Tabia ya kusifia watawala

Tabia ya kusifia watawala

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
3,193
Reaction score
6,149
Habari zenu wakuu

Sijajua namna bora ya kuwasilisha jambo hili ambalo kimsingi ilianza taratibu na sasa imekuwa kama tabia na imeshazoeleka.

Ningependa kufahamu kutoka kwa ndugu zetu mliokula chumvi kidogo tunaomba mtujuze,Tabia hii ya kusifia watawala muda wote ilikuwepo tokea enzi za Nyerere?

Kwa sasa imeshazoeleka
akisimama diwani atasifia sana (wakati mwingine mpaka kupitiliza)

Akisimama Mbunge ndio kabisa!
Akisimama Mkuu wa mkoa atasifia sana!
Akisimama Waziri ndio kabisa kila baada ya maneno mawili matatu lazima utasikia akimtaja na kusifia uongozi wa juu.

Wengine wanafika mbali kusema kiongozi fulani amemwaga mabilioni katika mradi fulani!

Tunafahamu sio jambo baya kwa kiongozi kusifiwa pale utendaji wake unapokuwa makini na amefanya vizuri.Lakini Je, Hiyo ndiyo kazi wananchi tuliyowatuma?

Wananchi wanahitaji kusikia mipango na mikakati ya viongozi wao katika kuwahudumia na walipofikia katika kuwahudumia wananchi! Sio utii wao kwa viongozi wa juu!

Walau ingekuwa sawa kama uchaguzi upo karibu maana ingekuwa ni mbinu ya kuvutia wapiga kura,Lakini kwa sasa uchaguzi bado lakini ni wazi kwamba tunaishi kana kwamba tupo katika kipindi cha kampeni!
 
Back
Top Bottom