Elections 2010 Tabia ya baadhi wa weneviti kamati za bunge kuingilia kazi za serikali - wanataka wao wawe mawaziri?

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,198
Hivi karibuni tulimsikia mwenyekiti wa kamati ya tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh. Lyatonga Mrema akitoa adhabu kwa Halmashauri ya Rombo. Kwa sheria hii ni kinyume na ni nje ya mamlaka ya kamati za bunge. Sasa, January Makama ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya nishati na madini nae anaokana kuiga mtindo huu wa Mrema.

Kiutendaji kazi za hizi kamati za bunge ni kusimamia utendaji wa serikali. Hivyo kamati zinatakiwa ku-report mapungufu wanayoona Bungeni na sio kwenye vyombo vya habari. Hata kama ni adhabu wao wanatakiwa watoe kama mapendekezo, maana hawana mamlaka kesheria ya kutoa adhabu. Hawana. Nimemuona January TBC1 akisema maneno kama "serikalini kuna vacuum'!!! unbelievable. Kwa nini asiende kwa spika ambako kimsingi niko anatakiwa kureport na akatoa malalamiko yake huko? Tena kimaandishi ili kuweka kumbukumbu.

Hii si mara ya kwanza January kujaribu kuonesha yeye ana 'silver bullet' kuhusu hali ya umeme Tanzania. Siku chache kabla ya kupata hicho cheo cha uenyekiti alimwandikia barua Ngeleja, na kwa kutumia ujanja ambao unatumika sana nchi za magharibi hususan Marekani barua hiyo ilikuwa leaked to the media. January hakukanusha wala kusema chochote kuhusu barua hiyo ilifikaje kwenye media. siku chache baadae ameenda Bungeni akapata uenyekiti wa kamati ya wizara hiyo aliyoindikia barua. Kwangu mimi naona January anataka sana kuwa kwenye cabinet, na anaonekana kutumia kila opportunity anayopata just to undermine Ngeleja pengine kwa matumaini ya kupata hiyo nafasi?
 
Back
Top Bottom