na Onyango. Azam Fc inakimbiza mwizi kimya kimya, KMC wapi kama hawapo, Namungo ndio kama hivyo ina kikosi kizuri chenye morali. Bila kuwasahau timu kama Polisi Tanzania, Ihefu, Kagera na Mtibwa Sugar.

Tabiri nani atakuwa bingwa na top 4 kwa ujumla.

Kwangu mimi, Bingwa ni Simba Sc kwa mara nyingine. Top 4 yangu ni hii;
1. Simba Sc
2. Azam Fc
3. Yanga Sc
4. Namungo

Karibu na wewe uweke utabiri wako...
 
Baada ya mechi ya ngao ya jamii kupigwa, ni kiashiria tosha kuwa ligi inakaribia kuanza.

Timu zimejiandaa vizuri, kuanzia kwenye usajili wa vikosi vyao mpaka kwenye benchi la ufundi...
Kadi yako ya uanachama wa mikia ni namba ngapi vile?!?
Ukweli mchungu lakini timu yangu Yanga itamaliza nafasi ya 4.

1.Simba Sc
2.Azam Fc
3.Namungo Fc
4.Yanga Sc
Tuambie namba yako ya kadi ya uanachama wa mikia...
 
Top 4 inasimama kwa ajili ya nini kwenye ligi yetu?

I mean, nini umuhimu wa kuwa namba 3 na 4 kiasi cha kuzijadili hizo nafasi?
 
Mkuu mimi ni Yanga damu lakini bado hatuna timu ya kuchukua ubingwa, kwenye ukweli tuseme tu.
Sasa kama huna timu ya kuchukua ubingwa povu la Nini...wewe siyo Yanga...Kama ni hivyo ni shabiki mfuata upepo...hakuna Cha Yanga damu hapo..Yanga wa ukweli ni watu makini...huwa hawaropoki na kulalamika ovyo ovyo...wewe hapo ulipo ni mshabiki oyaoyaoya ila siyo Yanga..
 
GSM imewasajilia Yanga matatizo kwani ujue mishahara ndio litakuwa tatizo kubwa kwa Yanga.Hela za mishahara watakosa na wachezaji hawataonyesha kiwango
1.Simba
2.Azam
3.Namungo
4.Police Tanzania

Yanga bado inaendeshwa kiswahili sana kama ianze kuimarika kama taasisi itachukua kama miaka 3 na approach ya GSM ya kuwanunulia wachezaji na kuwanunulia wasemaji au wahasishaji wa Timu unaendelea kuibomoa Yanga.

Angalia suala dogo tu kama msemaji wa Timu pale Yanga ni vurugu.Kuna Bumbuli, Baba Levo, Antonio Nugaz na wote hawajui kazi yao. Mwakalebela au Msola ukimuuliza mishahara GSM walikubaliana shs ngapi kwa mwezi hata hawajui na huyo Senzo hana kazi hapo
5.Yanga
 
Yanga kwasasa changamoto zake si vikombe vya Tanzania, Hakuna kikombe chochote apa nchini kinacho simamiwa na Tff ambacho Yanga haongozi kwa kukichukua. Changamoto za Yanga ni kimataifa apa ndani Simba ndio wanatakiwa kupambana kufikia mafanikio ya Yanga.
Mawazo ya kijinga Sana, kwa hiyo ukichukua ubingwa mara nyingi unaacha kwanza miaka kadhaa?

Sema hivi utopolo hamna uwezo wa kupambana na mnyama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom