monaco
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,184
- 1,780
Habari ya jumapili wadau,poleni na kwaresma,Namshukuru Mungu san asana kwa siku hii ya leo,na somo la leo.Basi yesu akawaambia na asie na dhambi kati yenu aanze kumpiga mawe,hakuna alie jaribu kumpiga Yule mama mzinifu,wote wakatokomea kasha Yesu akamwambia usitende tena Dhambi ,ondoka nenda zako.
Anyway ..leo ntazungumzia tabia za watu,Je
KUNA AINA 2 ZA TABIA YA MTU.
1. Aina ya Tabia A (Type A Personality)
2. Aina ya Tabia B (Type B Personality)
Tabia A.
1.Watu hawa huwa ni watu wa kwenda mbele,kusonga daima mbele
2.Hawana subira na uendaji wa matukio yeyote yanayotokea.
3.Wanafikiri zaidi na kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja
4.Hawawezi kuendana na muda wa kupumzika
5.Wana mtazamo hasi na namba
6.Hutamani haraka majibu ya walichofanya ili kupata feedback
7.Wana kiu.
Wanapenda kupimwa mafanikio yao kwa kiasi Fulani au kwa vitu vingapi wamefanya.
Tabia B.
1.Hawa huwa hawaumizwi na muda,hawana haraka.
2.Huona haina haja kutoa, kusema mafanikio yao,labda kuwe na uhitaji,ulazima wa kufanya hivyo.
3.Wanafanya vitu kwa kufurahi,na kujiridhisha,na sio kwa kutaka makuu au kwa Gharama Fulani.
4.Wanaweza kupumzika bila shinikizo au msongo wowote.kwao kupumzika ni muda wowote.
Kwa ujumla: Tabia A,(TYPE A PERSONALITY) wanaweza kufanya kazi kawaida na kazi za usumbufu.wanajitengenezea wenyewe mwisho wa majukumu yao/malengo.mfano hawa ni watu wa haraka,kwasababu wanapenda idadi zaidi ya ubora(Quantity than Qulity) wanajionesha kwa kufanya mambo/kazi muda mwingi zaidi.Hutegemea zaidi uzoefu wa matukio wanapokumbwa na matatizo.Tabio zao ni Rahisi kutabiri kuliko Tabia B (Type B Personality)
Kwa mtazamo tu,marafiki/wapenzi yawapasa wawe tofauti kitabia ili wavumiliane,pungufu la mmoja lizibwe na mmwingine.ili kusiwe na kushindana kama mafahali au kuwa aina moja tu.JE WEWE UNAONAJE?