Tabia ya Kurithishana madaraka inaivunja CCM.

Tabia ya Kurithishana madaraka inaivunja CCM.

mutate

Member
Joined
Mar 12, 2014
Posts
7
Reaction score
1
Sina shida na haki ya mtu ya kidemokrasia ya kugombea au kuchaguliwa au kuteuliwa, au hata kuajiriwa katika nafdasi yoyote hile. shida yangu ni haya mazingira ya kurithishana nafasi katika utumishi wa umma kwa mgongo wa chama na familia. katika uchanguzi mkuu 2010 suala hili lijitokeza majina ya vijana ya waliona nyadhifa serikalini.

tulishuhudia Bumbuli, lakini pia katika uchaguzi mdogo wa Arumeru, sasa Kalenga na Chalinze. CCM vijana msipo angalia hili mnakwenda na maji
 
Kwa kuwa watoto wa Karume, Malima, Mwinyi, Kawawa nk wametoka kwenye familia ambazo baba zao walikuwa marais au mawaziri, basi nao wanapewa vyeo si kwa kuwa wana uwezo ila ni kwa kufuata jina la mzazi. Na sasa ni zamu ya Ridhiwani na Geofrey Mgimwa!!
 
achenni watu watengeneze Chaniel za Maisha kwenye Familia zao .. hata nyie mnaoponda mtakuta mko kazizini au idara fulani nyeti coz of channiel ya familia ..

lakini pia kama kwa bahati mbaya haupo kwenye system yeyote .. basi usilaumu .. that is how life goes .. .

Kesho keshokutwa , mtoto anakuja kuanza kumwambia Baba acha niwe pumbafu ... ulikua mdarakani hakuna kitu umenifanyia ... so all blames on you ...
na nyie washangiliaji hamtakosekana ...mkisemma Lile lizee nilifala ...yaani na vyeo vyote hivyo hakuna alilofanyia watoto wake ..

So Zip ur Mouth .. !
 
Safari hii CCM hawamtumii tena mkapa kama walivyomtumia kule Arumeru Mashariki? Au wanaogopa kumdhalilisha tena?
 
Ndani ya ccm kuna matabaka ya watawala na watawaliwa! Watawaliwa kazi yao ni kuwapigia kampeni watawala huku wakipewa wali, vipesa vidogovidogo ili watawala wapate ubunge, udiwani na hata urais! Baada ya uchaguzi watawaliwa hupigika kimaisha huku watawala wakiishi kama wako peponi! Pia ndani ya ccm watoto wa vigogo huzawadiwa vyeo katika sehemu mbalimbali kuanzia chamani mpaka serikalini!
 
Chama kinajengwa na watu na sio propaganda .
 
Kwa vile wanapata madaraka ya ubunge kwa "uchaguzi na wanapewa kura za ushindi na raia", sidhani kama kuna tatizo hapo kwani nao ni raia kama mimi na wewe. Tatizo ni pale upatikanaji wa madaraka hayo unakuwa unaingiliana na madaraka ya wazazi wao. Hata hivyo mtu wa kulaumu kutokana na wabunge wote tulio nao ni wewe mpiga kura hasa iwapo unadhani kuwa ni kwa sababu ya majina yao tu. Ungelalamikia majina kama ya akina Mwinyi na Nnauye "walioteuliwa" huenda kutokana na majina ya wazazi wao lingekuwa ni jambo jingine.
 
Ili kulinda heshima yetu tusio kwenye mikondo ya kurithishwa ni kuwakuwachagua kabisa kama walivyofanya Arumeru mashariki.
Kama CHADEMA watashinda Kalenga,litakuwa ni somo kwa hawa mizigo
 
Jamani me nashangaa hii nchi kama ya kifalme...kwel 2napoteza dira..
 
Ninaowahurumia ni vigogo wa CCM wasipoamka watamalizwa na watoto wao ili warithi nafasi zao. Ikiwa Mgimwa na Ritz wakipata tutashuhudia vifo vingi vya vigogo wa CCM baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 kama mauwaji ya vikongwe kanda ya ziwa ili watoto wao warithi ardhi.
 
Hii tabia inanifanya nijiulize swali,kuwa watanzania kwanini tuaanza kupelekwa na hawa mabwana kama vile gari bovu?
Hivi inawezekanaje wakarithishana ubunge na vyeo vingine kwa staili ya kulipana fadhila?
Ndugu zangu wa tanzania tuwakatae hawa maimla wa c.cyem na utawala wao.
Inmetosha sasa!

"chadema ni mpango wa 'allah'"
 
ili kulinda heshima yetu tusio kwenye mikondo ya kurithishwa ni kuwakuwachagua kabisa kama walivyofanya arumeru mashariki.
Kama chadema watashinda kalenga,litakuwa ni somo kwa hawa mizigo

napiga sala zote kwa siku ili ushindi wa chadema kalenga uwe wa kishindo.
 
Mtazamo wangu sioni tatizo ilo lipo sana na si kwa siasa tu hata ktk taaluma zingine, yote yanatokana na jinsi ulivyokulia na hasa kufuata wazazi kwa mf. utakuta baba mwanajeshi mtoto tangia anakua yuko kambini naye ana adobt kiasi anaweza kujiita mie kamanda nitakuwa kama baba anakuwa kajijenga vile na baba anakua si rahisi kumrekebisha ikiwa nae anapenda, au Familia ya matumla wamekuwa ktk mazingira hayo hayo, familia ya Zahiri Zahoro, familia ya mwamunyange kuna familia nyingi tu zina fani moja wote hata kwenye mpira, na si Tanzania tu mf. familia ya bush ameiga ktk kwa baba yake, hivyo hivyo kwenye siasa wapo katika familia hizo za viongozi wanasiasa na wengine hawataki kusikia sias ktk maisha yao wanataaluma zao hayo inatokana na jinsi yule wa kwanza amefanikiwa au la hata mimi nijitolee mfano baba yngu alikuwa mchezaji mpira na ndg zangu wawili wapo wanacheza mpira uarabuni si kwa kiwango kile cha baba lkn wamethubutu na wameona hailipi wameachana nao.
 
Vijana nawashauri tusikubali huu usultani. Tujiandikishe na kujitokeza kupiga kura, kila mmoja aongozwe na dhamira yake, ukipewa rushwa kula, lakini usiruhusu mtu ajue msimamo wako, kura ni siri, hakuna atakaekuja kukudai kofia na fulana aliyokupa, hata baada ya kumnyima kura huyo aliekupa rushwa, wewe endelea kuvaa hiyo fulana na kofia bila kinyongo. tusipozuia hili ile falsafa ya "CCM ina wenyewa na wenyewe ni sisi" itadumu milele. vijana tusilale tuchukue hatua,
 
Akajiandikishe wapi wakati Daftari la wapiga kura lina kinga ya kutofanyiwa editing?Haujamsikia Mwenyekiti wake?Ila ilinishngangaza kusikia la Kalenga lilifanyiwa marekebisho 2014,ikabidi nianze kuona kuna something fishy imefanyika huko Kalenga sasa sijui wapinzani walisemaje?:A S confused:
 
CCM aliyoiasisi Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1977 ilishakufa na kuzikwa naye mwaka 1999. CCM ya sasa ni club ya wanafamilia na marafiki zao inayojiendesha kwa kivuli cha chama cha siasa
 
Sina shida na haki ya mtu ya kidemokrasia ya kugombea au kuchaguliwa au kuteuliwa, au hata kuajiriwa katika nafdasi yoyote hile. shida yangu ni haya mazingira ya kurithishana nafasi katika utumishi wa umma kwa mgongo wa chama na familia. katika uchanguzi mkuu 2010 suala hili lijitokeza majina ya vijana ya waliona nyadhifa serikalini.

tulishuhudia Bumbuli, lakini pia katika uchaguzi mdogo wa Arumeru, sasa Kalenga na Chalinze. CCM vijana msipo angalia hili mnakwenda na maji

- Yaaani naomba kuuliza inyovunjika ni CCM au Chadema, maana mara ya mwisho uchaguzi wa Madiwani si walioshindwa ni Chadema kwa kata 23 kwa 3, sasa anayevunjika hapa ni nani hasa unless kuna something sielewi, kama ni kurithishana nani anaweza kumfunga mwenziwe kengele au mleta mada na yeye amefundishwa siasa za makengeza za huko upande wa pili, hajaona jinsi Tundu Lissu na dada yake na mwanamke aliyezaa naye wote wakiwa wabunge wa Chadema, I mean mleta mada kajipange tena huna ishu if anything wanaovunjika ni chama chako Chadema,

Le Mutuz
 
Ndani ya ccm kuna matabaka ya watawala na watawaliwa! Watawaliwa kazi yao ni kuwapigia kampeni watawala huku wakipewa wali, vipesa vidogovidogo ili watawala wapate ubunge, udiwani na hata urais! Baada ya uchaguzi watawaliwa hupigika kimaisha huku watawala wakiishi kama wako peponi! Pia ndani ya ccm watoto wa vigogo huzawadiwa vyeo katika sehemu mbalimbali kuanzia chamani mpaka serikalini!

Sisi wapiga kura wetu tunawafurahisha kwa khanga,vitenge,kofia,fulana na skafu.zote zikiwa na rangi ya kijani na njano,tena uchaguzi ujao tutaanza pia kuwapa sabuni za kufulia kwani tumegundua wengi hawana uwezo wa kununua mche wa sabuni kwa matumizi ya kufulia.
 
Hili sioo jimbo la kifalme kwanza baba yake kashindwa pamoja na uwaziri wake ataweza nayo mtoto tena anaonekana kama domo zege.
 
Back
Top Bottom