Ninadhani wewe ni mmoja wa wanaoamini kuwa binadamu wote huwaza sawa. Au anayeamini kuna njia moya TU ya kufanya jambo fulani.
Ni kweli nimesikia mambo hayo yakipingwa lakini SIO umuhimu au uwepo wake. Kuoinga kumehusu jambo moja - CHANZO CHA FEDHA!! Wakati tukiambiwa “fedha zetu za ndani” watu wengi waliaminishwa ni makusanyo ya mapato ya ndani. Kumbe walimaanisha mikopo kwa kuwa tutailipa wenyewe basi ni fedha zetu!!
Wengi wa waliopinga walitaka au PPP model au mikopo ya riba nafuu. Tukachukua mikopo ya kibiashara kwa sababu tulikuwa tunaambiwa watoa riba nafuu ni “mabeberu”.
Binadamu wana mawazo tofauti tofauti. Hatuwazi sawa. Hata hao usiotaka wapingwe wanawaza tofauti na wapinzani wao! Haina maana kuwa wako sahihi au sio sahihi. Acha kuwaona wako sahihi ndio utaelewa umuhimu wa kuwa na fikra tofauti!!!