Tabasamu la Ukweli😀

Mtoto akiwa na maisha yake ya uhalisia hata tabasamu lake huwa halisi, sio la kufoji.
Maisha haya mtoto akiwa na amani ya rohoni bila nguo za thamani wala toys wala pizza furaha inakuwepo. [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Nature ya maisha ya sasa hivi yamekuwa ya ajabu sana ukimuacha mtoto careless utakachokipata kwa mwanao ni majanga.
Nikweli mkuu maisha yamebadirika sana inahitaji umakini, ila Baba angalau ukiwepo home pata muda wa kumtoa kidogo nje akiwa chini ya usimamizi wako tu.Nilienda kwa jamaa yangu fulani mtoto anaogopa watu wageni maana muda wote yupo ndani
 
Saizi watoto wanaishi mfano wa "Zero Grazing" mtoto hapati muda wa kujiachia muda wote amefungiwa tu
Tunaogopa sana, walimwengu wamekuwa wa ajabu kwahiyo ukitaka mtoto apitie hizo mambo sharti uwe karibu la sivyo ni hatari...
 
Shida tuliipata sisi kajamba nani ambao tulizungukwa na watoto wa kishua, badala ya kucheza tunawafanya watoto wa kishua tv kila wanachokifanya tunabaki kuwatazama na kuwatamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…