Za siku nyingi wakuu?
Mimi mzima bhana japo tuhoma twa hpa na ple hatukatiki mwilini ila Mungu bado ananipa uhai. Alhamudulillah..
Lengo la uzi huu sio kujisifia wala kuudhi watu humu. Ninataka kuwatia moyo vijana, hasahasa wa jinsi ya kiume ili waendelee kuwa na tabia nzuri kama yangu maana inalipa
Mimi huwa sivai mitepesho, huwa sigongi mademu hovyo kama mbwa.( Sifanyi uasherati kabisa, msinielewe vibaya) Huwa sivuti bhangi wala ugoro kama vijana wengine
Mi nasali, kila Jumapili huwezi nikosa kanisani. Kwa kifupi ni kijana wa kuingwa mtaani na kijiji chetu kwa ujumla
Juzi bhana mzee mmoja tajiri wa Mkoa mzima alikuja nyumbani kuniulizia. Bahati mbaya sikuwepo maeneo ya home, nilikuwa zangu kanisani kwenye mazoezi ya kwaya. Maana mi muimbaji mzuri sana wa sauti ya nne. Kanisani wananiita bufa ya injili.
Ngoja nisiwalotezee muda wenu, nimalizie kwa kusema kuwa tabia Njema inalipa.
Kwa kifupi, nimepewa Zawadi ya mke. Mwezi wa 10 kama hali itakaa vizuri atatoka masomoni Norway na ndoa yetu mwaka huu huu.
Jana mzee amenitumia picha zake...aisee huyu binti kaumbika.
TABIA NJEMA INALIPA.