Tabia ya kutegea kulipa bili

uajekundu

JF-Expert Member
Jan 14, 2016
541
461
Habari zenu wana jamvi,

Kuna tabia inakera sana utakuta umetoka lunch au dina na watu unaofahamiana nayo. Muda wa kùla ama kunywa chochote anaagiza tu tena vya bei kubwa bili ikija anajikausha mchange nyie alafu cha mwisho kinachobakia kidogo ndio alipe yeye.

1. Sipendi tabia ya bili kwa kuchangia.
2. Ni bora kila mtu alipe kulingana na alichokula hata kama mmekaa wote.
3. Wahudumu waache tabia ya kuchanganya bili, wampe kila mtu yake.
4. Tabia ya kujivunga wakati wa kulipa bili sio nzuri kabisa.

Je wewe unaonaje?
 
Wazungu hua wana utaratibu mzuri sana, ambao mimi nimeamua kuiga. Mnapoenda restaurant ama sehemu yoyote basi kama yupo vzr atasema - feel free to order. Bill ikitoka atalipa kila kitu bila hiyana. Pia km hakujiandaa vzr basi atasema - I will pay for 1, na anamwambia waiter/waitress 'separate orders please'. Hapo inabidi ujiandae kujilipia, km hauna ela unashinda njaa.

Sisi kilichotuharibu ni fikra za ujamaa. Haiwezekani wewe siku nzima upo juani unahenyeka, jitu jingine lipo kivulini linakula kiyoyozi, afu jioni ikifika wote mnakula pamoja jasho lako.
 
Namba mbili ndio mwendo.

Ni vizuri kama mmezoeana kuelezana mwanzoni jinsi mtakavyolipa, hii ni haswa hapa nchini.
Kuna kwingine wala mtu huambiwi unajua unaloweka mdomoni ni juu yako labda ujieleze mengine. Unapochagua kwa menu unajipigia mahesabu, sio kusubiri kuhesabiwa na muhudumu....

Ila hapa nchini najua inafanyika, mfano mimi na wanaonizunguka ndio zetu. Hivyo no purukushani za watu kununa, pia wakati mwingine kila mtu anatoa pesa na mmoja anasema rudisheni nalipa yote...maisha yanasonga kwa furaha sio chuki.
 
Wazungu hua wana utaratibu mzuri sana, ambao mimi nimeamua kuiga. Mnapoenda restaurant ama sehemu yoyote basi kama yupo vzr atasema - feel free to order. Bill ikitoka atalipa kila kitu bila hiyana. Pia km hakujiandaa vzr basi atasema - I will pay for 1, na anamwambia waiter/waitress 'separate orders please'. Hapo inabidi ujiandae kujilipia, km hauna ela unashinda njaa.

Sisi kilichotuharibu ni fikra za ujamaa. Haiwezekani wewe siku nzima upo juani unahenyeka, jitu jingine lipo kivulini linakula kiyoyozi, afu jioni ikifika wote mnakula pamoja jasho lako.
Huu ni ustaarabu wa kawaida tu. Hauhitaji Uwe Mbantu,mjapani,Mzungu wala muhundi mwekundu. Achana na fikra za koloni mgando ya kwamba kila afanyalo mzungu yuko sahihi.
Huu ni ustaarabu wa kawaida Kama unavyoenda Chooni ukajitawaza na Maji wakati hao jamaa zako "wazungu" wanajipangusha na makaratasi.
Jitafakari Msomi.
 
Habari Zenu wana jamvi,
kuna tabia inakera sana. utakuta umetoka lunch Au Dina na watu unaofahamiana nayo. muda wa kùla ama kunywa chochote anaagiza tu tena vya bei kubwa. bili ikija anajikausha mchange nyie Alafu cha mwisho kinachobakia kidogo ndio alipe yeye.
1. sipendi tabia ya KULIPA bili kwa kuchangia
2.ni bora kila mtu Alipe kulingana na alichokula hata kama mmekaa wote
3. wahudumu waache tabia ya kuchanganya bili, wampe kila mtu yake.
4. tabia ya kujivunga wakati wa kulipa bili sio nzuri kabisa.
Je wewe unaonaje??
Nafikiri kuna baadhi ya Wahudumu huwa wanafanya kusudi kwa kuleta bill pamoja inawezekana ni Uvivu au kwa malengo ya kupiga cha juu hapo. Kuna sehemu hapa Dar huwa nikienda tukiwa pamoja na marafiki mnapokuwa tayari kulipa,mhudumu huwa anauliza niunganishe bill pamoja au kila mtu na yake?
Ikitokea Kama haujaulizwa na mhudumu nafikiri ni wajibu wako pia kumueleza hiyo bill ailete tofauti.
 
Haaahaaa, watu hawana ustaraabu kabisa.

Siku moja nikiwa stand nikamsikia mpiga debe mmoja anamhadithia mwenzake, leo nimeenda kwa mama ntilie kunywa chai nikamwambia rafiki yangu twende tukanywe chai nitakununulia. Kufika nikaagiza Kikombe cha chai ya rangi na andazi moja. Jamaa yangu yeye si kaagiza pande la supu ya kuku na chapati tatu.., Mpiga debe akasema alilipa kikombe chake chai ya rangi na andazi akasepa akamwacha kwenye mataa.Nilicheka sana wee umeenda na mtu kwa ofa angalia basi hata anaagiza nni ili ujue mfuko wake umefika wapi,

Nakumbuka sana clip ya yule mkenya aliyeenda dating na mdada kaatarifu kampani yake kwenda kufanya kufuru...Haaaaahaaaa ukikutana na kauzu ni mwendo wa kujisoti kavyako vyako.. ujamaa hamnaga kwenye hela...
 
Kuna wengine wana tabia ya kusema,
'nilipie nitakurudishia hela yako baadae' lakini hapo hesabu maumivu hiyo hela hairudi!
 
kuna mgahawa nilienda kunywa supu kipindi nasubilia chenchi yangu akaja jamaa mpiga mizinga wa mjini kunisabahi na kunichombeza chombeza basi wale jamaa wa jikoni wakakausha kwanza kunirudishia chenchi muda ule mpaka yule jamaa alipoondoka...dah niliwashukuru mno watu wa jikoni mana ndo ilibakia ya ngama na usawa wenyewe wa Magufuli huu
 
Mimi huwa nasoma menu naagiza kabisa na kulipia chakula changu nikimaliza nabaki nawaangalia wanavyotegeana kulipa
I see, nadhani mimi na wewe tumechongwa kutoka kwenye mti mmoja. Mimi huwa naiandaa kabisa pesa yangu, naagiza nikiwa nimeishika na nina uhakika kuwa inatosha. Akileta tu chakula anapewa hela yake, ili hata nikitaka kuondoka nisibughudhiwe...
 
Bosi umekumbuka kumwelimisha huyo mhudumu? halafu na wahudumu kama wewe ni wa kwanza kukaa kwenye meza anajua wengine wote wanaokuja kwenye hiyo meza unawalipi... hatari sana
 
Mimi kusema ukweli Mtu akinikumbusha Eti twende tea/lunch...bill lazima atalipa yeye maana Sipendi kualikwa alikwa.Kama vipi tuwe tunakutana tuu Canteen kila mmoja na 50 zake.
 
Huu ni ustaarabu wa kawaida tu. Hauhitaji Uwe Mbantu,mjapani,Mzungu wala muhundi mwekundu. Achana na fikra za koloni mgando ya kwamba kila afanyalo mzungu yuko sahihi.
Huu ni ustaarabu wa kawaida Kama unavyoenda Chooni ukajitawaza na Maji wakati hao jamaa zako "wazungu" wanajipangusha na makaratasi.
Jitafakari Msomi.
....Mapovu ya nini sasa? Anachosema ni kweli bili ikija badala ya kuigawa ili kila mtu alipe kuna wengine wanachuna tuu . Wazungu hawana hizo.
 
Hii issue inakuja sababu sisi nj watu wa aibu, hatuwezi kumpa mtu ukweli kwamba mimi nalipa tu nilicho kunywa/kula.

Sasa tabia hiyo ina sabaabisha ukitoka hapo ni una jilaumu kwa bajeti yako kuharibika.

Ila ukiachana na hilo pia kuna watu wana makusudi, mshikaji wako kabisa ila mkienda canteen wewe kila siku ndio ulipe yeye aah hana habari... Ukiagiza mbuzi naye kala mbuzi, ukila andazi kala andazi...

Mi yashanikuta sana, bora uchomoke mwenyewe tu mkutane mezani umeagiza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom