Tabia za hovyo kwenye biashara

Tabia za hovyo kwenye biashara

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
65,015
Reaction score
111,404
Tabia hizi ukiziruhusu kwenye biashara yako utaendelea kufanya biashara ya ya kipato cha mkono kwa mdomo tu, hutakaa ukue na kufanya biashara kubwa

1. Kuruhusu watu wasiohusikia na biashara yako kuja kupiga story kwenye biashara yako,hii ni tabia ya hovyo sana ambayo unaweza kuikuta hata kwenye maduka ya madawa ambapo ungetegemea kungekuwa na kuzingatiwa kwa usiri wa wagonjwa kwa kiasi cha hali ya juu.

2. Kushindwa kuuza bidhaa kwa sababu huna chenji. Kama unajua kuna watu watakuja na pesa kubwa nunua hata chenji, usiache kuuza kisa umepewa pesa kubwa, ni ujinga sana.

3. Kujibu wateja vibaya au kuwapuuza

4. Kuchelewa kufungua biashara asubuhi au kumhudumia mteja.

5. Kukosa vifungashio vya bidhaa

6. Kutokowa na bidhaa au huduma ambazo ungetegemewa kuwa nazo.
 
Kuna watu wanaenda kwa waganga wanapewa mbinu zinazoendana na hivi hivi na baadaye wanafanikiwa na wanazidi kuamini kwenye ushirikina.

Mfano:
1. Mganga anakupa dawa unaweka kwenye draw anakuambia iyo dawa asione mtu yoyote. Maana yake mtu yoyote asiguse pesa kwenye draw yako hivyo hutakuwa na upotevu wa pesa.

2. Mganga anakuambia fungua duka saa 1 na uwe wa mwisho kufunga kulinganisha na majirani zako.

Na mengine mengi
 
3. Mganga anakupa sharti la kutozichanganya hela za biashara na hela nyingine hapa ni kuwa anakufundisha usiwe kama jpm ambae kakusanya pesa zote kwenye centralised acc( HAZINA) alafu anazitumia kwenye miradi ambayo haijapitishwa wala kuplaniwa na bunge mwisho wa siku hela za kumalizia project zenye kipaumbele na taifa zinakosekana na kuanza kubuni njia za kihuni za kukusanya hela kwenye jamii.
 
3.Mganga anakupa sharti la kutozichanganya hela za biashara na hela nyingine hapa ni kuwa anakufundisha usiwe jpm ambae kakusanya pesa zote kwenye centralised acc( HAZINA) alafu anazitumia kwenye miradi ambayo haijapitishwa wala kuplaniwa na bunge mwisho wa siku hela za kumalizia project zenye kipaumbele na taifa zinakosekana na kuanza kubuni njia za kiuni za kukusanya hela kwenye jamii.
😀😀😀😀😀😂😂😂😂 comment ya kukaribishia wiki mpya hii.
 
3.Mganga anakupa sharti la kutozichanganya hela za biashara na hela nyingine hapa ni kuwa anakufundisha usiwe jpm ambae kakusanya pesa zote kwenye centralised acc( HAZINA) alafu anazitumia kwenye miradi ambayo haijapitishwa wala kuplaniwa na bunge mwisho wa siku hela za kumalizia project zenye kipaumbele na taifa zinakosekana na kuanza kubuni njia za kiuni za kukusanya hela kwenye jamii.

Tabia nyingine ni ile unakuta madalali na wafanyabiashara, hasa samaki wakubwa (unaelewa!???) --- anakaribishwa nchini ili ajaribu kuwekeza ila yeye anaishia kutukana tu: anamtukana Rais wa nchi, anavikashifu vyombo vya ulinzi & usalama, anawabeza na kuwabaraguza Watanzania, anaichafua sifa nzuri ya nchi yetu, anabeza na kudhihaki miradi bora ya maendeleo, anakosa maadili na miiko, anachochea maandamano, vurugu, ghasia, fujo, uvunjifu wa amani na hata vita; ni muongo huyoooo hatari na nusu; anapindua na kupopotoa kila kauli nzuri ya Rais na viongozi wenzake wa nchi lengo kujipatia ^cheap popularity.^ Halafu ni muoga huyoooo, eti anawaandamanisha Watanzania huku yeye ameshajifungia ubalozi tayari kusepa zake kwao. Hizi tabia za wafanyabiashara na madalali ni za HOVYO KABISA!!!
 
Tabia hizi ukiziruhusu kwenye biashara yako utaendelea kufanya biashara ya ya kipato cha mkono kwa mdomo tu, hutakaa ukue na kufanya biashara kubwa

1.Kuruhusu watu wasiohusikia na biashara yako kuja kupiga story kwenye biashara yako,hii ni tabia ya hovyo sana ambayo unaweza kuikuta hata kwenye maduka ya madawa ambapo ungetegemea kungekuwa na kuzingatiwa kwa usiri wa wagonjwa kwa kiasi cha hali ya juu.

2.Kushindwa kuuza bidhaa kwa sababu huna chenji.Kama unajua kuna watu watakuja na pesa kubwa nunua hata chenji,usiache kuuza kisa umepewa pesa kubwa,ni ujinga sana.

3.Kujibu wateja vibaya au kuwapuuza

4.Kuchelewa kufungua biashara asubuhi au kumhudumia mteja.

5.Kukosa vifungashio vya bidhaa

6.Kutokowa na bidhaa au huduma ambazo ungetegemewa kuwa nazo.
Very good indeed!!
 
Bila kusahau record(book) keeping na kuzitumia record hizo kufanyia maamuzi .
 
3.Mganga anakupa sharti la kutozichanganya hela za biashara na hela nyingine hapa ni kuwa anakufundisha usiwe jpm ambae kakusanya pesa zote kwenye centralised acc( HAZINA) alafu anazitumia kwenye miradi ambayo haijapitishwa wala kuplaniwa na bunge mwisho wa siku hela za kumalizia project zenye kipaumbele na taifa zinakosekana na kuanza kubuni njia za kiuni za kukusanya hela kwenye jamii.
JPM ana akili sana.
Ngoja nikupe mfano mdogo sana.
Mara zote bajeti inatengenezwa kwa kutumia estimate za mapato yatakayopatikana. Sasa estimate ya mapato kwa mwaka mzima ikawa, kwa mfano, ikawa milioni 100.
Duu! Kufika miezi minne tu! JPM akaona zimeishakusanywa milioni 10,000!! Loooo!!! Hey, hey, hey, Waziri wa Fedha, sasa hivi makusanyo yote Hazina, haraka sana!
 
Walitaka fedha ziendelee kukusanyiwa mashinani ili wazidi kuzikunjua na kuzibungua kama kawa, siyo!???
 
Tabia nyingine ni ile unakuta madalali na wafanyabiashara, hasa samaki wakubwa (unaelewa!???) --- anakaribishwa nchini ili ajaribu kuwekeza ila yeye anaishia kutukana tu: anamtukana Rais wa nchi, anavikashifu vyombo vya ulinzi & usalama, anawabeza na kuwabaraguza Watanzania, anaichafua sifa nzuri ya nchi yetu, anabeza na kudhihaki miradi bora ya maendeleo, anakosa maadili na miiko, anachochea maandamano, vurugu, ghasia, fujo, uvunjifu wa amani na hata vita; ni muongo huyoooo hatari na nusu; anapindua na kupopotoa kila kauli nzuri ya Rais na viongozi wenzake wa nchi lengo kujipatia ^cheap popularity.^ Halafu ni muoga huyoooo, eti anawaandamanisha Watanzania huku yeye ameshajifungia ubalozi tayari kusepa zake kwao. Hizi tabia za wafanyabiashara na madalali ni za HOVYO KABISA!!!
Huwa nasikitika sana nikiona Uzi wa biashara serious kama huu,then mtu kama wewe na mwenzako aliye tangulia,mnaanza kupenyeza vi-sound vya kisiasa..Nendeni Kule jukwaa la siasa mkamalize mihemko yenu,hapa tunazungumzia biashara.
 
Safi sana, inakera mnooooo!!!
 
Kutaka kununuwa kitu halafu waambiwa hakuna, huku anaeuza duka anapiga zogo, cheza draft au kucheza na simu tu!
 
Kuna watu wanaenda kwa waganga wanapewa mbinu zinazoendana na hivi hivi na baadaye wanafanikiwa na wanazidi kuamini kwenye ushirikina.

Mfano:
1. Mganga anakupa dawa unaweka kwenye draw anakuambia iyo dawa asione mtu yoyote. Maana yake mtu yoyote asiguse pesa kwenye draw yako hivyo hutakuwa na upotevu wa pesa.

2. Mganga anakuambia fungua duka saa 1 na uwe wa mwisho kufunga kulinganisha na majirani zako.

Na mengine mengi
Ujinga wa mtanzania na Africa Kwa ujumla umejikita hapa
 
Ujinga wa mtanzania na Africa Kwa ujumla(Except south Africa) umejikita hapa
Aise SA ndiyo wanaongoza kwa ujinga huo, kina SANGOMA! Kumbuka wakati UKIMWI ulivyokuja juu, masangoma waliongoza kwa kushauri wanaume watapona wakiwabaka watoto wa kike walio wadogo kabisa!
Sijuwi lina tutaacha huu upuuzi?!
 
Back
Top Bottom