Tabia za watu waliofanikiwa

Tabia za watu waliofanikiwa

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Moja ya tabia ya watu waliofanikiwa ni watu wasiopenda kabisa kupewa vitu vya bure.Free lunch,free sijui nini nk
Ukitaka kuwakosa watu waliofanikiwa kwenye jambo lako wambie tu kuwa ni buree kamwe hutawaona kabisaa.

Na ukitaka kujua kuwa na wewe umekua na unaingia kwenye list ya watu waliofanikiwa utaanza kuchukia kulipiwa au kupewa vitu vya bure ambavyo hujavifanyia kazi.

Hata ikitokea mmetoka out na watu hata kama kuna mtu unaona ana uwezo wa kulipa Bill utakataa na kutaka kulipa walau kushare gharama iliyo tumika hata kama ni kulipia tu vinywaji.

Na hata ikitokea umealikwa sherehe na unajua kuwa kila kitu kipo na kimelipiwa walau unabeba zawadi kuwapa wale waliokualika walau ushiriki kwa namna moja ama nyingine.
Kumbuka hawa watu waliofanikiwa hawataki kabisa kupewa bure kitu,maana wanaamini kuwa cha kupewa bure hakina thamani.

Watu waliofanikiwa huamini kutoa kuliko kupokea.
Kwao, kutoa ndiyo njia ya kuongeza, si kupokea.
Na zaidi, wanathamini kile walichokitolea jasho, si walichopewa bure.

Wewe je? Uko kundi lipi?
Umeanza kuchukia "vya bure bure"? Basi karibu kwenye familia ya watu waliofanikiwa.
Unaweza kubadili mtazamo wako na Unaweza kuwa mmoja wa watu waliofanikiwa .
Mfalme Daudi alikataa kupewa vya bure
Esau alikataa kupewa vya bure na ndugu yake Yakobo. Ibrahimu alikataa kupewa ardhi bure kwaajili ya kumzikia mke wake Sara bali aliinunua (Mwanzo 23:17-18)
Ibrahimu Aliikataa zawadi ya bure kutoka kwa mfalme wa Sodoma (Mwanzo 14:23)

Daudi alikataa kumpa Mungu sadaka ya bure.
Wakati Daudi aliponunua kiwanja cha Arauna ili kumtolea Mungu sadaka (baada ya pigo kwa Israeli), Arauna alitaka kumpa kiwanja na sadaka bure. Lakini Daudi alikataa.

Lakini mfalme akamwambia Arauna, La! lakini nitakinunua kwako kwa thamani yake; maana sitamtolea Bwana, Mungu wangu, sadaka za kuteketezwa nisizozilipia gharama.”( 2 Samweli 24:24)

Ikawe amani,kibali na utoshelevu kwako
Bure ina gharama kubwa kwako kiroho.Toa ili upokee,kubali kulipia gharama ili ukue.
 
Hata pia usipende kuonewa huruma mtoto wa kiume et kutegemewa kupokea tuu..

Maana kama tabia ya mtu aliyefanikiwa ni kutoa unazani anayepokea ni nani...

Hayo yamekaa ki mahubiri mahubiri..
Mnawaza wenzenu watoe tuu mda wote..

Ukijiona na wewe unapenda kupokea pokea jua kuna shida na kitalam inaitwa hormonal imbalance XXY
 
Kupenda kuonewe huruma hasa kwa moto wa kiume ni ujinga uliovuka mipaka, ni ujinga ujinga ujinga!

Ni upumbavu!
 
Kupenda kuonewe huruma hasa kwa moto wa kiume ni ujinga uliovuka mipaka, ni ujinga ujinga ujinga!

Ni upumbavu!
Ukiona mtoto wa kiume anapenda kuonewa huruma maana yake anapenda kupokea na ndo hyo huyo anashawishi wenzake et wawe wanatoa tuu ndo kufanikiwa....

Kiufupi mtoto wa kiume ukipenda kuonewa huruma watakukula live live...

Sio kukukula tuu yaani unakua tayari ushajiunga na upinde mazima...

Toto la kiume hata kulalamika lalamika ni upinde pia..
Mtoto wa kiume kaza tuu
 
Eti jamaa yangu mmoja alikuwa anaumwa akapelekwa hospitalini nami kwa sababu nilibanwa na majukumu sikupata wasaa wa kwenda kumjulia hali. Baada ya kutoka akaanza kunilalamikia eti ananiambia mimi siyo mwana.

Nyambafu sana yule jamaa 😎.
 
Hapo mapaka ya baa umeyapa za uso. Kuna mtu anaoga vizuri anachomekea shati kisha anapitapita kwenye mabaa kuangalia kama kuna yeyote anayemjua amuombe bia. Shiti kantrii
 
Eti jamaa yangu mmoja alikuwa anaumwa akapelekwa hospitalini nami kwa sababu nilibanwa na majukumu sikupata wasaa wa kwenda kumjulia hali. Baada ya kutoka akaanza kunilalamikia eti ananiambia mimi siyo mwana.

Nyambafu sana yule jamaa 😎.
Jamaa ako kiufupi ni upinde hata kama sio upinde basi jua ana ugonjwa wa XXY..

Mi mdogo angu kila siku analalamika na nikimwambia aache huo ushoga.
Ananisemelewa kwa bi mdashi hapo nasemwa tuu..

Sasa dogo nimemkataa nimemwambia mpka aache umama wake...
 
Tabia ya kudekeza mtoto kiukweli mimi Sina.
Mtoto wangu wa kiume akipokea cha bure ana maswali ya kujibu.
 
ujinga ujinga tuu..
Hapa mtaani tunao kibao an mpaka kero aiseee an mtu kutwa kusifia wenzake mara tajiri mara boss...

Wakitegemea kupata kitu kwako...
Mi inanikera sana aisee
Mimi tangu nikiwa mdogo hata nikilewa kitu na kaka yangu wa damu huwa nasita kukichukua, lakini nashangaa Kuna vijana wa kiume wanaomba hela kwa watu ambao hata hawana ukaribu nao sana na wakinyimwa wanalalamika kama mtoto wa kambo.
 
Mkuu umeongea vizuri sana ila kuna kitu umekiacha hapo:

Sisi tuliofanikiwa tunapenda sana kutoa lakini hatupendi kuombwa, na hiyo ndio sababu hatupendi vya bure, mtu akikupa kitu bure kesho anaweza kuhitaji cha kwako kwa njia hiyo hiyo.

Cc: Binti Sayunii
 
Mimi tangu nikiwa mdogo hata nikilewa kitu na kaka yangu wa damu huwa nasita kukichukua, lakini nashangaa Kuna vijana wa kiume wanaomba hela kwa watu ambao hata hawana ukaribu nao sana na wakinyimwa wanalalamika kama mtoto wa kambo.
Mtoto wa kiume unaomba pesa...
Mtot wa kiume unaomba uonewe huruma...

Alafu watu wa namna hiyo wanajiona wajanja wajanja mjini hapa kumbe ni ujinga ujinga tuu..

Mi kuvaliana nguo hapana aiseee
 
Back
Top Bottom