Tabia Mbaya za Watanzania; Tubadilike

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Ndugu Watanzania wenzangu, salamu kwenu.

Leo ninaomba tutafakari matukio/mambo yafuatayo:

1. Usafiri wa pantoni ndio usafiri tegemewa kwa wakazi wengi wa Kigamboni kuwaunganisha na sehemu nyingine za Dar es Salaam. Asubuhi na jioni foleni inakuwa kubwa sana. Hapa sasa utawaona wababa na wamama wenye heshima zao, mabrazameni na masista duu na wananchi wa kawaida wasiokuwa wazee sana, hawana ulemavu wowote wala hawana watoto wadogo waliombatana nao na sio wajawazito. Utawasikia "kaka naomba unikatie na Mimi".

Hapa maana yake ni kuwa mtu huyu anavuka foleni ya watu waliojipanga kwaajili ya kukata tiketi, moja kwa moja anakwenda kwa watu ambao tayari wapo karibu na kukata tiketi. Hakuna analalamika na ukijaribu kuingilia basi wewe ndio unashambuliwa kwa kuonesha tabia tofauti. Mara nyingi utasikia "kaka huo sio ustaarabu wa Watanzania, sisi ni watu wakusaidiana". Ninashukuru mimi wananitambua na nimeshapeleka malalamiko kwa mamlaka husika zitoe elimu kwa abiria.

2. Ukienda kupanda mwendokasi, kuna hali inayofanana na hiyo ila kwenye mwendokasi kuna nafuu kulinganisha na pantoni. Muda wa kuingia kwenye basi watu husukumana kama ng'ombe na wengine kuumia na kuibiwa. Hili nimelilalamikia sana na kulifikisha kwa viongozi husika. Sasa hivi Kuna utaratibu wa foleni japo hauzingatiwi muda wote. Hongera nyingi kwa kituo cha Kimara mwisho. Wako vizuri.

3. Kwenye harusi Mara nyingi (sio sehemu zote) chakula huliwa mara baada ya watu kutoa zawadi. Wazoefu wa kamati za harusi wanajua hili. Watu wakila shughuli imeisha, wanasepa. Lakini chunguza hata kwenye chakula na vinywaji. Watu wa huduma za chakula au wahudumiaji wa vinywaji kwa makusudi kabisa watamuwekea zaidi labda nyama au bia nyingi zaidi rafiki, mkwe au ndugu yake. Hii mara nyingi hutokea kwenye harusi zetu za bajeti ndogo. Anayepewa vitu hivyo kwa wingi mpaka mara nyingine kupelekea kukosa, nyumbani kwake ameacha hivyo vitu kwenye friji.

4. Watoto wetu, kaka na ndugu zetu wanapopata nafasi nzuri ya kazi basi jamaa na ndugu zake humsonga kwa maneno mengi kuwa huo ndio wakati wa kuchomeka ndugu zake kwenye kazi au ndio wakati wa kupiga hela (rushwa). Yeyote ambaye hafanyi hivyo hulaumiwa kuwa alipata nafasi akachezea. Mfano halisi ni hayati Mwalimu Nyerere, watu husema alishindwa kujimilikisha mali na kuendeleza kwao kana kwamba hilo ndio jambo la msingi.

5. Ni mara ngapi watumishi hasa wa umma (sio wote) wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea? Unaweza kuta mwalimu anawaambia wanafunzi "kazi hiyo nimetoa, anayetaka afanye na asiyetaka aache, mtajua wenyewe, mimi mshahara wangu uko palepale".

Nimetoa mifano hiyo michache ili tujitafakari sisi wenyewe. Mambo yanapokuwa hayaendi sawa, lawama zote hutupiwa serikali huku tukisahau kuwa sisi Kama wananchi wa kawaida tunasehemu kubwa ya kuleta mabadiliko.

Mifano hiyo hapo juu inaweza kuwa ya kawaida au kitu kidogo lakini inamaana kubwa sana inayoonesha sisi tulivyo. Mtu asiyeheshimu foleni anawasilisha kile kilichopo ndani yake.

Mtaani watu wanamiliki magari ya thamani kubwa lakini hawawezi kujichanga na kuweka makalavati au kuchonga barabara yao. Wanaisubiri serikali. Ukiuliza, wanasema tunalipa kodi.

Tubadilike. Tanzania itajengwa na Watanzania.

Amani Msumari
Tanga
 
Kwani hujui, tumeambiwa mpaka tuwachague ndio tupate Maen deleo bila kujali tunalipa Kodi.
 
Wewe jamaa unaonekana kuwa na gubu sana. Usipobadilika utajikuta unaishi maisha ya peke yako na upweke tu. Sasa huko ferry kama kuna hilo tatizo usilopendezwa nalo la foleni na kukatiana tiketi, si ununue gari lako na upitie kwenye lile daraja la kisasa!

Huko kwenye harusi nako, umelazimishwa kuchangia kadi na pia kuhudhuria? Bora hata ungekua tu mzaramo wa Pwani. Yaani unataka hadi makalavati nayo tujenge sisi!! Wewe ni tatizo.
 
Wewe jamaa unaonekana kuwa na gubu sana. Usipobadilika utajikuta unaishi maisha ya peke yako na upweke tu. Sasa huko ferry kama kuna hilo tatizo usilopendezwa nalo la foleni na kukatiana tiketi, si ununue gari lako na upitie kwenye lile daraja la kisasa!

Huko kwenye harusi nako, umelazimishwa kuchangia kadi na pia kuhudhuria? Bora hata ungekua tu mzaramo wa Pwani. Yaani unataka hadi makalavati nayo tujenge sisi!! Wewe ni tatizo.
Kukimbia tatizo sio suluhisho. Kama mimi nitapita darajani huku ferry bado tabia hiyo itaendelea kuwakera wengine.

Ila ushairu wako nimeuchukua. Nitajichunguza kama nina "gubu" kwani ni kweli huwa nakasirika sana na kuwataka wale Suma JKT na muda mwingine wale wajeda pale waingilie kati. Nimeshafika mpaka kwa uongozi wa pale na kuwaeleza. Inawezekana kweli hili likawa Jambo la kawaida ila kukuta wenzako halafu wewe ndio kujiona una haraka dah!
 
Yap. Kuna muda ujumbe uleule unakuwa na uzito tofauti kutegemegemeana na aliyeutoa. Muhimu kwangu ni kuwa nimetekeleza jukumu langu Kama mwananchi wa kawaida
Hapo yafaa tuuzungumzie na uzalendo, ule maslahi au uzalendo halisi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom