Wisest man
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 993
- 332
Nimegundua kuna tabia ambazo huwa zinawakera watu wengi ila wanashindwa kuzisema kwasababu aidha ni kuona muhusika anaweza asielewe/kupuuza anachoambiwa au kumpotezea mhusika kwa kumchukulia kama chizi au mtoto asiyeelewa anachokisema kwa kuangalia mazingira aliyopo.
Ni hivi, kuna wakati unajikuta uko na watu tuseme ni marafiki au mnafahamiana tu ila sio sana kiasi cha kuanza kuongea mambo yako binafsi kwa sababu ya kutoona umuhimu wa kufanya hivyo halafu anatokea mtu mmoja katika ya watu anaongea kitu anachodhani ni utani kwako ili tu kujenga mazingira ya kufurahisha hadhira, tena unakuta wewe mwenyewe sio muongeaji mbele ya watu hasa wale usiowafahamu ila unakuta mtu anaingilia uhuru wako wa kukaa kimya au kutosema chochote chako kwa watu. Tabia hii nimegundua ndio inayowafanya watu wapotezeane kimya kimya bila kuambiana.
Unakuta mtu mkiwa wawili, labda ofisini au hata mmekutana sehemu anaongea vizuri tu ila wakitokea watu wengine anaanza kuongea upuuzi tu. Watu wenye tabia hii hata JF wapo, mnatakiwa kubadilika na kuhakikisha mnaheshimu uhuru wa wengine. Kukaa kimya kuna maana yake, sio kila kitu ni kuongea tu, na siri tabia hii imekithiri kwa wanaume.
Acheni kulazimisha mazoea kwa watu wasiopenda mazoeano ya kijinga.