Tabia ya kununua Vitu vya wizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabia ya kununua Vitu vya wizi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mjasiria, May 28, 2012.

 1. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Habari zenyu bana,Natumaini kwa uwezo wake manani, tuko salama. Pia napenda kuchukua fursa hii kuwapa pole watanzania wote waliofikwa na masaibu ya kunyanyaswa huko visiwani kwa kuwa tu wao ni watanganyika. Watanganyika hawa wamenyanyaswa na kudhalilishwa na watanzania wenzao. Ni jambo la kusikitisha na kulaaniwa kwa nguvu zote. Pili leo ningependa kuzungumzia hili suala la sisi watanzania kupenda kununua vitu vya wizi hasa simu, laptops, kamera, redio na vifaa vingine vya magari na vingine vingi. Kwa uzoefu nilionao tabia hii inasababishwa na urahisi wa bidhaa hizi. Yaani unaweza kukuta mtu na akili zake timamu anaazimia kwenda kutafuta simu kwa teja, akijua wazi kuwa itakuwa imeibwa mahali fulani. Halafu baadaye mtu huyuhuyu akija kuibiwa yeye unakuta analalamika sana. Tunashindwa kuelewa kuwa kwa kuendekeza kwetu tabia hii ya kununua vitu vya wizi ndivyo inavyofanya tabia ya wizi kukoma kuwa ngumu sana.Kifupi ni kuwa kama watu wote tutaacha kununua vitu vya wizi ni wazi tabia ya wizi itapungua sana kama si kukoma kabisa. Nina mfano hai wa hiki ninachokizungumza, Kuna baadhi ya nchi ni vigumu sana kwa mtu kununua kitu chochote kama hakina risiti inayoonesha ni wapi ulinunua na kwa bei gani. Japokuwa ni kweli ni rahisi kutengeneza risiti lakini utaona kuwa raia wa nchi hizo wamejiwekea utaratibu ambao unajaribu kukwepa bidhaa za wizi kwa nguvu zote. Matokeo yake katika nchi ni vigumu sana kukuta mtu anaibiwa simu au sijui TV.Hivyo basi wadau wa JF leo ninatoa wito, tuache na tuwaase wenzetu kuacha kununua bidhaa za wizi mtaani. Hii itasaidia sana kuondoa tatizo la wizi.Jumatatu njema.
   
 2. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Ahsante kwa darasa zuri.
   
 3. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kutuelimisha ,kwani imefika mahali watu wanajisifu kununua vitu vya wizi kwa bei rahisi na kusababisha wizi kuendelea
   
 4. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,211
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Lakini kwa nini twapenda vitu vya bei rahisi?
  Labda kipato kidogo!
  Kwanini hatuogopi vya wizi?
  Labda imani yetu dhaifu!
  Na wezi twawajua lakini kwanini wanaendelea kuwepo tu uraiani?
  Labda ni facilitator wa madili ya wakubwa!
  Ila tuache hii tabia nashkuru Mungu mimi sijawah kuwa nayo!
   
 5. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,486
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Ifikie sehem tuchukie wizi kutoka moyoni huwezi ukawa unachukia wizi wakati huohuo unanunua vitu vya wizi.
   
Loading...