Tabia mbaya 10, zinazofanya ushindwe kuwa na akiba

Joealexist

Member
Jun 1, 2012
21
10
Ndani ya posti hii nimejifunza mambo mengi ya muhimu ambayo yatanisaidia sana katika kuifikia ndoto yangu ya kuwa mjasiriamalimkubwa.
Inaelezea tabia ambazo wengi wetu tunazo, na hizo tabia ndizo zinazopelekea kuamua sisi ni aina gani ya ya watu.
Kumbuka, "Daraja kati ya mtu na malengo/Ndoto ni TABIA yake"

1.Unanunua nguo bila mpangilio..

Kuna watu wana nguo kama duka. Plz Kuwa na nguo chache Tu huwezi kushindana na fashion.

2.Unanunua Viatu bila mpango.

Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea chache zenye ubora ili zidumu.

3.Unatoa ofa bar bila mpango.

Nenda bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakae kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale kwa urefu Wa kamba yake. Jifunze ubepari.

4.Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya sh 7000 au 10000 ili uchati na marafiki Fb au wasaap Huo ni ujinga. Badilika.

5.Unakopa hela benki na kununua vitu kama simu ya milioni na gari ambazo sio productive. Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi Wa kuzalisha ndio ununue gari?

6.Una marafiki wengi ambao ni mizigo kwako au hamuendani kivipato hivyo unajikuta unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili uwa-impress. Meneja Wa TRA na mwalimu Wa sec unatarajia utoe offer mpaka umfurahishe meneja? Utabaki na sh ngapi toka kwenye salary yako?? Zinduka.

7.Huna timetable ya kudumu ya maisha yako, unajikuta unaburuzwa Tu na marafiki zako kwa kwenda sehemu mbalimbali za matumizi.

Kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie kikamilifu, usiburuzwe!

8.Una michepuko inayokutegemea wewe kwa kila kitu. Wanakuita ATM we we unakenua Tu huzinduki. Badilika.

9.Una huruma sana kuliko kipato chako. Yaani kila ukiombwa unatoa hata kama muombaji hana genuine need. Usiwe mkristo kuliko Yesu. Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio kila anaekupiga mzinga unapigika.

10.Unatembea na hela nyingi kwenye wallet au mshahara wote kwenye wallet au handbag au nyumbani kwako. Unapokuwa na petty cash nyingi unatengeneza mazingira ya kutumia hovyo. Jifunze kuweka hela benki. Tembea na hela Tu unayoihitaji kwa matumizi ya lazima.

Naamini tukizingatia kanuni hizi kumi tutaongeza savings zetu na kuwa na mtaji Wa kufanya vitu vikubwa endelevu.
Pia unaweza ukajipatia kitabu hiki kizuri cha Ujasiriamali..
jukwaa la sheria ad.jpg
 
Namba 3,4,5,6,7,8 na 9 ndiyo zinazotuponza waTz wengi.Yaani kuna lifestyle ambazo kuweka akiba au kuwekeza ni haiwezekani kabisaaa..Ila Asahnte kwa orodha..watazinduka sasa!!!
 
sitakaa nifikie malengo bila kuidhibiti no.3

tatizo nikishalewa..........omba unikute nimelewa.

mpaka watu wanavizia nilewe, halafu wanaanza kuhamia mezani kwangu mmojammoja, na mimi natandaza kama sina akili nzuri
 
Ndani ya posti hii nimejifunza mambo mengi ya muhimu ambayo yatanisaidia sana katika kuifikia ndoto yangu ya kuwa mjasiriamalimkubwa.
Inaelezea tabia ambazo wengi wetu tunazo, na hizo tabia ndizo zinazopelekea kuamua sisi ni aina gani ya ya watu.
Kumbuka, "Daraja kati ya mtu na malengo/Ndoto ni TABIA yake"

1.Unanunua nguo bila mpangilio..

Kuna watu wana nguo kama duka. Plz Kuwa na nguo chache Tu huwezi kushindana na fashion.

2.Unanunua Viatu bila mpango.

Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea chache zenye ubora ili zidumu.

3.Unatoa ofa bar bila mpango.

Nenda bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakae kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale kwa urefu Wa kamba yake. Jifunze ubepari.

4.Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya sh 7000 au 10000 ili uchati na marafiki Fb au wasaap Huo ni ujinga. Badilika.

5.Unakopa hela benki na kununua vitu kama simu ya milioni na gari ambazo sio productive. Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi Wa kuzalisha ndio ununue gari?

6.Una marafiki wengi ambao ni mizigo kwako au hamuendani kivipato hivyo unajikuta unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili uwa-impress. Meneja Wa TRA na mwalimu Wa sec unatarajia utoe offer mpaka umfurahishe meneja? Utabaki na sh ngapi toka kwenye salary yako?? Zinduka.

7.Huna timetable ya kudumu ya maisha yako, unajikuta unaburuzwa Tu na marafiki zako kwa kwenda sehemu mbalimbali za matumizi.

Kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie kikamilifu, usiburuzwe!

8.Una michepuko inayokutegemea wewe kwa kila kitu. Wanakuita ATM we we unakenua Tu huzinduki. Badilika.

9.Una huruma sana kuliko kipato chako. Yaani kila ukiombwa unatoa hata kama muombaji hana genuine need. Usiwe mkristo kuliko Yesu. Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio kila anaekupiga mzinga unapigika.

10.Unatembea na hela nyingi kwenye wallet au mshahara wote kwenye wallet au handbag au nyumbani kwako. Unapokuwa na petty cash nyingi unatengeneza mazingira ya kutumia hovyo. Jifunze kuweka hela benki. Tembea na hela Tu unayoihitaji kwa matumizi ya lazima.

Naamini tukizingatia kanuni hizi kumi tutaongeza savings zetu na kuwa na mtaji Wa kufanya vitu vikubwa endelevu.
Pia unaweza ukajipatia kitabu hiki kizuri cha Ujasiriamali..
View attachment 314996

Iko kitabu nakiitaji ila picha aifunguki naomba jina lake pls
 
Back
Top Bottom