Taazia: Dr. Tamim Bushiri

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,191
30,533
DR. TAMIM DAKTARI AMBAE HAKUGOMA MADAKTARI WALIPOGOMA

Nimempiga Dr. Tamim picha nyingi na zote ninazo zipo Maktaba.

Kila picha niliyompiga nilijitahidi kumpelekea nakala.

Tabu iliyonifika ni picha ipi nichague itakayomueleza na kumuonyesha yule ambae hakupata kumfahamu Dr. Tamim katika uhai wake alikuwa mtu wa aina gani.

Nimechagua picha hii Dr. Tamim amekaa kwenye kizingiti cha Msikiti wa Makonde.

Dr. Tamim amekaa kwenye kizingiti cha msikiti.

Ndani msikiti ulikuwa umejaa watu wanasalia maiti.

Ilibidi wengine wabakie nje.

Msikiti wa Makonde juu ya ukongwe na umaarufu wake si katika misikiti yenye nafasi ya kuchukua watu wengi.

Watu wangeamua kufunga safu hadi nje kusalia jeneza ingebidi Mtaa wa Swahili makutano na Msimbazi ufungwe kwa magari na wenda kwa miguu.

Hakuna asiyejua hekaheka ya magari ya kawaida, Mwendokasi, Bodaboda, Daladala katika makutano ya Swahili na Msimbazi.

Dr. Tamim Daktari Bingwa wa Watoto amekaa nje kwenye kizingiti cha msikiti akisubiri jeneza litoke tuelekee mazikoni.

Nimemjua Dr. Tamim tayari mganga yuko Makuti Clinic, Muhimbili akiwa pale na kaka yangu Dr. Mgone.

Kaka yangu ndiye aliyenijulisha kwake na tukawa marafiki ndugu.

Katika taarifa za msiba nilizopokea mapema moja ni kutoka kwa kaka yangu Prof. Mgone.

Hapa Makuti Clinic hapahitaji maelezo kwani baba, mama na watoto wao ambao sasa pengine na wao ni baba na mama hapa wanapajua vyema ama kwa wao kukumbuka kuambiwa na mama, "Ukiendelea na utundu wako nitakupeleka kwa Dr. Tamim akakuchome sindano."

Naamini leo wapo vijana waliokuwa wanatibiwa na Dr. Tamim Makuti Clinic watoto wao baadae wametibiwa na yeye.

Mgomo wa madaktari ulitikisa serikali.

Vyombo vya habari vikapata stori ya kuuza gazeti.

Asubuhi naangalia Daily News habari kuu iliyoandikwa kwa kichwa cha habari kwa wino mweusi uliokoza ni mgomo wa madaktari.

Chini ya kichwa cha habari naona picha ya Dr. Tamim yuko hospitali anatibia wagonjwa.

Dr. Tamim yeye hakugoma.

Nilipokutananae nikamuuliza kwa nini hakugoma?

"Mimi siwezi kugoma kwa sababu wako wale wagonjwa wametoka mbali sana mfano wa Chamazi kabadili mabasi hadi kafika Muhimbili akitegemea tiba.

Hawa ndiyo walionifanya mimi niende hospitali kuwasubiri niwatibu.

Wako wagonjwa nikiwa pale hospitali nawaona wanapoelezwa hakuna huduma wanaingia kwenye magari yao wanakwenda kwenye hospitali za kulipia.

Hawa si watu wa dhiki.

Lakini vipi jamaa zangu wa Manzese Uzuri hawa maskini ya Mungu watakwenda wapi wakinikuta mimi sipo?"

Huyu ndiye Dr. Tamim.

Watu wengi wamepita mikononi mwake kwa kutibiwa.

Aliwapenda watu na watu wakampenda.
Tamim hakuwa mtu wa kujikweza.

Tamim hakuwa mtu wa kujiona.

Tamim alikuwa mtu wa msaada kwa amjuaye na asiyemjua.

Buriani ndugu yetu.
Umeacha jina.

Wengi hawatakusahau.
Mwenyezi Mungu alipanue kaburi lako.

Amin.

1716050745630.jpeg
 
Poleni wote mlioguswa na Msiba huu, mwenyezi Mungu ampungizie adhabu ya kaburi Dr Tamimu...

Kama hautajali Mkuu Mohamed Said ningependa kufahamu urafiki wa Mwl Nyerere na Rashid Kawawa, Kuna mahali nilisikia Hawa Wazee wawili walikuwa marafiki sana enzi za Uhai wao.
 
Poleni wote mlioguswa na Msiba huu, mwenyezi Mungu ampungizie adhabu ya kaburi Dr Tamimu...

Kama hautajali Mkuu Mohamed Said ningependa kufahamu urafiki wa Mwl Nyerere na Rashid Kawawa, Kuna mahali nilisikia Hawa Wazee wawili walikuwa marafiki sana enzi za Uhai wao.
Grahams,
Kuwa Kawawa na Mwalimu Nyerere walikuwa marafiki siwezi kukujibu kwa uhakika.

Siwezi kukujibu kwa uhakika kwa sababu sijui lolote kuhusu urafiki wao.

Ninachojua ni kuwa wote wawili walikuwa pamoja katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Suala la urafiki kati ya watu wawili ni kitu kinachobeba mambo mengi.

Marafiki wa Nyerere wote wanafahamika kutokana na historia baina yao mfano wa Nyerere na Andrew Tibandebage, Joseph Kasella Bantu, Hamza Mwapachu, Abdul na Ally Sykes, Dossa Aziz, Amir Jamal, John Rupia, Mshume Kiyate na pengine wengine ambao mimi sina historia zao.

Bahati mbaya mimi katika kuijua historia ya Nyerere sikumuona Kawawa katika hao niliowataja
hapo juu.

Uswahiba yaani urafiki unaambatana na hisani yaani wema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom